Kuna vita ya kilonzi inaendelea hivi sasa kati ya Simba na Yanga kuelekea musimu mpya wa ligi

Kuna vita ya kilonzi inaendelea hivi sasa kati ya Simba na Yanga kuelekea musimu mpya wa ligi

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Amini usiamini, simba na yanga wanajuana na ndio maana ni ngumu sana kwa vilabu vingine kugombea kombe lolote dhidi ya miamba hii miwili hapa nchini.

Azam anajitahidi kufurukuta ila anazidiwa nje ya uwanja (ulonzi)
Simba na yanga waneshaanza kupigishana shoti hivi sasa, wazee wanahaha huku na kule ili mambo yaende sawa pindi msimu mpya utakapo anza.

kwa simba na yanga usajili mzuri pekee siyo silaha ya mafanikio yao, nyuma ya pazia kuna sarakasi nyingi sana kulinda nyota za wachezaji wao.

Simba tofauti na misimu mitatu nyuma msimu huu waneamua kurudi kwa wazee wao kuweka mambo sawa, yanga nao misimu hii mitatu ya mafanikio, wazee wao walikuwa kitu kimoja pia usiri ulikuwa mkubwa mno kwenye mikakati yao.

Ndugu zangu kwenye maisha ya mwanadamu hakuna kitu kibaya kama (gundu) yaani unaweza kuwa msomi mzuri, mafanyaji wa kazi mzuri, ila watu wakipigisha shoti nyota yako basi utahangaika sana, kila unalolifanya hola. Kama usiposanuka, utasubiri sana.
 
Para ya mwisho ina ujumbe muhimu sana ila tusiache kumtumainia Mungu. Yeye ndiye muweza wa yote.
 
Back
Top Bottom