Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari!
Mimi ni mwajiriwa katika ofisi moja ya umma.
Sasa hapa kazini kuna watumishi wa kudumu, wa mkataba wa muda mfupi na wanafunzi waliokuja kufanya field na wengine wamezamia mazima wakisubiri huruma za boss huenda atawaajiri.
Yes. Wapo walioanza kama wanafunzi mpaka wakaajiriwa kwa mkataba mfupi (renewable). Wengine huu mwaka wa 5, 6, n.k hawana hata mkataba, wanaambulia kaposho kidogo tu ingawa ndio hutegemewa sana kwenye majukumu.
Wameshindwa kupata ajira kwasababu aidha vigezo vyao ni hafifu au uchache wa ajira. Kwa huruma nikawashauri vijana watatu waliobobea kwenye utaalamu tofauti ambao wakijumuisha nguvu wanaweza kufungua ofisi moja na wakawa na maisha mazuri au hata wakawa matajiri baada ya miaka kadhaa.
"Kwakuwa nyie karibu wote mna uzoefu wa kazi na hamjaajirwa kwa miaka zaidi ya minne sasa basi muwaze kujiajiri kwa kuunganisha nguvu, mtapata pesa nyingi huko mbele kuliko hata sisi wenye ajira" Niliwaambia.
Niliwasihii watafute milioni 3 ya kianzio (kukodi) ofisi au fremu na kununua vitendea kazi.
Jibu walilonipa kuwa hawana pesa.
Nikawaambia kila mmoja wenu akamwambie mzazi au mlezi wake ampatie milioni moja hata kwa mkopo. Kama hilo humu basi mumtafute mtu mwenye pesa mumpe wazo lenu awakopeshe au naye akubali kuwa sehemu ya ofisi.
Wakawa wagumu kuelewa. Nikawaambia hata Mimi kama mko tayari naweza kutoa hiyo pesa kwa masharti ya umiliki wa ofisi kwa 25% yaani mgawanyo sawa. Bado wamekuwa wazito.
Vijana wajinga sana hawa, tunafanya kazi tena wao hutumikishwa zaidi kwa malipo ya pesa ya nauli tu na kila siku kazini wanakuja.
Hii nchi ina vijana wajinga sana.