Unakaribishwa chakula kwenye familia, mabakuli makubwa ya chakula na mbogamboga yanawekwa katikati. Inakuja wakati kila mtu ajiwekee chakula anachopenda.
Mezani mpo nane. Wewe ni mtu wa tatu kujiwekea chakula, utamsikia shemeji leo umenipatia kweli, hawa samaki ndiyo ugonjwa wangu. Anachukua vipande vitatu pasi kufikiria watano wanaomsubiri watapata samaki.
Ustaarabu ni kuchukua chakula kidogo, subiri round ya kwanza iishe. Kama ulipenda sana samaki unaweza kujiongezea katika round ya pili kama watakuwa wamebaki. Wakati huo ndiyo unaweza kusema kama hakuna anaeongeza ninatongeza hawa samaki maana hiki ndiyo chakula ninachokipenda, leo shemeji umenipatia.
Kuna wengine anakula huku anashika smart phone yake mezani anaangalia messages. Jamani hao wanaokutumia hawawezi kusubiri mpaka umalize kula na wenzako? Kama una ujumbe wa muhimu sana deal la mahela unaweza kuwataarifu wenyeji wako kuwa kuna ujumbe ninautegemea lakini ni ustaarabu kuachana na simu wakati mko mezani.
Hapa ndio unasikia mgongano wa tamaduni.
Binafsi mimi kwetu Musoma, kwa kawaida unapikwa ugali mkubwa watu mnakaa round mnakula.
Sasa baada ya kuanza kuzurula kwenye mikoa ya watu nikaanza kupata changamoto.
1. Kisa cha kwanza, nilienda familia fulani wakati wa kula mimi nikawa namega tonge kubwa nakata ( maarufu kama chumba na sebule ) nikichunguza wenyeji wangu, wanamega tonge moja Moja. Ikabidi nijifunze na mimi kula kama wao. Ila sasa nikawa sometimes namega kubwa sometimes dogo 🤣🤣🤣 yaani ilikuwa tabu sana.
Nikawa sishibi kabisa, njaa muda wote.
Kumbuka ukiwa mgeni wenyeji hawawezi kushiba wote halafu wewe ukabaki unendelea kula ni Aibu.
( Ndio maana kwa Musoma mostly, mgeni hawezi kula peke yake na wewe kama mwenyeji hupaswi kuacha kula hata umeshiba mpaka mgeni ashibe )
2. Kisa cha pili, wewe probably kwenu huwa chakula kikitengwa ni kula tu, na wengine wanasali kwanza: sasa uko ugenini chakula kimetengwa kabla hawajasali wewe ushamega, wanaanza kusali wewe tayari una tonge umeshiiiria kwa AIBU. Hili limenikuta sana.
3. Kisa kingine kilimtokea Mshkaji wangu, yeye alienda zile familia za kujipakulia mwenyewe. Sasa chakula chenyewe wanapika kidogo. Na kibaya zaidi hizi familia nyingi za Pwani huwa usiku wanakula chai na chapati.
Sasa wameweka chapati 6 mezani, jamaa kachukua 4 mwenyewe vila kujua. Yaani tayari akawa katia hasara mtu mmoja kakosa.
Ukiachana na hayo, mimi kwetu siyo ufahari mtu kwenda chooni watu wanakuangalia. Nilivyoanza kuzurula kwenye mikoa mikubwa, nilipata tabu sana, unaamka asubuhi unakuta watu wamekaa nje yaani 🤣🤣 na wewe unataka kwenda chooni. Tabu sana
Kutembea na kujifunza tamaduni za watu pia ni vizuri maana kunafungua akili na kukufaya uweze kuwa na utu na ku embrace diversity.