Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu
Baada ya kutumika kumchafua Lisu hadharani kwa lengo la kutaka kumdidimiza kisiasa, au kumkatisha tamaa ya kugombea uenyekiti wa Chadema taifa, sasa ni wazi kuwa mbinu zake hizo za kumchafua, kumdidimiza na kumkatisha tamaa zimeshindwa. Hivyo inabidi yeye mwenyewe na chawa wenzake wajipange kwa ajili ya plan B.
Namaanisha kwamba ikitokea mwenyekiti wa sasa mh. Mbowe akaweka mpira kwapani siku hiyo ya J'mosi na kuruhusu Lisu kupata nafasi nzuri ya kugombea uenyekiti na kushinda nafado hiyo hapo mwakani, basi Yericko Nyerere hatokuwa na chaguo lingine zaidi ya kukihama chama yeye mwenyewe kwa aibu, na fedheha ili kukwepa lawama na unafiki wa yeye kuendelea kuongozwa na mwenyekiti alietumia muda mwingi kumchafua mitandaoni.
Kwa kauli iliyotoka jana kutoka kwa mwenyekiti wa chama, ni dhahiri kuwa mwenyekiti huyo ameshasoma upepo wa kile kinachoendelea katika chama chake, hivyo ili kunusu mpasuko na mgawanyiko chamani itambidi tu siku hiyo atangaze kutogombea tena uenyekiti. Sasa kauli hiyo ikishatoka kina Yericko Nyerere na Bon Yai wataweka wapi sura zao?
Ndiomaana wahenga walituasa kwamba "Usimtukane mamba, kabla ya kuvuka mto". Sasa Yericko katanguliza kashfa, dhihaka na kejeli kabla ya kujua kwamba mwenyekiti wake wa chama ajae atakuwa ni nani.
Hizi ndio siasa zetu za Tanzania.