Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 33,894
- 76,810
Kuna nchi hapa Africa zimefanya hivi.Basi kwenye kipindi hiki serikali ichukue hatua kwa:
- Kupunguza kodi... Kwa maana ya PAYE, VAT, Coperate Tax, Income Tax na nyinginezo..
- Miradi mikubwa isimame kwanza, na pesa zielekezwe kwenye kukabiliana na hili janga.
- Pesa zilizonadiliwa kwa uchaguzi, zisitumike huko, badala yake zielekezwe kwenye kukabliana na Covid19
Cc: mahondaw
Kwanza zili-lockdown kabisa huduma zisizo na lazima kama Bars, clubs na mihadhara ya kidini. Ukikosa hizi hautakufa.
Lakini dini walianza na mikusanyiko ya watu 50. Sisi tulikuwa tunaswali kwa sessions...zilikuwa zinaenda hadi tatu.
Baada ya hapo bado wakaona haisaidii.
Walichofanya ni lockdown ya huduma zote na kuacha tu zile za lazima.
-Hauruhusiwi kutoka nje hadi uwe na kibali.
-unapotoka nje mtaani kwako kuna road block. Utawaonyesha polisi kibali watakipiga mhuri...na kibali kitaeleza uendako.
-ukirudi utawaonyesha huduma uliyoifuata na watakugongea mhuri mwingine.
-Makampuni yaliyoathirika yamesaidiwa kwa asilimia 50%....hivyo hayana sababu ya kutokuendelea kuwalipa wafanyakazi.
Hii japo sio kinga ya asilimia 100 lakini inasaidia.