mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 88,759
- 123,368
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haaaaaaa [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] duu ulipataje aibu, sasa nawewe kwanini ulikuwa unaenda karibu na nyumbani haaa haa mtoto huyo noma , pole sana!Nikiwah kwenda ugenini....sasa sijui ilikuwa wananikomoa maana kiukweli chakula nilichokuwa naekewa hata mtoto hashibi mwanzoni niliona pengine wamekosea..huko mbeleni nikaona isiwe tabu cha kujitesa nn....nikila pale najivuta mtaani nazuga naenda kuangalia mpira napitia kibandani nakandamiza chipsi yai fresh, heeee! Sikh tupo sebleni dogo si akaropoka, Duuuh, uncle mchoyo sana chakula chetu tunampa ila yeye akila chipsi zake kule barabarani anajificha...dogo asijue nilikuwa namtoa shemeji hela kila asubuhi aongeze kwenye bajeti ya msosi licha ya kuachiwa hela na mumewe...hakuna siku nilijisikia noma kama siku hiyo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hahahaaa lazima nitoke kwenye hiyo meza aisee kwa maana nina kinyaa hatare
Sasa mgahawani na pesa uwe nayo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ha ha ha ha ha ha
Kwa upande wangu me nadhani kama una expect ugeni ni vema basi ukaandaa chakula ambacho wageni watakula na kufurahia na sio kujibana bana na kujutia.
Lakini kama ugeni ulikuwa ni wa ghafla ni vema ukawachukua wageni mkaenda mgahawani mkapiga menyu huko.....
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mgeni wa hivyo shida jamani kuishi naye, ni jamaa mmoja uwii akija halafu kanizoea ni muda wote kula kama nzige, Baba mwenye nyumba huwa ananitizama tu ninavyohaika naye kumpikia haaa haaa hata sijui na kwa wengine akienda haa haa haa![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kuna watu hadi ukitoka nae hapo unajiapiza huyu mbwa sitakwenda nae popote siku nyingine. Mtu anakula as if amekuja duniani kula tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sana...Watu wa hivyo very selfish.
Sana...
Nina wifi yangu ndiyo zake hizo, yeye hajali wenzake anapakuwa mboga nyingi wengine mtajua wenyewe. Siku hiyo nikamwambia wakati wa kula uwe unafikiria na wenzio.
Kakasirika kasema kwao na rafiki zake mimi nimemwambia anakula sana, basi saivi anakula chai nusu kikombe, km ni mkate slice1,chakula vijiko km 5 kashiba mpk kapungua.
Imeniuma sana najuta ht kumwambia vile ijapokuwa inakera sana
Usitilie shaka wala kujiskia vibaya kumkanya mtu anapokuwa na tabia mbaya. Tabia mbaya kukemewa ni lazima na mtu mwenye tabia mbaya hatakiwi kukasirika hata iweje.Sana...
Nina wifi yangu ndiyo zake hizo, yeye hajali wenzake anapakuwa mboga nyingi wengine mtajua wenyewe. Siku hiyo nikamwambia wakati wa kula uwe unafikiria na wenzio.
Kakasirika kasema kwao na rafiki zake mimi nimemwambia anakula sana, basi saivi anakula chai nusu kikombe, km ni mkate slice1,chakula vijiko km 5 kashiba mpk kapungua.
Imeniuma sana najuta ht kumwambia vile ijapokuwa inakera sana
Ukiambiwa ukweli unapofanya makosa, yale maumivu, hasira, ghubu na kisirani ndio tabia mbaya inatoka pale so inabidi ujifunze tabia mbadala ili uwe mtu safi.Mara nyingi wakosaji wakikosolewa wanaumia mno na kuona wameonewa. Sasa huyo si anajitesa tu bora angekubali kubadilika kuliko kufanya hasira kisa kaambiwa ukweli
Kwa kweli tumeumia wote. Ila tunamtizama tuMara nyingi wakosaji wakikosolewa wanaumia mno na kuona wameonewa. Sasa huyo si anajitesa tu bora angekubali kubadilika kuliko kufanya hasira kisa kaambiwa ukweli
Mimi hii kitu alinifundisha bro wangu. Nilikuwa na shobo saba na nyama. Na vyakula fast food kama soda, biscuits keki, etc, nilipoanza kazi, na kuanza kujitegemea nikawa navila hivi vyakula kwa uroho.Kuna baadhi ya watu bado haiwasaidii.
