Kuna uwezekano mwanamke wa dini la Anglican kuoana na mwanaume wa dini la kiislamu?

Wahusika wameshapendana tayari. Dini haina maana tena
Kama dini haina maana kwanini kila mtu anangangania abaki kwenye dini yake badala mmoja kufuata mwenzake ili iwe rahisi kwao kufunga ndoa?
Kama dini haina maana yeyote mbele ya upendo huyo mleta mada hata asinge kuja hapa kuomba ushauri wa ni namna gani afunge ndoa na mtu wa dini tofauti bali angetekeleza matakwa ya wazazi wa binti.
Lakini kwa sababu dini yake ni muhimu ndo maana kaja hapa kuomba ushauli ina maana hiyo yote yakishindikana yuko tiyari kumuacha binti lakini sio kubadili dini.
 
Hili ndio jibu sahihi kabisa.
 
Ameleta mada kwa sababu shida ni hao wazazi ndio wanekumbatia dini
Ila wao wamependana na wako tayari kuoana. Kwa hiyo dini sio shida kwa upande wa mleta mada. Shida ni kutaka ndoa yao imfurahishe kila mtu kwenye familia
 
Fanyeni uamuzi nyinyi wenyewe bioa kujali wazazi wenu.Fanyeni kati ya haya:
1.Fungeni ndoa ya serikali ili kila mmoja abaki na dini yake
2.Mmoja wenu abadili dininamfaye mwenzie ili mfunge ndoa ama ya kanisani au ya kiislamu
 
Hebu soma tena kwa makini nilichoandika
Mnaweza kuoana lakini ndoa isidumu.. Asilimia 90 ya ndoa za namna hiyo huwa hazidumu.. Hizo ni falme mbili tofauti, zikisigana kutafuta umiliki mtaishia kuachana! Labda ufalme mmoja ukubali kushindwa na kutii mamlaka ya mwingine
 
Sawa nimekuelewa
 
Halafu hizi dini ni kama zilileta ligi flani hivi. Iweje kuwe na mungu wawili?
 
Ameleta mada kwa sababu shida ni hao wazazi ndio wanekumbatia dini
Ila wao wamependana na wako tayari kuoana. Kwa hiyo dini sio shida kwa upande wa mleta mada. Shida ni kutaka ndoa yao imfurahishe kila mtu kwenye familia
Wazazi ni kikwazo kwani wao wamemkataza kumoa au wamempa masharti ya kutimiza ili aweze kumuoa?

Dini isingekuwa na uzito wowote kwa mleta mada asingeona uzito wowote wa kufuata matakwa ya wazazi wa binti kwa kuihama dini yake na kuhamia dini ya binti ili amuoe kwa sababu dini kwake haina maana.
Upendo ungeonekana unanguvu kuliko dini iwapo mmoja wao angekubali kuasi dini yake na kumfuata mwenzake.
Ina maana wazazi wa binti wasipo legeza kamba kuhusu shariti lao huyo mleta mada yuko tiyari ayaasi mapenzi kwa huyo binti ili kulinda dini yake.

Alafu haya ninayo yasema nimeyashuhudia miongoni mwa ndugu zangu na sio kwamba naongea kinadharia au kwa kusikia tu.
 

Kwa Hiyo Binti Kulia Asipokutia Machoni...Unaamini Anakupenda Sana Sana....Na Ukaona Ni Vyema Kuhitaji Kuwa Naye Katika Taasisi Ya Ndoa....??
###KilaLaKheri###
​
 
Uko sahihi mkuu, dini ni kikwazo
Ila upande wa wazazi. Mi sidhani kama wapendanao wana shida
Ila yeah, ameleta mada anahitaji msaada. Na tatizo liko kwa wazazi, naelewa
 
Kwanini wataka binti tu ndiye abadili dini awe mwislam na sio huyo muislam abadili dini na kuwa mkristo?
Au kwasababu ni binti ndiye kampenda sana mwanaume kuliko mwanaume alivyo mpenda binti?

Kama mwanaume hana mapenzi ya kutosha kwa binti kiasi cha kutosha kubadili dini kuwa mkristo basi aachane naye aende tafuta mwislam mwenzake.
 
