Asante sana kwa ushauri wakoMnaweza kuoana lakini ndoa isidumu.. Asilimia 90 ya ndoa za namna hiyo huwa hazidumu.. Hizo ni falme mbili tofauti, zikisigana kutafuta umiliki mtaishia kuachana! Labda ufalme mmoja ukubali kushindwa na kutii mamlaka ya mwingine
Hapa umepuyungaKidini hakuna ndoa kati ya watu wawili wenye dini tofauti iwe upande wa waislam au wakristo ni lazima mmoja amfuate mwingine kwenye dini yake.
Kama unataka kufunga ndoa labda mfunge ya kiserikali tu ndo inatambua ndoa ya watu wenye dini mbili tofauti.
Lakini pia kuoana watu wa dini mbili tofauti kuna hasara kubwa sana kuliko faida hasa ukizingatia ndoa za kizazi cha sasa
UbinafsiHapa umepuyunga
Kidini waislamu tunaruhusiwa kuoa mwanamke wa kikristo bila yeye kubadilisha dini yake lakni mwanaume unatakiwa usimamie uzao wako uwe wa dini ya kiislamu namaanisha watoto wenu mtakao zaa wasifate upande wa mwanamke kwenye dini wawe waislam
Kuona watu wa dini mbili tofauti hasara ni zipi?Kidini hakuna ndoa kati ya watu wawili wenye dini tofauti iwe upande wa waislam au wakristo ni lazima mmoja amfuate mwingine kwenye dini yake.
Kama unataka kufunga ndoa labda mfunge ya kiserikali tu ndo inatambua ndoa ya watu wenye dini mbili tofauti.
Lakini pia kuoana watu wa dini mbili tofauti kuna hasara kubwa sana kuliko faida hasa ukizingatia ndoa za kizazi cha sasa
FafanuaUbinafsi
Ni ubinafsi kusema watoto lazima wawe Waislamu badala ya kuwaachia wachague wenyewe.Fafanua
Vipi kama hawataki watoto?Hiyo ni ndoa isiyowezekana katika ukamilifu wa kiimani. Ni aheri wewe ungekuwa msichana halafu hiyo binti angekuwa mwanaume. Hapo ndoa ingeweza kufungwa kwa sharti moja kuu kuwa watoto watakaozaliwa watakuwa wakristo, ndoa za namna hiyo kibali hutolewa na askofu. Maana kiapo kimoja kikuu wakati wa kufunga ndoa ni kuwa mtawalea watoto mtakaowapata katika msingi wa dini, yaani dini ya kikristo.
Kwa upande mwingine, kwenye uislam, watoto ni wa baba, na yeye baba ana wajibu wa kuhakikisha watoto watakaozaliwa wanalelewa kwa misingi ya dini ya kiislam.
Hao wazazi kukataa binti yao asiolewe na mtu wa imani tofauti ya kidini, kiimani wapo sahihi maana waliapa kuwa watawalea na kuwaongoza watoto wao katika imani ya kikristo.
Kuweza kuoana, labda huyo binti aasi imani yake na aolewa bila ridhaa ya wazazi wake. Au wewe uasi imani yako, ufuate masharti ya imani ya unayetaka kumwoa.
Kiuhalisia, kwa ninyi mkiwa kwenye imani tofauti, na kila mmoja akaishi kwa imani yake, halafu ndoa ikawa na amani, kuna nafasi ndogo sana. Labda muishi nusu waumini, nusu wapagani. Lakini kama kila mmoja akiishi kwa kuzingatia kikamilifu imani yake, mtagongana tu. Hapa mwanzoni mnaweza kuishi vizuri kwa sababu ya nguvu za mapenzi, lakini baadaye mtakapotakiwa kuishi kwa kutegemea zaidi hekima, mtatofautiana. Na hilo nimelishuhudia kwa baadhi ya wanafamilia.
Tatizo ni hao wazazi wake
Ila mimi wazazi wangu, mzee ni Anglican na maza ni muislamu na wameoana fresh tu bila shida
Tho sikuwepo in their marriage ila at least unaweza kujua inawezekana kuoana watu wa dini tofauti wakaishi muda mrefu huku kila mtu akibaki na dini yake
So ni suala la makubaliano tu. Dini za waarabu na wazungu zisikuzuie kumuoa umpendae
Ningehitaji uendelee nijifunze zaidNdiyo mnaweza.
Njia ya kwanza ni mmoja wenu kubadili dini ili ndoa ifungwe kidini.
Njia ya pili ni kuoana kiserikali.
Njia ya tatu ni kuoana kimila.
Hizi ndoa tatu zote zinatambulika kisheria ukiamua kufunga yoyote kati ya hizi.
Umeandika juu juu sana. Ningejua uhusiano una muda gani, financial muscle ya nyinyi wawili ningeweza andika kitu zaidi ya hii ndiyo inawezekana.
Binti kulia msipoonana usidhani ni mapenzi pekee inawezekana binti ana attachment issues, yuko njiani kumaliza stages za wivu au labda ni kweli mapenzi anayaonyesha hivyo.
Kwani mungu wa Ukristo na Uislamu sio mmoja?!Mnaweza kuoana lakini ndoa isidumu.. Asilimia 90 ya ndoa za namna hiyo huwa hazidumu.. Hizo ni falme mbili tofauti, zikisigana kutafuta umiliki mtaishia kuachana! Labda ufalme mmoja ukubali kushindwa na kutii mamlaka ya mwingine