Kuna Video iliyokuwa ikionesha Polisi/traffic wa Inyala, Mbeya wakimshusha kwa nguvu dereva wa lori. Polisi wadai amekufa kwa homa ya mapafu

Kuna Video iliyokuwa ikionesha Polisi/traffic wa Inyala, Mbeya wakimshusha kwa nguvu dereva wa lori. Polisi wadai amekufa kwa homa ya mapafu

Mbona kauli zinafanana na za Aquilina,hizi kauli wanazihifadhi kwenye kofia?
Kama madereva wenzake walimpeleka! Inamaana wao hawahusiki ila madereva wenzake ndio wakuhojiwa, sungura mjanja.
😆😆😆
 
Sijawahi kuziamini taarifa za polisi hata siku moja.
 
Sinema la M0 lishaanza tena - episode 2

Tayari washapandikiza corona kwa mwili wa marehemu dereva - wabongo ni balaa!! Mchina akasome!!
 
Uandishi gani huu wa habari!
====
Toa details za wahusika, mazingira yalikuwaje, ndipo utoe taarifa ya tukio zima. Siyo wote wanaelewa unayoelewa juu ya mkasa huu. Hata hivyo asante sana mleta mada kwa kutujuza uwepo wa mkasa huu.
====
Moderators, mkiwa mnapata wasaa muwe 'mnatupiga shule', namna ya kuwasiliza taarifa hapa JF.

Uandishi gani huu?
Toa kibanzi jichoni kwako kabla ya kutoa boriti la jicho la mwenzako.
"Kuwasiliza" ni nini!?
 
Na kwamba walipomkamata waligundua kwamba anaumwa ambapo madereva wenzake walipompeleka kwenye hospitali ya Chimala aligundulika kuwa na homa ya mapafu, hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Jerome Ngowi

View attachment 1689757

Natoa pole kwa wafiwa na Namuomba Mwenyezi Mungu aipokee roho ya Marehemu Dereva , Amina

Watakuwa wamesahau kuandika homa kali ya mapafu. Yaani wametaka tujiongeze wenyewe kuwa alichelewa kupiga nyungu.
 
Na kwamba walipomkamata waligundua kwamba anaumwa ambapo madereva wenzake walipompeleka kwenye hospitali ya Chimala aligundulika kuwa na homa ya mapafu, hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Jerome Ngowi

View attachment 1689757

Natoa pole kwa wafiwa na Namuomba Mwenyezi Mungu aipokee roho ya Marehemu Dereva , Amina

Kuna mijamaa ya chama fulani itachukua jukumu la kujaribu kutushawishi kuwa polisi wako right.

Mijamaa ya chama hicho pia ikidai kwa mara ya kwanza kuwa alikuwa ni mgonjwa wa Corona tu na hivyo ilikuwa halali kufa hivi wala haitakuwa ajabu:

Mijamaa ya fursa za kisiasa.
 
Polisi Mbeya wadai dereva wa lori alikuwa na homa ya mapafu
Mbeya. Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limesema dereva wa lori, Abrahaman Hussein (61) aliyefariki dunia muda mfupi baada ya kumkamata alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa homa ya mapafu
Ugonjwa huu haupo katika orodha ya magonjwa ya binadamu
 
Uandishi gani huu?
Toa kibanzi jichoni kwako kabla ya kutoa boriti la jicho la mwenzako.
"Kuwasiliza" ni nini!?
Kwenye kiswahili kuna maneno mawili, dhima na Maudhi! Ukitofautisha maneno haya utaelewa ujumbe ulio kwenye bandiko langu. Karibu.
 
Polisi watueleze tu sababu iliyopelekea mpaka kumshusha kwenye gari,Tuanzie hapo kwanza
 
Back
Top Bottom