Fanyeni uamuzi nyinyi wenyewe bioa kujali wazazi wenu.Fanyeni kati ya haya:
1.Fungeni ndoa ya serikali ili kila mmoja abaki na dini yake
2.Mmoja wenu abadili dininamfaye mwenzie ili mfunge ndoa ama ya kanisani au ya kiislamu
Yaani uoe au kuolewa na mtu wazazi hawajataka?
Hiyo ndoa ikipatwa na changamoto suluhisho mnakwenda kwa nani?
Au ndio mnaalika marafiki waje wawasuluhishe?
Au mnakimbilia kwa mashehe?

Ni wazazi pekee ndio wenye uwezo wa kumuonya kijana au binti anayekengeuka katika ndoa wakasikilizwa.

Kawaida ya wazazi huwa hawachagui muonekano wa umbo la mtu anayefaa kuolewa au kuoa mtoto wao lakini maadili hilo wazazi huwa nalo makini sana na maadili ni pamoja na dini na kabila.

Sio kila kilicho kawaida kwa kabila flani kitu hicho kinakuwa ni maadili mazuri kwa kabila lingine.

Sio kila kilicho sawa kwa dini flani ni maadili mazuri kwa dini nyingine.
Mfano katika ukristo ni maadili mabaya kuoa mke zaidi ya mmoja sasa ni mzazi kichaa tu anaweza kubali binti yake mabichi kwenda olewa na mwislam ambako uwezekano wa kuongezewa wake wengine mpaka watatu ni kugusa tu.
 
Uko sahihi mkuu, dini ni kikwazo
Ila upande wa wazazi. Mi sidhani kama wapendanao wana shida
Ila yeah, ameleta mada anahitaji msaada. Na tatizo liko kwa wazazi, naelewa
Wazazi hawana tatizo lolote ni haki yao kuhakikisha kuwa binti yao anaolewa sehemu ambayo wao wanahisi ni salama hata kama anaye taka kumuoa ni wa imani moja.
Hata wewe binti yako huwezi kumuacha akaolewa na yeyote eti kwa kigezo cha wamependana je ww uko tiyari mtoto wako aolewe na jambazi au kibaka eti kwasababu wamependana tu?
Upendo ni sehemu ya ndoa na sio ndoa yenyewe kitu kinacho itwa ndoa ni muunganiko wa vitu vingi sana na kimoja kikikosekana ndoa nilazima ipate mushikeli.

Tatizo lipo kwa mleta mada inaonesha dini kwake ni muhimu kuliko mapenzi ya binti ndo masna anaona ugumu kufuata matakwa ya wazazi wa binti.
 
Upo sahihi mkuu
 
Sasa jambazi na kibaka inafanana vipi ni Mkristo na Muislamu 😂
 
Sasa jambazi na kibaka inafanana vipi ni Mkristo na Muislamu 😂
Mm nimetoa mfano ili kukuonesha kuwa upendo tu hautoshi kuamua hatima fulani ya mapenzi ya wapendanao.
Mnaweza kuwa mnapendana lakini kukawa na kikwazo kigumu ambacho mapenzi yenu hayana uwezo wa kukivunja na moja wapo ya kitu hicho ni imani.
Nakushangaa sana unapo puuza nguvu ya kitu kinacho itwa dini hasa kwa jamii ya waafrika.
 
Mnaweza kulazimisha na kuona haina shida, ila ipo shida, kusudi la kuoana ni kuja kusaidiana katika kulitimiza kusudi la Mungu. Kuwa imani tofauti tena wanandoa ni mgogoro mmojawapo... Kwenye urafiki/uchumba unaweza kuona haina shida ila kwenye ndoa ni maisha halisi na utaona rangi ambayo hukuwahi kuiona kwenye uchumba.

Suala la ndoa ni la kiroho na kimwili, kama kiroho mnatofautiana kiimani tayari hapo mmetengeneza tatizo kabla ya kukutana nalo.

Kibiblia hili jambo haliruhusiwi na Mungu, unapaswa kuoa/kuolewa na mkristo mwenzako mwenye mapokeo sawa na yako, na imani sawa na yako.

Acha kujidanganya kuwa tunapendane sana, imani ni suala muhimu sana katika ndoa yenu.

Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…