Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Sijui ni ulafi au Uzungu, wewe kama umepika wachache si shida ni yako? kwanini usiweke kwenye sahani na mkashea hasa kwenye upande wa mboga? Hivyo vipande vitatu ni vya gram ngapi kila kimoja? Chakula cha manung'uniko bhana mwisho mtu anigwe na mfupa kisa jicho la usuda la kuchukua samaki mmoja (tena kagawanywa vipande vitatu) mwenye gram 400.

Kwani haufahamu siku hizi chakula ni mboga, YAANI MBOGA INAKUWA KUBWA ZAIDI YA WALI/UGALI?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ha ha ha ha ha ha


Kwa upande wangu me nadhani kama una expect ugeni ni vema basi ukaandaa chakula ambacho wageni watakula na kufurahia na sio kujibana bana na kujutia.

Lakini kama ugeni ulikuwa ni wa ghafla ni vema ukawachukua wageni mkaenda mgahawani mkapiga menyu huko.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu kisa kakaribishwa kaambiwa jiskie uko nyumbani. Kakaanga mayai tisa toka kwny tray. [emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Uroho mwingine bwana...... Sasa mayai 9 kweli jamani. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ila vijana ambao wanatokea maisha ya kipato cha chini wajifunze kutoa uroho kipindi cha kujitegemea. Kama kwenu walikuwa hawapiki vyakula unavyopenda kama kuku, chips, mayai, samaki, nyama, sijui maziwa etc. Then utakapo anaza jitegemea hebu anza kwanza kuishi pekee yako kwa muda ukiwa unajinunulia hizo vitu pekee yako na kuvila hadi uvizoee. Ukienda kwa mtu au ugenini hata ukikaribishwa hautaona ajabu kuviona hivyo vitu..... Na havitakushawishi sana....

Ila unakuta mtu maisha yake yote amezoea kula kuku kibawa au shingo, hajawahi kujiachia kula hata nusu kuku pekee yake..... Au kuku mzima.....

Kaa mwenyewe amua tu kwa kutenga bajeti, nunua hivi vitu na uvile kwa hamu hadi usaze. Utaona namna utavizoea na kuona hali ya kuvikifu mtu akikukaribisha kwake na kukupatia....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha nimemkumbuka jamaa fulani family friend wa dingi yangu mdogo ilikuwa kama kuna ka event hapo kwa mdingi mdogo basi yeye anawaambia kabisa kila mtu apakue ale ashibe yeye ni wamwisho kula maana anapita na kila kitu yani kiujumla jamaa alikuwa hapakui kwenye sahani bali kama ni hot pot anakula humo humo.

Halafu wala hakuwa na aibu na ni mtu mzima na mke wake yupo hapo hahaha.
 
Ilinitokea moja niko ugenini na mgen nilienda nae mimi wote tulikua wagen mgen alijaza wali mama mwenye nyumba akamkata jicho na mdomo ukakunjwa mimi ndio niliona jicho jamaa alikua anachekelea tu zamu yangu nikachota kias kidogo ila nikaona jamaa langu lilikosea unaenda kwa mtu bila miad alafu unskuta msosi usiku saa tatu hujui ratiba zao unajaza juuu mpala sahan inakua full hata ujiongezi

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Aisee watu wanaopakua milima huwa siwaelewi hata kidogo...... Yaani why mtu unachota chakula as if hautakuja kula tena.....?!

Ulafi ni tabia mbaya sana na unapokuwa mlafi unaonekana wazi wewe ni mbinafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwingine aliniuzi sana alikunywa chupa nzima ya chai ya maziwa na mkate nzima mdogo kisa hajawahi kula mkate wa karanga eti ni mtamu sana.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kuna watu hadi ukitoka nae hapo unajiapiza huyu mbwa sitakwenda nae popote siku nyingine. Mtu anakula as if amekuja duniani kula tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nilifundishwa na wazazi ukienda kwa mtu bila ya ahadi na ukakuta wanakula usile maana katika bajeti hujuwepo kabisa na ukiangalia ni sawa,mpaka leo hili nimeliweka kichwani.
Muda mwingine inakuwa ngumu sababu unapata picha gani umekwenda kwa watu wao wote wanakula halafu wewe umeketi tu hauli.

