Kuna tuhuma kuwa baadhi ya viongozi wa awamu iliyopita na wengine wa awamu hii wako kwenye payroll ya serikali ya Egypt ili kuzima au ku sabotage kwa namna mbali mbali miradi ya kilimo cha Umwagiliaji na matumizi mengine ya maji toka ziwa victoria
Baadhi yao wako ndani ya idara mbali mbali za serikali na maslahi yao ni kwa ajili ya serikali ya Misri na sio Tanzania
Imefika mahala baadhi ya miradi imepigwa chini na watu wa idara ya mazingira kwa visingizio mbali mbali kuwa ili watanzania wasitumie maji ya aiwa victoria
Naomba wenye kujua undani wa haya madai watujuze kwa nini tumewekewa restriction kutumia maji wakati Ethiopia na Sudan wanaendelea na miradi mikubwa mikubwa ya Umwagiliaji na Mabwawa makubwa ya umeme na kadhalika huku sisi tunaambiwa kuwa maji kwenda Shinyanga na mikoa mingine haiwezekani