Tetesi: Kuna viongozi wanaolipwa na serikali ya Misri ili tusitumie maji ya ziwa Victoria

Tetesi: Kuna viongozi wanaolipwa na serikali ya Misri ili tusitumie maji ya ziwa Victoria

Maji ya Lake Victoria yanatakiwa yalishe chakula kwa nchi nzima na yavalishe nguo mpya kwa kilimo cha pamba africa nzima
 
Serikali ifanye maamuzi juu ya suala hili, siasi iwekwe pembeni maji yatoke kwa ajili ya kilimo kikubwa cha umwagiliaji kanda ya ziwa. Ni aibu taifa halina maji ya kunywa, mifugo na watu wanachangia maji ndiyo maana bajeti yetu ya afya lazima ipande kila mwaka kwa ajili ya kutibu magonjwa yanayosababishwa na maji machafu vijijini. Jambo hili halihitaji la Rais ako compromise katika awamu yake hii, vinginevyo tujue ziwa ni la misri yaishe kama tunashindwa jambo dogo kama hili na njaa inatusakata tutaweza viwanda kweli !!!
 
Hiyo mikataba ya kijinga jinga inatekelezwaje??? Yaani mie natokea Kigera Etuma pale ziwani kabisa nishindwe kufanya kilimo cha umwagiliaji mkubwa nikiwa na fedha kisa kuna Mwarabu wa Misri anayo haki ya maji ya Ziwa Victoria!!!

Kama wapo viongozi hao, wakijulikana Mh. Rais aidhinishe tuwanyonge hadharani.
 
Nilishangaa kuona Membe anataka tusiyatumie maji ya Ziwa victoria eti kwa sababu Misri itaathirika. Akaenda mbele hata k kuzishawishi nchi za Maziwa makuu kuifikiria Misri zaidi kwa madai eti sisi nchi za ukanda huu wa kusini mwa mto nile tunapata mvua za kutosha! Huyu Membe mtu wa ajabu sana!.

Wao Misri wana bahari ya mediteranian, wanaweza kufanya desalination.

Misri wana Jangwa la Sahara. Ambayo chini yake huenda kuna maji mengi kama ambayo Libya waligundua.

Isitoshe sisi tuna mgogoro wa Ziwa Nyasa, sasa inakuwaje anagive up rights za Watanzania kuyafaidi Maji ya Ziwa hilo la Victoria?

Huyu Membe hatufai,angetuuza!!
 
Lowasa alilikuta tu aliyewakabili wamisri kuwa lilwalo na liwe Tanzania itatumia maji ya Victoria kupeleleka maji maeneo kame ya shinyanga alikuwa Mwandosya alipotamka Hilo misri wakasema Hilo tamko ni kutangaza vita Mwandosya akiwa waziri akakomaa wamisri WAKANYWEA NDIPO LOWASA akiwa waziri akatekeleza Yale aliyokomalia mwandosya.
Sasa unamaanisha nini? nami nimesema nini? chuki yako kwa Lowasa haiwezi futa mazuri yake, Lowasa amekomaa maji yakaenda shinyanga, hutaki basi edit badala ya Lowasa weka jina la mpenzi wako, mccm sijui nani kawaloga mnachuki mbaya sana.
 
Ziwa victoria ni chanzo kinachopeleka maji river nile, Ambapo misri ni final destination kama mpokeaji maji kutoka ziwa victoria.

Hivyo basi sisi watanzania tukiwa na project (irrigation schemes) nyingi kama hzi kiwago cha maji kitakacho kua kinapotea kila siku kitakua kikubwa, Na kupelekea kiwango cha maji kupungua nchini misri.
Tukumbuke kwamba maji hadi yafike misri yanipita sudani na uganda ambapo pia yatatumika katika miradi mbalimbali.

Egypt ni nchi inayotegemea sana kilimo(large scale agriculture) kwa kutumia njia ya umwagiliaji.