Hapo unachofanya unashika sahani unapakuwa kidogo sana cha kuzuga japo vijiko vitatu au tonge tatu. Then unakula taratibu sana ili uende sambamba na wenyeji wako. Baada ya hapo unatulia unaenda kunawa unaendelea na ratiba zingine.

Si kila familia watakuelewa mgeni ukija halafu usile. Kwao inawajengea picha mbaya kuwa wao ni wachoyo au sio wakarimu na pia wewe kuwa wakija kwako pia wasile.

Mfano mimi ukija kwangu kula ni lazima ule. Usije ukaja umekula, utatapika ule tena, kula ni lazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli ni kwamba waandaji mnatukosea waalikwa..
Unamualika mtu chakula cha mchana may be na unajua nyakat hzo ni njaa sana alf unatenga vi-hotpot vyenye chakula kidg kdg..hapa anaeumia huwa ni wa kwanza kupakua au wa mwisho..

Wa kwanza atapakua kukadilia wenzie wanaofata wa mwisho anaweza kutana na chakula kimebaki kdg,so hawa wanaweza wasishibe..

ukiamua kualika watu pika chakula cha kutosha hata wanapoondoka usibaki na manung'uniko,huwa mnatupa tabu ya kwenda kuongeza mlo mwngne vibandan huko kufidia nafas iliobaki wazi
[emoji23][emoji23] mkuu umeona useme ukweli eeeh
 
Me nikiwa naenda popote huwa nahakikisha nimekula kabisa japo nipo half way full. Ili nikienda kwa watu niwe comfortable wakati wa msosi au kama ni mtoko tuweze agiza hata chakula simple kama bites au dessert.

Lakini unapokwenda kwa watu na njaa zako hii huwa inakufanya kuwa na akili ambayo haipo under control. Hebu imagine unakwenda kwa rafiki yako halafu haujala tokea asubuhi ulipokunywa chai kavu.

Halafu unafika unakuta wameandaa msosi unaopenda. Hapo kujicontrol itakuwa ngumu sana kwakweli. Maana utaona kazi kweli kweli kujizuia unajikuta unajiachia tu bila kujua kuwa unachafuka CV.


Sent using Jamii Forums mobile app
Usiombee ikukute mkuu
 
Kuna baadhi ya watu bado haiwasaidii.
Bado wanaulimbukeni wa chakula.
Yaani akitoka akala au akapika kitu kizuri anaona siifa hadi anatangaza.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Uroho mwingine bwana...... Sasa mayai 9 kweli jamani. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ila vijana ambao wanatokea maisha ya kipato cha chini wajifunze kutoa uroho kipindi cha kujitegemea. Kama kwenu walikuwa hawapiki vyakula unavyopenda kama kuku, chips, mayai, samaki, nyama, sijui maziwa etc. Then utakapo anaza jitegemea hebu anza kwanza kuishi pekee yako kwa muda ukiwa unajinunulia hizo vitu pekee yako na kuvila hadi uvizoee. Ukienda kwa mtu au ugenini hata ukikaribishwa hautaona ajabu kuviona hivyo vitu..... Na havitakushawishi sana....

Ila unakuta mtu maisha yake yote amezoea kula kuku kibawa au shingo, hajawahi kujiachia kula hata nusu kuku pekee yake..... Au kuku mzima.....

Kaa mwenyewe amua tu kwa kutenga bajeti, nunua hivi vitu na uvile kwa hamu hadi usaze. Utaona namna utavizoea na kuona hali ya kuvikifu mtu akikukaribisha kwake na kukupatia....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ndio unasikia mgongano wa tamaduni.

Binafsi mimi kwetu Musoma, kwa kawaida unapikwa ugali mkubwa watu mnakaa round mnakula.

Sasa baada ya kuanza kuzurula kwenye mikoa ya watu nikaanza kupata changamoto.

