Tetesi: Kuna viongozi wanaolipwa na serikali ya Misri ili tusitumie maji ya ziwa Victoria

Tetesi: Kuna viongozi wanaolipwa na serikali ya Misri ili tusitumie maji ya ziwa Victoria

Nilishangaa kuona Membe anataka tusiyatumie maji ya Ziwa victoria eti kwa sababu Misri itaathirika. Akaenda mbele hata k kuzishawishi nchi za Maziwa makuu kuifikiria Misri zaidi kwa madai eti sisi nchi za ukanda huu wa kusini mwa mto nile tunapata mvua za kutosha! Huyu Membe mtu wa ajabu sana!.

Wao Misri wana bahari ya mediteranian, wanaweza kufanya desalination.

Misri wana Jangwa la Sahara. Ambayo chini yake huenda kuna maji mengi kama ambayo Libya waligundua.

Isitoshe sisi tuna mgogoro wa Ziwa Nyasa, sasa inakuwaje anagive up rights za Watanzania kuyafaidi Maji ya Ziwa hilo la Victoria?

Huyu Membe hatufai,angetuuza!!
alafu kawa balozi wako, mwishoe atakunyima visa huko alikoenda tuweni macho
 
Ziwa victoria ni chanzo kinachopeleka maji river nile, Ambapo misri ni final destination kama mpokeaji maji kutoka ziwa victoria.

Hivyo basi sisi watanzania tukiwa na project (irrigation schemes) nyingi kama hzi kiwago cha maji kitakacho kua kinapotea kila siku kitakua kikubwa, Na kupelekea kiwango cha maji kupungua nchini misri.
Tukumbuke kwamba maji hadi yafike misri yanipita sudani na uganda ambapo pia yatatumika katika miradi mbalimbali.

Egypt ni nchi inayotegemea sana kilimo(large scale agriculture) kwa kutumia njia ya umwagiliaji.

Hitimisho.
Egypt ili wafanikishe kilimo cha umwagiliaji wanategemea maji kutoka victoria kupitia mto nile.
Kiwango cha wingi au uchache wa maji mto nile unategemea sana utumiaji wetu maji sisi watanzania.


Kwahiyo nini hitimisho la mchango wako?
 
hii habari niliwahi isikia na jamaa akamtaja mtu mkubwa tu serikalini katika awamu iliyopita na alikuwepo kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mwaka 2015, kumbe haya madai ni kweli, aisee, basi hawa jamaa wanatuua sana, nenda ukerewe waliozungukwa na ziwa victoria, shida ya maji ile mbaya,
 
kuna mtu yuko na JK leo huko addis analeta ngonjera zake JF usiku huu kuteteta ujinga
 
Back
Top Bottom