Kuna uwezekano mwanamke wa dini la Anglican kuoana na mwanaume wa dini la kiislamu?

Bwege2030

Member
Joined
May 10, 2025
Posts
97
Reaction score
197
Habari Ndugu zangu, Mimi Kuna jambo napenda kuwashirikisha labda huenda naweza pata suluhisho..kama kuna mashehe humu au wachungaji mnisaidie..

~Mimi binafsi Kuna Binti tumependana, tumependana mpaka kwenye hatua ya kuwa tusipoonana Binti anaanza kulia...ila sasa Binti ni wa dini la Anglican na Mimi ni dini la Kiislamu..
Ninaitwa Abdullah kutoka Arusha nina miaka 25..na sote Mimi na yeye tupo ARUSHA...
~ Sasa pamoja na hayo wazazi wake wakaja juu haiwezekani mara wakaweka vikwazo vingi wakanambia mpaka niwe tayari kubadirisha dini...
Wakasema tukioana kikawaida bila ndoa kanisani wao watatengwa na wasimamishwe utumishi.

~ Sasa Binti ashanipenda anapenda tuoane...
Unaweza kuwa na ushauri wowote? Chakufanya ili tuoane kwa njia nzurii na rahisi?
Naombeni ushauri wataalamu
 
Tatizo ni hao wazazi wake
Ila mimi wazazi wangu, mzee ni Anglican na maza ni muislamu na wameoana fresh tu bila shida
Tho sikuwepo in their marriage ila at least unaweza kujua inawezekana kuoana watu wa dini tofauti wakaishi muda mrefu huku kila mtu akibaki na dini yake
So ni suala la makubaliano tu. Dini za waarabu na wazungu zisikuzuie kumuoa umpendae
 
Ukweli kwa kizazi hiki ni ngumu sana..
Kwa sasa inaweza kuwa rahisi kutokana na mapenzi,
Lakini ndoa ikianza kukomaa yale mapenzi hupungua na mnaanza kuishi uhalisia,

Hapo ndo changamoto zitakapoanzia, na tofauti zenu za dini ndo mtaanza kuzionea hapo, sasa hivi hamuwezi kuona.
 
Mnaweza kuoana lakini ndoa isidumu.. Asilimia 90 ya ndoa za namna hiyo huwa hazidumu.. Hizo ni falme mbili tofauti, zikisigana kutafuta umiliki mtaishia kuachana! Labda ufalme mmoja ukubali kushindwa na kutii mamlaka ya mwingine
 
Ndiyo mnaweza.

Njia ya kwanza ni mmoja wenu kubadili dini ili ndoa ifungwe kidini.

Njia ya pili ni kuoana kiserikali.

Njia ya tatu ni kuoana kimila.

Hizi ndoa tatu zote zinatambulika kisheria ukiamua kufunga yoyote kati ya hizi.

Umeandika juu juu sana. Ningejua uhusiano una muda gani, financial muscle ya nyinyi wawili ningeweza andika kitu zaidi ya hii ndiyo inawezekana.

Binti kulia msipoonana usidhani ni mapenzi pekee inawezekana binti ana attachment issues, yuko njiani kumaliza stages za wivu au labda ni kweli mapenzi anayaonyesha hivyo.
 
Kidini hakuna ndoa kati ya watu wawili wenye dini tofauti iwe upande wa waislam au wakristo ni lazima mmoja amfuate mwingine kwenye dini yake.
Kama unataka kufunga ndoa labda mfunge ya kiserikali tu ndo inatambua ndoa ya watu wenye dini mbili tofauti.

Lakini pia kuoana watu wa dini mbili tofauti kuna hasara kubwa sana kuliko faida hasa ukizingatia ndoa za kizazi cha sasa
 
Hapa umepuyunga

Kidini waislamu tunaruhusiwa kuoa mwanamke wa kikristo bila yeye kubadilisha dini yake lakni mwanaume unatakiwa usimamie uzao wako uwe wa dini ya kiislamu namaanisha watoto wenu mtakao zaa wasifate upande wa mwanamke kwenye dini wawe waislam
 
Ubinafsi
 
Kidini hakuna ndoa kati ya watu wawili wenye dini tofauti iwe upande wa waislam au wakristo ni lazima mmoja amfuate mwingine kwenye dini yake.
Kama unataka kufunga ndoa labda mfunge ya kiserikali tu ndo inatambua ndoa ya watu wenye dini mbili tofauti.

