Kuna uwezekano wa kuacha au kupunguza tabia zetu mbaya pamoja na mapungufu ili tuishi vizuri na watu?

Kuna uwezekano wa kuacha au kupunguza tabia zetu mbaya pamoja na mapungufu ili tuishi vizuri na watu?

TRABSOH

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
351
Reaction score
559
Habari wakuu,

Kama wanadamu tuna kasoro na mapungufu mengi ambayo katika hali ya kawaida ni kama tumeumbwa navyo yani huyo ndo wewe huwezi kumbadilisha.

Katika hali hii wengi wanapata shida kuishi na watu ata wenza wao wanajikuta wanakuwa kero kwa watu wanaowazunguka.

Wakati mwingine inatesa kwasabbu unatamani kuacha lakini inakuwa ngumu au unajikuta unateseka kuacha, kwa mfano mtu unaongea sana na unajikuta maeneo mengi unakuwa unakataliwa au kukimbiwa kwa sababu ya mdomo na umelijua hilo unatamani kuacha lakini unashindwa.

Twende kwenye mfano halisi; mimi katika jamii nilizoishi katika nyakati tofauti nimejikuta naambiwa nina dharau hasa na wanawake nmejitaidi kujaribu sasa kuongeza mazoea ya kuongea na kusalimia watu hili huu mtazamo kwa watu upungue na nisipewe hiyo sifa mbaya. Inaniwia ugumu lakini nmeamua nitabadilsha hii tabia ambayo ni kama ndo mimi sasa siwezi kujikataa!

Je, inawezakana kuacha tabia mbaya ambazo huko nazo na unajijua uko nazo na ni kero kwa mkeo, watoto ,ndugu, jamii na watu wanaokuzunguka?
 
Nyingine zinawezekana, nyingine haiwezekani ila inategemea nyakati na majira

Waswahili wanaseme TABIA ni kama ngozi ya mwili hauwezi kuibadili
 
Nyingine zinawezekana, nyingine haiwezekani ila inategemea nyakati na majira

Waswahili wanaseme TABIA ni kama ngozi ya mwili hauwezi kuibadili
Sasa usipobadili sindo unajiweka kwenye nafasi ya kuwa mtu mwenye sifa mbaya katika jamiii, mfano wale ambao ukifika tu ofisi flani unaambiwa flani kaa nae mbali mmbea alafu mnafiki tena unakuta unaambiwa na watu wengi wa mahali hapo
 
Nadhani waswahili walikuwa sawa 50%
 
Sasa usipobadili sindo unajiweka kwenye nafasi ya kuwa mtu mwenye sifa mbaya katika jamiii, mfano wale ambao ukifika tu ofisi flani unaambiwa flani kaa nae mbali mmbea alafu mnafiki tena unakuta unaambiwa na watu wengi wa mahali hapo
Kitu kimoja utambue binadamu haitakaa hata siku moja tufanane.. never ever
 
Back
Top Bottom