Tetesi: Kuna viongozi wanaolipwa na serikali ya Misri ili tusitumie maji ya ziwa Victoria

Tetesi: Kuna viongozi wanaolipwa na serikali ya Misri ili tusitumie maji ya ziwa Victoria

mh huogopi sandarusi?
Hivi tumefika hapa kweli?
256px-River_Nile_map.svg.png

Kuna tuhuma kuwa baadhi ya viongozi wa awamu iliyopita na wengine wa awamu hii wako kwenye payroll ya serikali ya Egypt ili kuzima au ku sabotage kwa namna mbali mbali miradi ya kilimo cha Umwagiliaji na matumizi mengine ya maji toka ziwa victoria

Baadhi yao wako ndani ya idara mbali mbali za serikali na maslahi yao ni kwa ajili ya serikali ya Misri na sio Tanzania

Imefika mahala baadhi ya miradi imepigwa chini na watu wa idara ya mazingira kwa visingizio mbali mbali kuwa ili watanzania wasitumie maji ya aiwa victoria

Naomba wenye kujua undani wa haya madai watujuze kwa nini tumewekewa restriction kutumia maji wakati Ethiopia na Sudan wanaendelea na miradi mikubwa mikubwa ya Umwagiliaji na Mabwawa makubwa ya umeme na kadhalika huku sisi tunaambiwa kuwa maji kwenda Shinyanga na mikoa mingine haiwezekani kwa kiwango cha kutosheleza wananchi.

Huko juu Ethiopia wao wameamua kujenga na KUMALIZA kujengaBwawa la umeme kubwa kuliko yote Africa kwenye mto Nile ambao chanzo cha maji yake ni huku kwenye ziwa Victoria

C2hd6jQXUAA9n_t.jpg:large

ges_velykaya_plotyna_efyopskogo_vozrozhdenyya_3d_2.png
 
Hizi conspiracies ziko duniani kote.Wapo walioko kwenye payroll ya Masonic organizations ili kufanikisha Masonic agendas,kama kuharibu elimu,kuharibu kilimo,na depopulation through kufumbia macho vyakula vyenye sumu nk. Sitashangaa kama hii itakuwa kweli.Serikali ilifanyie kazi kwa kutuimia vyombo vyake vya usalama.
Ukweli utabaki pale pale kuwa Misri can't enjoy the benefits of having access to the sea, while blocking a country like Tanzania from profiting from the fact that it sits at the source of the Nile
 
Ziwa victoria ni chanzo kinachopeleka maji river nile, Ambapo misri ni final destination kama mpokeaji maji kutoka ziwa victoria.

Hivyo basi sisi watanzania tukiwa na project (irrigation schemes) nyingi kama hzi kiwago cha maji kitakacho kua kinapotea kila siku kitakua kikubwa, Na kupelekea kiwango cha maji kupungua nchini misri.
Tukumbuke kwamba maji hadi yafike misri yanipita sudani na uganda ambapo pia yatatumika katika miradi mbalimbali.

Egypt ni nchi inayotegemea sana kilimo(large scale agriculture) kwa kutumia njia ya umwagiliaji.

Hitimisho.
Egypt ili wafanikishe kilimo cha umwagiliaji wanategemea maji kutoka victoria kupitia mto nile.
Kiwango cha wingi au uchache wa maji mto nile unategemea sana utumiaji wetu maji sisi watanzania.
Walewale mliokunywa uji wa mgonjwa
 
Bac wote wa kupongezwa sio cooz lowasa yupo upnzn aszungumzwe kwa mazuri ni ujnga wa zaid ya knyumbu mhm tujuzane kama kwel watu wanalipwa na Egypt kama wamaajliwa hawahujum nch sio hoja hata kdogo hapa tunataka kujua ishu ya lugum iliishia WAP na wale waliochukua hela za kutengengeneza share hewa za jesh LA police b63 alizsema babaetu mwen yewe akiongea na maafsa WA police sio udaku!
 