Lakini pia kuoana watu wa dini mbili tofauti kuna hasara kubwa sana kuliko faida hasa ukizingatia ndoa za kizazi cha sasa
Kuona watu wa dini mbili tofauti hasara ni zipi?
 
Hiyo ni ndoa isiyowezekana katika ukamilifu wa kiimani. Ni aheri wewe ungekuwa msichana halafu hiyo binti angekuwa mwanaume. Hapo ndoa ingeweza kufungwa kwa sharti moja kuu kuwa watoto watakaozaliwa watakuwa wakristo, ndoa za namna hiyo kibali hutolewa na askofu. Maana kiapo kimoja kikuu wakati wa kufunga ndoa ni kuwa mtawalea watoto mtakaowapata katika msingi wa dini, yaani dini ya kikristo.

Kwa upande mwingine, kwenye uislam, watoto ni wa baba, na yeye baba ana wajibu wa kuhakikisha watoto watakaozaliwa wanalelewa kwa misingi ya dini ya kiislam.

Hao wazazi kukataa binti yao asiolewe na mtu wa imani tofauti ya kidini, kiimani wapo sahihi maana waliapa kuwa watawalea na kuwaongoza watoto wao katika imani ya kikristo.

Kuweza kuoana, labda huyo binti aasi imani yake na aolewa bila ridhaa ya wazazi wake. Au wewe uasi imani yako, ufuate masharti ya imani ya unayetaka kumwoa.

Kiuhalisia, kwa ninyi mkiwa kwenye imani tofauti, na kila mmoja akaishi kwa imani yake, halafu ndoa ikawa na amani, kuna nafasi ndogo sana. Labda muishi nusu waumini, nusu wapagani. Lakini kama kila mmoja akiishi kwa kuzingatia kikamilifu imani yake, mtagongana tu. Hapa mwanzoni mnaweza kuishi vizuri kwa sababu ya nguvu za mapenzi, lakini baadaye mtakapotakiwa kuishi kwa kutegemea zaidi hekima, mtatofautiana. Na hilo nimelishuhudia kwa baadhi ya wanafamilia.
 
Vipi kama hawataki watoto?
 
Ziacheni wote dini zenu kisha muoane, hakuna mtu aliyezaliwa ni muislamu au mu anglican yote mmerithi so mkiziacha mtaona faida zake na mtaoana. Ukishindwa sana nipasie mimi huyo binti maana hata mimi ni muanglican
 
Tatizo ni hao wazazi wake
Ila mimi wazazi wangu, mzee ni Anglican na maza ni muislamu na wameoana fresh tu bila shida
Tho sikuwepo in their marriage ila at least unaweza kujua inawezekana kuoana watu wa dini tofauti wakaishi muda mrefu huku kila mtu akibaki na dini yake
So ni suala la makubaliano tu. Dini za waarabu na wazungu zisikuzuie kumuoa umpendae
Ndiyo mnaweza.

Njia ya kwanza ni mmoja wenu kubadili dini ili ndoa ifungwe kidini.

Njia ya pili ni kuoana kiserikali.

Njia ya tatu ni kuoana kimila.

Hizi ndoa tatu zote zinatambulika kisheria ukiamua kufunga yoyote kati ya hizi.

Umeandika juu juu sana. Ningejua uhusiano una muda gani, financial muscle ya nyinyi wawili ningeweza andika kitu zaidi ya hii ndiyo inawezekana.

Binti kulia msipoonana usidhani ni mapenzi pekee inawezekana binti ana attachment issues, yuko njiani kumaliza stages za wivu au labda ni kweli mapenzi anayaonyesha hivyo.
Ningehitaji uendelee nijifunze zaid
 
Back
Top Bottom