1. Kisa cha kwanza, nilienda familia fulani wakati wa kula mimi nikawa namega tonge kubwa nakata ( maarufu kama chumba na sebule ) nikichunguza wenyeji wangu, wanamega tonge moja Moja. Ikabidi nijifunze na mimi kula kama wao. Ila sasa nikawa sometimes namega kubwa sometimes dogo 🤣🤣🤣 yaani ilikuwa tabu sana.

Nikawa sishibi kabisa, njaa muda wote.

Kumbuka ukiwa mgeni wenyeji hawawezi kushiba wote halafu wewe ukabaki unendelea kula ni Aibu.

( Ndio maana kwa Musoma mostly, mgeni hawezi kula peke yake na wewe kama mwenyeji hupaswi kuacha kula hata umeshiba mpaka mgeni ashibe )

2. Kisa cha pili, wewe probably kwenu huwa chakula kikitengwa ni kula tu, na wengine wanasali kwanza: sasa uko ugenini chakula kimetengwa kabla hawajasali wewe ushamega, wanaanza kusali wewe tayari una tonge umeshiiiria kwa AIBU. Hili limenikuta sana.

3. Kisa kingine kilimtokea Mshkaji wangu, yeye alienda zile familia za kujipakulia mwenyewe. Sasa chakula chenyewe wanapika kidogo. Na kibaya zaidi hizi familia nyingi za Pwani huwa usiku wanakula chai na chapati.

Sasa wameweka chapati 6 mezani, jamaa kachukua 4 mwenyewe vila kujua. Yaani tayari akawa katia hasara mtu mmoja kakosa.

Ukiachana na hayo, mimi kwetu siyo ufahari mtu kwenda chooni watu wanakuangalia. Nilivyoanza kuzurula kwenye mikoa mikubwa, nilipata tabu sana, unaamka asubuhi unakuta watu wamekaa nje yaani 🤣🤣 na wewe unataka kwenda chooni. Tabu sana

Kutembea na kujifunza tamaduni za watu pia ni vizuri maana kunafungua akili na kukufaya uweze kuwa na utu na ku embrace diversity.
Hiyo namba 2 hata mimi imenikuta sana
 
Kama mambo yenyeww ndio kusimangana hivi, mimi ndio maana huwa siwezi kwenda kwa watu. Mimi kwangu nusu ya dona nikipika unga unabaki kidogo sana hata kuupika tena inakuwa ngumu na bakuli linajaa nyama au samaki. Nikitaka samaki naenda mwenyewe Kunduchi kununua ninaowataka. Sasa wewe unikaribishe nyumbani kwako na habari za ubwabwa upawa mbili na kamchuzi na kakipande ka kasamaki, si bora nibaki kwangu tu. Huwa ni bora nisile kabisa, kuliko kuichokoza njaa kwa kichakula cha masimango.

Wasukuma Tunajuana
 
Hahaha nimemkumbuka jamaa fulani family friend wa dingi yangu mdogo ilikuwa kama kuna ka event hapo kwa mdingi mdogo basi yeye anawaambia kabisa kila mtu apakue ale ashibe yeye ni wamwisho kula maana anapita na kila kitu yani kiujumla jamaa alikuwa hapakui kwenye sahani bali kama ni hot pot anakula humo humo.

Halafu wala hakuwa na aibu na ni mtu mzima na mke wake yupo hapo hahaha.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwenye kula unaweza ukajisahau jamani! Mpaka ukishtuka ushatia aibu tayari ,[emoji1]
 
Kula mwenyewe raha sana. Unakula kwa style unayopenda.

Hizi table manners zikizidi huwa zinakera. Mfano wale wa hakuna kuongea wakati wa kula. Nyumbani kwangu ndo muda wa story maana kukaa pamoja tena ni muda wa kula kesho jioni.
 
Oya
My dear Sky Eclat

Ndio maana siku zote wazazi huwa wanashauriwa kuwa wanakula meza moja na watoto wao ili wawafundishe TABLE MANNERS ikiwamo kuwafikiria wengine na hata namna ya kutafuna chakula.

Inawezekana hao wageni ndio wale waliopelekwa boarding wakiwa bado wadogo sana (darasa la tatu) wakakosa muda wa kufundishwa tabia njema na wazazi/walezi wao.
dogo interview yako iliendaje?
 
Back
Top Bottom