Mbona unamungunya maneno ?Waziri wa mambo ya nchi za nje alietoka alipinga kutumia maji ,je alitaka kuwa raisi wa Tanzania au wa Misri?
Njaa na uroho wa kujilimbikizia mali tu sijui hawajui ipo siku watakufa nakuicha dunia[emoji57]
 
Ziwa victoria ni chanzo kinachopeleka maji river nile, Ambapo misri ni final destination kama mpokeaji maji kutoka ziwa victoria.

Hivyo basi sisi watanzania tukiwa na project (irrigation schemes) nyingi kama hzi kiwago cha maji kitakacho kua kinapotea kila siku kitakua kikubwa, Na kupelekea kiwango cha maji kupungua nchini misri.
Tukumbuke kwamba maji hadi yafike misri yanipita sudani na uganda ambapo pia yatatumika katika miradi mbalimbali.

Egypt ni nchi inayotegemea sana kilimo(large scale agriculture) kwa kutumia njia ya umwagiliaji.

Hitimisho.
Egypt ili wafanikishe kilimo cha umwagiliaji wanategemea maji kutoka victoria kupitia mto nile.
Kiwango cha wingi au uchache wa maji mto nile unategemea sana utumiaji wetu maji sisi watanzania.
Kwa hiyo?
 
Hapo ndo ujue kwamba serikali yetu inathamini sana maslahi ya Egypt kuliko sisi watanzania.
Haiwezekani misri wapewe kipao mbele ya matumizi ya ziwa victoria wakati nchin kwetu bado tunaupungufu wa maji hata kwa baadhi ya mikoa inayozunguka ziwa.

Kuna wanasiasa kadhaa wa Tz ambao wanasimama kidete kwa maslahi ya misri na sio kwa taifa.
Ndiyo maana mleta uzi kakueleza kuwa kuna viongozi wa siasa nchini mwetu wapo kwenye payroll la Misri kupiga hela, ili kuhakikisha kwamba wazawa hatufurukuti "kuyanywa" maji ya ziwa hilo.
Kila mtakapojaribu kufurukuta kubuni miradi mbalimbali ya umwagiliaji ama kuyavuta kwa masafa marefu yafaidishe waTz walio wengi, wao hudhoofisha kwa kutumia madaraka ama ushauri wa blahblah, ili mradi jambo hilo lisifanyike.
Haiwezekani tukabweteka kulialia na visingizio lukuki vya mvua kutonyesha, wakati tumezungukwa na maji ya maziwa makuu na bahari ya hindi.
Wayahudi na Wafilisti wanafanya kilimo kikubwa cha umwagiliaji kwa kuyapoza maji chumvi ya bahari ya mediterenian, kulikoni sisi?
Nataka kuyasadiki maneno ya mtoa uzi kulingana na ukimya wa wanasiasa juu ya utumiaji wa rasilimali maji yatuzungukayo kuiepusha nchi na baa la njaa. Kwanini kimya?
 
Walioingia mikataba ndio hao hao walioweka mipaka mpaka hii leo unaona Egypt si nduhu zako. Wameamua wewe uwe nani, uitwe jina gani, jirani yako awe nani, uwe dini gani na uamini katika kitu kisichoonekana kiitwacho mpaka lakini kitu hicho kikuingie akili mwako mpaka uwe hata radhi kufa kwa ajili ya kuulinda mpaka japo hauonekani

Mkuu Domokaya:
Sasa umeanza kufunguka. ....Kudos....
Je ni vyema ufe njaa na familia yako kutokana na ukame wakati mto unao tiririsha maji unapita mbele ya nyumba yako kwa sababu ya hao hao walio tuletea vitu vya kusadikika.
Sisi hatukuwepo na wala hatuku husishwa kwenye huo unao itwa mkataba.
Je huo mkataba ulihusisha mabadiliko ya tabia nchi.
Mkataba si msahafu, ni wakati wa kukusanya fikra/nguvu za pamoja ili tujenge hoja timilifu.
 
