Kuna tuhuma kuwa baadhi ya viongozi wa awamu iliyopita na wengine wa awamu hii wako kwenye payroll ya serikali ya Egypt ili kuzima au ku sabotage kwa namna mbali mbali miradi ya kilimo cha Umwagiliaji na matumizi mengine ya maji toka ziwa victoria
Baadhi yao wako ndani ya idara mbali mbali za serikali na maslahi yao ni kwa ajili ya serikali ya Misri na sio Tanzania
Imefika mahala baadhi ya miradi imepigwa chini na watu wa idara ya mazingira kwa visingizio mbali mbali kuwa ili watanzania wasitumie maji ya aiwa victoria
Naomba wenye kujua undani wa haya madai watujuze kwa nini tumewekewa restriction kutumia maji wakati Ethiopia na Sudan wanaendelea na miradi mikubwa mikubwa ya Umwagiliaji na Mabwawa makubwa ya umeme na kadhalika huku sisi tunaambiwa kuwa maji kwenda Shinyanga na mikoa mingine haiwezekani kwa kiwango cha kutosheleza wananchi.
Huko juu Ethiopia wao wameamua kujenga na KUMALIZA kujengaBwawa la umeme kubwa kuliko yote Africa kwenye mto Nile ambao chanzo cha maji yake ni huku kwenye ziwa Victoria
SHERIA
Kuna watu watakuja hapa kukujazeni ujinga wao kuwa kuna mkataba wa 1929 ambao lazima sisi tuuheshim
Ukweli ni kuwa:
1. MKATABA ulikuwa kati ya serikali ya kikoloni ya UINGEREZA na MISRI
2. Kuna mkataba wa Vienna wa
The Vienna Convention on Succession of States in Respect of Treaties, ibara ya 16, inasema kuwa mataifa huru au yaliyopata uhuru kama TANGANYIA/TANZANIA hayahitaji kurithi treaty obligations of its colonial power.
Someni mkataba wa Vienna ambao sisi ni signatory na link hii hapa:
http://legal.un.org/ilc/texts/instruments/english/conventions/3_2_1978.pdf
Hili ni jambo muhimu sana. Ila kabla hatujaenda mbali nikukumbushe kwamba mradi wa umeme wa Ethiopia ulioutaja uko kwenye tawi la mto Nile kutoka milima ya nchini Ethiopia nadhani mto wao unaitwa White Nile; ambapo tawi la pili (Blue Nile) ndilo linaanzia Lake Victoria etc.
Pili ni vema wataalamu waje na takwimu kuhusu athari za kila mradi wa matumizi ya maji ya ziwa Victoria (kwa nchi zote za Afrika Mashariki na kueleza jinsi outflow ya maji itakavyopungua katika mto Nile pale Jinja kuelekea Misri.
Nasema hivi kwasababu enzi za Wajerumani kulikuwa na mpango wa kuchimba mfereji kupeleka maji sehemu za Shinyanga na Tabora. Kwa mahesabu yao Wajerumani walionyesha kwamba mradi huo sio tu, usingeathiri kiasi cha maji kinachotoka ziwa Victoria kwenda mto Nile; bali hesabu zao zilionyesha kwamba maji yanayopotea kwa mvuke wa jua (L. Victoria surface evaporation) kwa mwaka mzima ni mengi kuliko maji ambayo yangeondolewa kupitia mfereji huo. Ambao volume ya maji iliyokusudiwa ilikuwa mara kumi na zaidi ya mradi wa bomba la Kahama!
Lakini pia zipo taarifa kwamba kina cha ziwa Victoria nacho kinazidi kupungua kutokana na siltation, inayosababishwa na deforestation kwenye catchment area ya ziwa na maeneo mengine. Kwahiyo future ya Lake Victoria inategemea mambo mengi pamoja na matumizi ya maji kwa umwagiliaji.
Tusingoje Wamisri watusemee au waje na data zao kupinga miradi yetu halafu sisi tusiwe na zetu. Ikiwa hivyo itabidi tuwe tunasalimu amri za watu wengine.