Kuna Video iliyokuwa ikionesha Polisi/traffic wa Inyala, Mbeya wakimshusha kwa nguvu dereva wa lori. Polisi wadai amekufa kwa homa ya mapafu

Si kazi yetu kukuamsha usingizini , taarifa hii ipo humu jf tena kwa upana sana , hatuwezi kuirudia , hata hivyo hata utaratibu wa jf hauruhusu kurudia kuleta habari , tumeleta tamko la polisi tu , ni kazi yako kutafuta habari zilizotangulia .

Tunatambua gharama ya bando kwa sasa imefanya wengi muwe nje ya mtandao , poleni sana , #Mitano tena .
 
Homa yamapafu ndyo ugonjwa gani si waseme tu covid na aliwwzaje kuebdesha gar akiwa na hali mbaya kiasi kile
 
Nikikumbuka RPC njombe alivomdanganya waziri kuhusu mauaji ya watoto njombe.tangu siku ile sina imani na polisi aisee.iviagonge magari.halafu gari lake lisikwaruzwe hata kidogo.kwamba alikimbia ni gari la kukimbia hilo?
 
Hili tukio halina tofauti na lile la mauji ya Mwangosi enzi za Kikwete na msishangae kuona hakuna askari ataechukuliwa hatua.

Nashangaa sana watu wanapomkubuka Kikwete na si ajabu watakuja tena kumkumbuka Magu kwani wanadamu tumeumbwa kusahau.
Mkapa hakukumbukwa Kwa mema ujue
 
Ukifungwa akili omba Mungu usifungwe na utu.
 
Kuna kitu kwenye sheria kinaitwa causation/chanzo....hata mtu kama alikuwa vakiumwa marelia kali ukampiga/ukamuangusha kwa makusudi akafa......!!
huzo tuhuma unawajibika nazo
 
Kuna kitu kwenye sheria kinaitwa causation/chanzo....hata mtu kama alikuwa vakiumwa marelia kali ukampiga/ukamuangusha kwa makusudi akafa......!!
huzo tuhuma unawajibika nazo
Umesoma sheria gani?Mbona mwandiko mbaya na hausomeki!
 
Hilo lilikuwa wazi polisi wasingeweza kukubali kuonekana wao ndo wenye makosa so wametafuta kisingizio kinachoweza kukubalika
 
Kwa hiyo walikuwa wanamtibu kwa kumrusha toka juu ya gari?
Majibu rahisi kwenye tuhuma nzito kama hii
Dhulma hii ya kiumbe huyo haitawaacha salama
 
Nimekupata.
 
Muda Mwingine nguvu wanazo tumia Police Mhhh ni bora Tupewe chanjo ya CORONA tuu
 
ila binadamu tujitahidi kuwasemea mabaya watu, maelezo yanasema dereva aliambiwa na daktari karibia anafika Mbeya( yaani hospitali ya Chimala) 1. anatakiwa kulazwa , 2. baadae akawa anaendesha gari na kuyagonga magari kadhaa kutokana na udhaifu3. watu wakapiga simu kwa askari kulalamika uendeshaji wake,. naomba tuwe na subira, kuna madhara kuchochea mambo kama haya; mfano mke wako au mama yako mwalimu, akiwa shuleni akamchapa mtoto (adhabu ya kawaida ) bila kujua akafariki, watu bila kujua undani wakaja hapa kusema , '' aaah walimu wamezidi saaana , huyo ni kkufunga tu ! tutakuwa tunaharibu mfumo wa haki
 
Mbona kauli zinafanana na za Aquilina,hizi kauli wanazihifadhi kwenye kofia?
Kama madereva wenzake walimpeleka! Inamaana wao hawahusiki ila madereva wenzake ndio wakuhojiwa, sungura mjanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…