Tafuta kwanza mkataba wa matumizi ya maji ya Lake Nile na Victoria kwanza The Nile Water Agreement of 1929 ndipo uju na hizi allegations. Nakushauri uwe unafanya kwanza home work kwa kina kabla hujafanya tuhuma kwa watu kwa kujisingizia eti unauliza.
Kaeleza vizuri hizo agreement za kitumwa za mwaka '29 zilivyo na mbadala wa kuzipangua.
Sasa wewe inaonekana ni wale anaotuhabarisha kuwa ni wafaidika mahsusi ama ni masalia wao, kwaajili ya kukwamisha ama kuvuruga "mpango mzima".
Haiwezekani ukakuta msibani watu wanalia, wewe ukaanza kucheka! Lazima wakutilie mashaka juu ya afya ya akili zako.
 
Shoga Sblandes alivyoukataa ndio ikawa nini? Kama alivyoshindwa katika mipaka iliyowekwa na wakubwa zetu, hakuwa na mamlaka na huo mkataba ndio maana mpaka anakufa huo mataba unafanya kazi. Tujifunze kuutambua ukweli na tuache kuukumbatia upashkuna, uongo na uzandiki kwani hivyo havitatui matatizo yanayotukabili, vinakidhi kiu ya ashki zetu za kutoa maneno ya ovyo ili tuonekane wa maana na wasiojua wenzetu
Wewe ni mtanzania au wamisri
 
Mkuu Domokaya:
Sasa umeanza kufunguka. ....Kudos....
Je ni vyema ufe njaa na familia yako kutokana na ukame wakati mto unao tiririsha maji unapita mbele ya nyumba yako kwa sababu ya hao hao walio tuletea vitu vya kusadikika.
Sisi hatukuwepo na wala hatuku husishwa kwenye huo unao itwa mkataba.
Je huo mkataba ulihusisha mabadiliko ya tabia nchi.
Mkataba si msahafu, ni wakati wa kukusanya fikra/nguvu za pamoja ili tujenge hoja timilifu.

Mwiba hutolewa pale ulipoingilia! Hayo ndio maneno ya kusema, hoja ijengwe taratibu zifuatwe mkataba urekebishwe na si kusambaza uongo na kuwasingizia watu mambo ya kizushi. Mkataba umeingiwa mwaka 1929 wazandiki wanataka kutuaminisha waliosababisha ni waziri wa mambo ya nje wa awamuiliyopita na maafisa wa serikali. Huu ni uongo, tena uongo wa kiinga, wa kipumbavu na wa kilofa
 
Kaeleza vizuri hizo agreement za kitumwa za mwaka '29 zilivyo na mbadala wa kuzipangua.
Sasa wewe inaonekana ni wale anaotuhabarisha kuwa ni wafaidika mahsusi ama ni masalia wao, kwaajili ya kukwamisha ama kuvuruga "mpango mzima".
Haiwezekani ukakuta msibani watu wanalia, wewe ukaanza kucheka! Lazima wakutilie mashaka juu ya afya ya akili zako.

Kuna muda huwa najiuliza kama kuna watu wengine hufikiri hata kidogo. Hiyo Geneva convention inayotaka tukatae mikataba iliyoingiwa na wakoloni ime classify ni mikataba ya aina gani? Kama huo utaifa tu ni mikataba ya kikoloni sasa tunaweza tukakataa nini? Tupo commonwealth halafu tukatae mikataba iliyoingiwa na waingereza. Aaaaa, ngoja nifanye mengine, maana kama huwezi kufikiri halafu ukataka uweze kufikiri kwa kusema tu 'mimi najua kufikiri' bila kujifunza kufikiri kamwe hutoweza kufikiri. Mungu atutetee!
 
Back
Top Bottom