Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Unakaribishwa chakula kwenye familia, mabakuli makubwa ya chakula na mbogamboga yanawekwa kati kati. Inakuja wakati kila mtu ajiwekee chakula anachopenda...
Pole sana, lakini sio vizuri kuleta siri za shemeji yako humu ndani.

Halafu kwakuwa ni shemeji yako ilikupasa usubiri mkiwa peke yenu ndipo ungemchana huo ukweli "kishemeji".

The title is:- manners at the dinning table. 🤣
 
Ilinitokea moja niko ugenini na mgen nilienda nae mimi wote tulikua wagen mgen alijaza wali mama mwenye nyumba akamkata jicho na mdomo ukakunjwa mimi ndio niliona jicho jamaa alikua anachekelea tu zamu yangu nikachota kias kidogo ila nikaona jamaa langu lilikosea unaenda kwa mtu bila miad alafu unskuta msosi usiku saa tatu hujui ratiba zao unajaza juuu mpala sahan inakua full hata ujiongezi

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Wengine wanaushindilia wali na kijiko. Akipasi hotpot kwako liko nusu.
 
Wengine wanaushindilia wali na kijiko. Akipasi hotpot kwako liko nusu.


Poleni sana watu wa Dar, sisi huku mikoani mgeni akikaribishwa na akajipakulia Lumbesa ndiyo furaha yetu na faraja ya kumkirimu mgeni, hatuna takrima zingine mbali na msosi lumbesa.

Huko Dar chakula ni ghali mno hiyo ndiyo sababu ya manung'uniko yenu.

Mimi siwezi kuishi Dar katika hali ya kawaida, huko nasikia Embe dodo moja ni sh 1000---1500, wakati huku nilipo ni shs 250---300 nk.🤣
 
Poleni sana watu wa Dar, sisi huku mikoani mgeni akikaribishwa na akajipakulia Lumbesa ndiyo furaha yetu na faraja ya kumkirimu mgeni, hatuna takrima zingine mbali na msosi lumbesa...
Fikiria mgeni ameweka vipande vitatu na Junior akose kabisa samaki, inabidi Baba Junior atoe samaki wake ampe Junior. Mgeni atajisikiaje!
 
My dear Sky Eclat

Ndio maana siku zote wazazi huwa wanashauriwa kuwa wanakula meza moja na watoto wao ili wawafundishe TABLE MANNERS ikiwamo kuwafikiria wengine na hata namna ya kutafuna chakula...
Wengine si boarding bali ni malezi mabaya, kama wale wababa wapenda kuoa oa hawanaga muda wa kula na watoto wao muda wote wanawaza vimada
 
Sijui ni ulafi au Uzungu, wewe kama umepika wachache si shida ni yako? kwanini usiweke kwenye sahani na mkashea hasa kwenye upande wa mboga? Hivyo vipande vitatu ni vya gram ngapi kila kimoja? Chakula cha manung'uniko bhana mwisho mtu anigwe na mfupa kisa jicho la usuda la kuchukua samaki mmoja (tena kagawanywa vipande vitatu) mwenye gram 400.

Kwani haufahamu siku hizi chakula ni mboga, YAANI MBOGA INAKUWA KUBWA ZAIDI YA WALI/UGALI?
Nunua basi mpelekee shemeji yako akapike, sio kupiga domo tu hata chungwa la mia haubebi watoto wapokee bamdogo karudi[emoji23][emoji23][emoji23] ila kwangu kama samaki nitakujazia wewe tu!
 
Watu wa Dar acheni uchoyo kwanini msipike chakula kingi?..ndo mana mnakufa kwa stress mana moyoni mmejaza kila aina za uchoyo....
Sasa ndiyo bajeti zao, wewe umetoka mkoa hata kilo 5 za mchele hujabeba, unafika ndugu yako nyie mnapenda kula ugali usiku sie kwetu ni wali na ndizi sasa watu wakuelewe vipi jamani?
 
Back
Top Bottom