Salaam wakuu,
Kumekuwa na video mitandaoni ikionesha polisi/traffic wa Inyala, Mbeya wakimshusha kwa nguvu dereva wa lori na kumuangusha chini, na baada ya hapo imeripotiwa dereva huyo amefariki. Tunaomba mamlaka husika itolee majibu sintofahamu hii, na ni nini kinachopelekea matumizi ya nguvu kubwa namna hiyo kwa askari wa usalama barabarani?
Hiyo video imeonesha dereva akiwa amevuliwa suruali nusu hadi magotini.
Hii ni post ya dereva wa magari makubwa kuhusiana na hii:
"Habarini za mida wapambanaji wenzangu nimesikia mahala kua kuna dereva kapigwa na askari wa usalama barabarani huko Mbeya na amefariki alipokua sero. Je, imekaaje hii viongozi wetu? Kama ni kweli mbona tunafanywa kama nguruwe tukiwa barabarani? Mimi huea nadhani nikikutana na askari wa usalama barabarani najua nimekutana na nipo salama lakin sasa kwa staili hii tunapelekwa wapi? Makosa watubambikie na hauna pakwenda kulalamika hasa ukishapigwa cheti, kutupiga watupige ndio; na kifo?
Polisi kama kweli mmelifanya hili, hampo sahihi ndugu zetu. Kumbukeni mapolisi wengine mmesomeshwa na baba ambaye ni dereva. Pia je, wakati unasoma usikie baba yako amepigwa na police, ungejisikiaje?
Tubadilikeni maaskari; hicho ni cheo tu. Sisi na ninyi wote ni sawa. Tofauti yetu isikufanye kumuona dereva ni adui yako. Mmefundishwa kutenda haki, tendeni haki ndugu zangu. Haya, Mwenyezi Mungu awabariki. Labda mlichokitaka ndio hicho.
Pumzika kwa amani mpambanaji mwenzetu, mbele yako nyuma yetu"
Tunaomba kujua kama kuna ukweli wowote juu ya video hii.