Bado wanaulimbukeni wa chakula.
Yaani akitoka akala au akapika kitu kizuri anaona siifa hadi anatangaza.
Ni kweli nakumbuka wakati wetu sinia lina wekwa hapo limejaa wali harage lime mwagwa juu watu tuna lifinyaaa likiisha tunaulizana jamani mmeona?tunajibu bado ngoma linapigwa la pili tuna kulaa hapo anaanza mmoja mmoja kuinuka ujue watu wameona sasa!!Binadamu ni social mammals, kula pamoja ni sehemu ya utamaduni wetu tangu enzi za mababu zetu. Tena kula pamoja ni kama tiba maana mtaongea na kucheka na wenzako.
Kitu cha kuzingatia ni ustaarabu tu mkiwa mnakula pamoja. Wengine wanaona ni kawaida ku fart saa ya kula kisa wamezoea kula wenyewe.
Huyo mama wa kula haraka nadhani atakua kakulia nakuolewa uswahilini aiseeKweli wazazi huwa baadhi wanafeli katika malezi.
Mtoto anafanya jambo la aibu unamuangalia tu hukemei unasahau kuwa yeye atachukulia sawa na tabia atakuwa nayo hadi utu uzima.
Kuna sherehe tulienda jirani akabeba wanae wote akaenda nap sasa mle ukumbini mezani zikaletwa sambusa acha waanze kugombania wakati zimeletwa idadi sawa na watu waliomo mezani na mama hakemei anaona tu kawaida.
Mwingine aliwekewa chakula akamfuata mama yake analia chakula kidogo mama akamjibu kula haraka ukarudie awamu nyingine.
Sasa watoto kama hao wakikua watakuwa na tabia gani kama sio za ajabu na wala haoni tatizo.
Mtoto usipomfunza na kumkemea anaweza kukutia aibu.
Sio watu wote walifundishwa nidhamu ya mezani (table manners) wasamehe tu malezi pia yanachangiaUnakaribishwa chakula kwenye familia, mabakuli makubwa ya chakula na mbogamboga yanawekwa katikati. Inakuja wakati kila mtu ajiwekee chakula anachopenda.
Mezani mpo nane. Wewe ni mtu wa tatu kujiwekea chakula, utamsikia shemeji leo umenipatia kweli, hawa samaki ndiyo ugonjwa wangu. Anachukua vipande vitatu pasi kufikiria watano wanaomsubiri watapata samaki.
Ustaarabu ni kuchukua chakula kidogo, subiri round ya kwanza iishe. Kama ulipenda sana samaki unaweza kujiongezea katika round ya pili kama watakuwa wamebaki. Wakati huo ndiyo unaweza kusema kama hakuna anaeongeza ninatongeza hawa samaki maana hiki ndiyo chakula ninachokipenda, leo shemeji umenipatia.
Kuna wengine anakula huku anashika smart phone yake mezani anaangalia messages. Jamani hao wanaokutumia hawawezi kusubiri mpaka umalize kula na wenzako? Kama una ujumbe wa muhimu sana deal la mahela unaweza kuwataarifu wenyeji wako kuwa kuna ujumbe ninautegemea lakini ni ustaarabu kuachana na simu wakati mko mezani.
Ndio maana sisi nyumbani tunapakua kwenye sinia kubwa kila kitu ni spidi yako tu na efficiency, na bahati yako kukaa upande mzuri utaweza kufaidi vinono. Shika smartphone uone kama utapata kitoweo
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Kama hatokei Kigoma Basi Ni Kanda ya ziwa.Kaka hapo kwenye shemeji umenipatia nilishapata kumuona kima mmoja mwenye tabia hizo.