Hitimisho.
Egypt ili wafanikishe kilimo cha umwagiliaji wanategemea maji kutoka victoria kupitia mto nile.
Kiwango cha wingi au uchache wa maji mto nile unategemea sana utumiaji wetu maji sisi watanzania.
kijiografia pia misri wapo karibu na bahari ya mediteraniani sasa basi kwann wasitumie hiyo bahari pindi wakiona maji yamepungua ebu wacha maneno yako mkuu maji yanatoka kwetu alafu tupewe mashart tena ya kuyatumia
hata hivyo bahar ya shamu ipo karibu na ndio maana waisraeli walikimbilia huko coz waliona ni karibu hivyo basi hawa watu wasitegemee ziwa victoria
 
Mkuu:
Kwa hiyo sisi hatuna haki ya matumizi ya hayo maji, kwa sababu tutaleta upungufu.

Je tukichukua kutoka kwenye vyanzo au mito inayo ingiza kwenye ziwa victoria bado tutakuwa hatuna haki?

Point Taken for action
 
Mbona ni miaka mingi sana watu wanafaidika na ziwa NYANZA kwa sisi wazaliwa wa huko tunajua hilo.

Hadi kipindi fulani misri waliandaa michuano ya soka kwa timu za taifa zinazopitiwa na Mto Nile lengo likiwa kunakopita huo Mto kusiwe na matumizi makubwa zaidi ya matumizi ya majumbani.
 
Ziwa victoria ni chanzo kinachopeleka maji river nile, Ambapo misri ni final destination kama mpokeaji maji kutoka ziwa victoria.

Hivyo basi sisi watanzania tukiwa na project (irrigation schemes) nyingi kama hzi kiwago cha maji kitakacho kua kinapotea kila siku kitakua kikubwa, Na kupelekea kiwango cha maji kupungua nchini misri.
Tukumbuke kwamba maji hadi yafike misri yanipita sudani na uganda ambapo pia yatatumika katika miradi mbalimbali.

Egypt ni nchi inayotegemea sana kilimo(large scale agriculture) kwa kutumia njia ya umwagiliaji.

Hitimisho.
Egypt ili wafanikishe kilimo cha umwagiliaji wanategemea maji kutoka victoria kupitia mto nile.
Kiwango cha wingi au uchache wa maji mto nile unategemea sana utumiaji wetu maji sisi watanzania.
Sasa sisi ziwa lipo kwetu, kwanini tusitumoe kwa maslahi yeteu na tumuangalie maslah ya wamisri?
 
Tukilitumia ziwa Victoria kwa kilimo cha umwagiliaji tutajiongezea uhakika wa chakula toka akiba ya sasa tani 1.5 million za sasa mpaka tani 4 million na kusahau njaa
 
kijiografia pia misri wapo karibu na bahari ya mediteraniani sasa basi kwann wasitumie hiyo bahari pindi wakiona maji yamepungua ebu wacha maneno yako mkuu maji yanatoka kwetu alafu tupewe mashart tena ya kuyatumia
hata hivyo bahar ya shamu ipo karibu na ndio maana waisraeli walikimbilia huko coz waliona ni karibu hivyo basi hawa watu wasitegemee ziwa victoria

Hapo ndo ujue kwamba serikali yetu inathamini sana maslahi ya Egypt kuliko sisi watanzania.
Haiwezekani misri wapewe kipao mbele ya matumizi ya ziwa victoria wakati nchin kwetu bado tunaupungufu wa maji hata kwa baadhi ya mikoa inayozunguka ziwa.

Kuna wanasiasa kadhaa wa Tz ambao wanasimama kidete kwa maslahi ya misri na sio kwa taifa.
 
Kuna miradi ya kilimo ya Bugwema Kakono Buswahili nk tafiti zimefanyika tangu miaka ya 70. Implementation ni shida kisa pesa.

Ukienda WB kukopa pesa ya mradi unakutana na kigingi cha mmisri kwa kisingizio miradi hailipi.
 
Back
Top Bottom