Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Kuna jamaa yangu mmoja mkila sahani moja utajuta,Yani anajiramba vidole kila baada ya tonge moja,elimu ya kula sharing wengi hawajui.
 
Mkuu Uchoyo na umasikini umetamalaki katika hoja hii,acha watu wakule wajisikie,imagine mgeni kanitembelea nikaamua kumchinjia kambuzi ka sh.50,000/= yanini ajibane,mwache akule hadi akunywe na mchuzi.

Ungeongelea utafunaji wa chakula ningekuelewa,lakini mtu kula chakula kingi nalo liwe kosa,hata akulee pleti sita huku kwetu ni kawaida,nikiangalia ndani Nina gunia kumi za mpunga kwanini mgeni wangu ajibane?

Hameni huko dasilamu mtakufa kwa misongo ya mawazo kisa wageni na mashemeji ,mkuje huku mikoani where we cultivate,we plant ,we weed,we harvest and then we eat,life in the village is very simple (in Mabala's voice)
 
Ukija huku kwetu kalambo ,tunakuchinjia mbuzi , kuku ni kifungua kinywa, maziwa utachangua mwenyewe unywe jagi la maziwa mgando au Lita mbili za maziwa fresh.( Usione aibu sisi huku kula Sana kazi iendelee)
Wakati wa kurudi kwenu Huko dar, tunakufungashia maziwa Lita 40, mchele kilo utakazoweza kubeba kwenye gari yako Hadi gari ikae Kama chura, maboga, maharage, matango, mayai ya kuku wakienyeji, Mahindi, unga wa Mahindi, kuku ,bata ,pilipili, matikiti maji.mjage na double cabine tuwafungie na mabeberu( mbuzi madume) mkachinje mjini mpate mboga ya kutusema tukija na mnatusema kweli kweli.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kweli mkuu nitie timu? Natafuta kashamba huko
 
Sijui ni ulafi au Uzungu, wewe kama umepika wachache si shida ni yako? kwanini usiweke kwenye sahani na mkashea hasa kwenye upande wa mboga? Hivyo vipande vitatu ni vya gram ngapi kila kimoja? Chakula cha manung'uniko bhana mwisho mtu anigwe na mfupa kisa jicho la usuda la kuchukua samaki mmoja (tena kagawanywa vipande vitatu) mwenye gram 400.

Kwani haufahamu siku hizi chakula ni mboga, YAANI MBOGA INAKUWA KUBWA ZAIDI YA WALI/UGALI?
Uchoyo tu unamsumbua, Usimsimange Binadamu mwenzio kisa Chakula.
 
Uchoyo tu unamsumbua, Usimsimange Binadamu mwenzio kisa Chakula.
Pichani, angalia wanavyokula kwa furaha, wakati unasikitikia samaki.
FB_IMG_1617908198823.jpg
 
Ukiwa na wageni halafu hujui kiasi gani wanachokula wakashiba, pika chakula cha kutosha. Baada ya mlo wa kwanza na wageni utatambua wanapenda kula chakula cha kiasi gani(ingawa wageni wengine wanaweza kula kidogo hata kama wanakula zaidi).

Ni heri chakula kibaki baada ya wote kutosheka/kushiba kuliko na wageni wale chakula waanze kunung'unika moyoni kisa umepika chakula kidogo(hili lilinikuta kwa ndugu yangu)
 
Back
Top Bottom