Kuna uwezekano mkubwa wa Yericko Nyerere kutimkia CCM muda wowote

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu

Baada ya kutumika kumchafua Lisu hadharani kwa lengo la kutaka kumdidimiza kisiasa, au kumkatisha tamaa ya kugombea uenyekiti wa Chadema taifa, sasa ni wazi kuwa mbinu zake hizo za kumchafua, kumdidimiza na kumkatisha tamaa zimeshindwa. Hivyo inabidi yeye mwenyewe na chawa wenzake wajipange kwa ajili ya plan B.

Namaanisha kwamba ikitokea mwenyekiti wa sasa mh. Mbowe akaweka mpira kwapani siku hiyo ya J'mosi na kuruhusu Lisu kupata nafasi nzuri ya kugombea uenyekiti na kushinda nafado hiyo hapo mwakani, basi Yericko Nyerere hatokuwa na chaguo lingine zaidi ya kukihama chama yeye mwenyewe kwa aibu, na fedheha ili kukwepa lawama na unafiki wa yeye kuendelea kuongozwa na mwenyekiti alietumia muda mwingi kumchafua mitandaoni.

Kwa kauli iliyotoka jana kutoka kwa mwenyekiti wa chama, ni dhahiri kuwa mwenyekiti huyo ameshasoma upepo wa kile kinachoendelea katika chama chake, hivyo ili kunusu mpasuko na mgawanyiko chamani itambidi tu siku hiyo atangaze kutogombea tena uenyekiti. Sasa kauli hiyo ikishatoka kina Yericko Nyerere na Bon Yai wataweka wapi sura zao?

Ndiomaana wahenga walituasa kwamba "Usimtukane mamba, kabla ya kuvuka mto". Sasa Yericko katanguliza kashfa, dhihaka na kejeli kabla ya kujua kwamba mwenyekiti wake wa chama ajae atakuwa ni nani.

Hizi ndio siasa zetu za Tanzania.
 
Tunawatakia safari njema
 
Leo umeandika Kweli. Mbowe HATOGOMBEA uenyekiti, amelenga Urais,

Lakini Yeriko Nyerere Kutoa maoni Si usaliti kwamba asulubishwe, maoni yake yaheshimiwe.
 
Jamaa kuna uwezekano akatimka muda mchache baada ya mwamba kutangaza kutogombea. Hivyo Lisu akiingia ofisini atamkuta jamaa tayar ashakuwa upande wa pili wa chama 🀣🀣🀣
 
Leo umeandika Kweli. Mbowe HATOGOMBEA uenyekiti, amelenga Urais,

Lakini Yeriko Nyerere Kutoa maoni Si usaliti kwamba asulubishwe, maoni yake yaheshimiwe.
Ukisoma vizuri yale aliyokuwa anaandika Yericko Nyerere kumhusu Lisu, utagundua kwamba yale hayakuwa maoni, bali ni udhalilishaji kwa makamu wake wa chama.

Sasa game linaenda kugeuka, yeye (Yericko) ndo anaenda kudhalilika.
 
Aende tu chama tawala, wanatambua mtu wakiamua

Maana anafanya kazi sana na matunda chapati alipo

Watamkaribisha kwa furaha nae ajaze tumbo a relaksiiiiii kwa furaha πŸ˜‚
 
Kwa nini isiwe kinyume chake? Agombee ili anusuru mpasuko wa chama. Angalia pande zote mbili, ndipo utagundua mantiki ya ile kauli ya mwenyekiti.
Akigombea na kushinda, kutaibuka ile dhana ya kwamba hela za mama Abdul zimetumika kuharibu uchaguzi ili jamaa apite.
 
ni uhuru na haki ya kikatiba kwa mwananchi yeyote huru, kuamua kujiunga na chama chochote cha siasa kadiri apendavyo na kwa wakati muafaka wowote, bila mtu mwingine kupata mihemko wala makasiriko dhidi ya uamuzi huo huru πŸ’
 
CCM ilishakufa wamebaki wezi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…