Kuna viongozi wengi ni Usalama wa Taifa!?

Kuna viongozi wengi ni Usalama wa Taifa!?

Mbona kashindwa sasa kuzuia makamanda kina soka, saanane wasipotezwe ?...au mbona kashindwa kufahamu hata waliopo ?
Kwasababu level yake ni informer, anavuta posho, tokea lini Mangi akaacha posho?
Upande mmoja analamba asali ya Mama, upande mwingine anapokea posho za kitengo, na upande mwingine ni Jackpot la Ruzuku.

Halafu ati tunamuambia amuachie Lissu😆
 
Mkuu Mundu, Kamundu , kwa lengo la kusaidiana tuu, kukusaidia wewe na wengine wasiojua, kumtaja kwa majina mtu yoyote wa TISS na kumu expose kuwa ni TISS, huyo mtu akiwa ni TISS kweli, then kumtaja kwa jina ni kosa la jinai!.

I can just imagine, kama sisi tuliajaliwa jicho la tatu, ma Tiss tunawajua kwa kuwaona tuu sura, je tungewataja ma Tiss wote tunaowajua, tungebaki salama?
Huwezi kutoboa boti mnayasafiria. Ikizama mnakufa wote!, au kulikata tawi la mti uliolalia!.

Kwa taarifa yako ma TISS ni wengi kuliko unavyodhania hata Sultani naye ni Tiss, hata Mkuu nanilii pia ni Tiss
Ila sio kila Tiss ni Tiss

Kuna Tiss wa aina 3.
  1. Staff hawa ni waajiriwa, wafanyakazi wa Tiss, ni watumishi wa mishahara, hawa staff wako wa aina mbili, kuna open staff, hawa wanajulikana kama DGIS na maofisa wote wa TISS wanaojulikana kama RSO, ma DSO etc, hawa kuwataja hakuna tatizo, ila kuna ma SS, secret service, hawa hawatakiwi kujulikana, na ikitokea ukawajua, huruhusiwi kuwataja!.
  2. Viongozi wote, wateuliwa wote na watendaji wote, hawa ni ma Tiss kwa mujibu wa positions zao, wakiwemo mabenki yote yana mtu wa kitengo cha FIU hawa ni ma TISS, taarifa ya FIU lazima ipite kwa bank manager hivyo mameneja wote wa financial institutions zote ni ma Tiss.
  3. Informers, hawa ni watu wa kawaida wanakuwa recruited kuripoti Tiss na kulipwa posho tuu, huku wakiendelea na shughuli zao.
NB. Mimi nina damu ya TISS kwenye veins zangu kwa wazazi wangu wote wawili, na tumezaliwa 8, haiwezekani sisi wote nane tukawamo!. Kunidhania mimi ni mmoja wao rukhsa na angalia hapa ninavyoisifia ofisi yangu TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Hapa namtishia bosi wangu Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe

Na kunapotokea matishio ya kiusalama, badala ya kuripoti ofisini, mimi naripoti jf Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

P.
Mmmh ngumu kumeza kaka,,tamu kusikiliza,lkn nakumbuka kuna uzi aliwahi kuutoa humu yeriko Nyerere,jinsi wafanyavyo kazi watu hawa,na mtu 1 yuko swideni nadhani,ametunga kitabu kabisa,nadhani wanatoa elimu ili si raia tujue tu namna yakuishi nao,na si kuwataja, maana haifai kufanya hivyo.
 
Una mdogo wa kike? Around 30's hivi?

Nataka tu nijue kama ni mdogo wako...

Cc: Mahondaw
The family tuna 5 boys na 3 girls, na sisi Wasukuma ni ma jembe kazi, mimi nina 5 girls na 4 boys. Ila Mzee si haba, wadogo zangu kwa baba wametapakaa kila kona!. Ukimuona kama anafanana na mimi tuu ni wetu, binti yangu mwenyewe wa kwanza ni over 30!.
P
 
The family tuna 5 boys na 3 girls, na sisi Wasukuma ni ma jembe kazi, mimi nina 5 girls na 4 boys. Ila Mzee si haba, wadogo zangu kwa baba wametapakaa kila kona!. Ukimuona kama anafanana na mimi tuu ni wetu, binti yangu mwenyewe wa kwanza ni over 30!.
P
Hahaha...
Over 30yrs...

Msukuma!!
Dah!! Basi sikuulizi tena...
Nishapata jibu...


Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom