Tetesi: Kuna uwezekano mkubwa wa LOCKDOWN nchi nzima. Kama hujajiandaa fanya sasa

Status
Not open for further replies.
Kuna nchi hapa Africa zimefanya hivi.

Kwanza zili-lockdown kabisa huduma zisizo na lazima kama Bars, clubs na mihadhara ya kidini. Ukikosa hizi hautakufa.

Lakini dini walianza na mikusanyiko ya watu 50. Sisi tulikuwa tunaswali kwa sessions...zilikuwa zinaenda hadi tatu.

Baada ya hapo bado wakaona haisaidii.

Walichofanya ni lockdown ya huduma zote na kuacha tu zile za lazima.

-Hauruhusiwi kutoka nje hadi uwe na kibali.
-unapotoka nje mtaani kwako kuna road block. Utawaonyesha polisi kibali watakipiga mhuri...na kibali kitaeleza uendako.

-ukirudi utawaonyesha huduma uliyoifuata na watakugongea mhuri mwingine.

-Makampuni yaliyoathirika yamesaidiwa kwa asilimia 50%....hivyo hayana sababu ya kutokuendelea kuwalipa wafanyakazi.

Hii japo sio kinga ya asilimia 100 lakini inasaidia.
 
Kuna mkopo tumeomba Marekani
Halafu kuna msaada tumepewa na mmarekani
Jr[emoji769]
 
Waliowekwa kwenye karantini wanatoroka, itakuwa sisi ambao hatuna tuhuma za kubeba hivyo virus !!

Ukweli ni kwamba hali itakuwa mbaya kuwahi kutokea tangu Tanzania itambulike kama nchi.

Sisi acha tuendelee na maisha yetu haya ya kubangaiza, kama corona itatuua kwa mamia basi hata watawala hawatatumia nguvu kutufungia ndani.
 
Basi wakifanya hivyo itakuwa ni kufata mkumbo usio na maana.

Hebu tuangazie pande za U.S.A, walitangaza total lockdown idadi ikiwa bado iko chini sasa hivi tunapojadili hili suala wamefika wagonjwa 277000 + na ndani ya masaa 24 wamekufa watu 1100 ambayo ni idadi kubwa kuwahi tokea toka janga lianze.

Soon nitaweka uzi kwa nini idadi imekuwa kubwa America na kwa nini watu wanakufa sana.

God save us
 
Kwetu sidhani mkuu,tumeona majirani serikali imemsaidia corona kuua raia wake,tuendelee kujikinga kwa kadiri inavyowezekana na kujiepusha kukaa kwenye misongamano,pia kama hauna issue ni bora kutulia home kama mimi ninavyofanya leo.

macson
Wewe umeanza leo, mimi nina wiki nzima niko ndani

God save us
 
Lockdown haiwezekani Dar es Salaam.
1. Kuna nyumba ya vyumba 6 kila chumba kina familia ya watu wanne, hawa utawafanyaje.
2. Kila mkubwa ana mchepuko wake, sasa wakitangaza lockdown huko michepukoni wataendaje.
3. Wanawake wakitanzania wana gubu sana, ni mkubwa gani atakaa na mke mwenye gubu 24/7 kwa siku 30?
4. Dada poa wanapata rizki zao usiku hususan pale Sinza, Kimboka,, Sewa, Great park Tabata. Sasa ukiloki wateja wao huoni watabaka mbuzi na kuku?
5. Trafik polis watakufa njaa maana magari yatakua hayatembei. Hata polisi wa kawaida watakosa mtu wa kumbambikia kesi.
Pointi ziko nyingi ila muda hautoshi
 
Mmeshaandaa Videmu Vyenu vya Kujifungia Navyo ndani basi Mnaombea Lockdown kwa nguvu zote kwa kujifanya mnatabili kwa kutisha Watu..

Wiki moja Lockdown kwa Tanzania ni mateso makubwa kwa 95% ya wananchi

Huu ugonjwa kila anayehusiana na aliyeathirika atakuwa ameathirika. Mnyororo unaendelea. Huu mnyororo utavunjwa vipi bila total lockdown?

Hebu toeni mawazo ya namna ya kuuvunja huu mnyororo.

Ni wakati wa kuisadia serikali kuchukua maamuzi haya magumu.

Bila total lockdown tutakwisha. Hii ni kwa sababu watu wengi wanapokuwa wameambukizwa udhibiti utakuwa tumepoteza.

Bahati mbaya sana serikali nayo imechukua hii ficha ficha ya taarifa sahihi ambako hausaidii.
 
Kuperekeshwa... [emoji30][emoji30][emoji30][emoji30]
Serikali ya awamu ya 5 iko makini sana haiwezi kuperekeshwa na wanasaccos akina Mshana Jr eti lockdown. Kama wanapenda sana hiyo lockdown si wajifungie wao majumbani mwao! Mshana Jr

Jr[emoji769]
 
Marekani waliweka hii lockdown lakini maambukizi yaliendelea kwa kasi ya ajabu

Japan, Sweden hawajaweka lockdown watu wanaendelea na mishe kama kawa maambukizi ni kidogo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna nchi huko wamepinga TOTAL LOCK DOWN.
86% ya waTZ ni wabangaizaji,ila kuna hela zimekuja toka kwa mabeberu naamini Lais wa wanyonge naamini atatupatia viroba vya unga , mchele na sukari ataongea na Rostam atukopeshe mtungi mmoja mmoja wa gesi kila mwananchi .

Piga kelele kwa mheshimiwa Lais wetu.
 

Hapo at least itasaidia...

Kwenye hili janga kuna mambo kama:
  • Kwanza Afya na uhai wa watu.
  • Kipato na maisha ya watu...
  • Unaweza ukafanya total lock down kuokoa Afya na uhai wa watu.
  • Challenge ikaibuka kwenye kipato na maisha ya watu...


Cc: mahondaw
 
Mimi nafikri wafungie mikoa ambayo tayari imesharipoti wagonjwa! Hakuna kutoka wala kuingia kwenye mkoa huko! Mgeni akionekana atolewe taarifa haraka au awekwe quarantine haraka sana! Wananchi tuwe walinzi!
 
Mku Mkuu kuna watu tumepata taarifa wanao tayari ila ndugu wanaficha kuogopa serikali wanachofanya wanasafiri kwenda vijijini kwao kujificha kama mikoani. Shule zikifunguliwa karibuni balaa lake litakuwa sio la kawaida serikali iwe makini sana wanafunzi wengi walioko likizo wataanbukizana vibaya mno shule zikifunguliwa .
 
Do you think wenye hayo maduka ambayo ww unataka yafungwe watakuelewa?
Swala sio kuelewana.. ndio reality maduka yenye vitu muhimu kama madawa na vyakula ndio yanabaki wazi.. hii ndio iko hivyo hata nchi walizofanya quarantine... sio lazima wenye maduka waelewe
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…