Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Sijui ni ulafi au Uzungu, wewe kama umepika wachache si shida ni yako? kwanini usiweke kwenye sahani na mkashea hasa kwenye upande wa mboga? Hivyo vipande vitatu ni vya gram ngapi kila kimoja? Chakula cha manung'uniko bhana mwisho mtu anigwe na mfupa kisa jicho la usuda la kuchukua samaki mmoja (tena kagawanywa vipande vitatu) mwenye gram 400.

Kwani haufahamu siku hizi chakula ni mboga, YAANI MBOGA INAKUWA KUBWA ZAIDI YA WALI/UGALI?
Tatizo si kupika kidogo, inawezekana wako wengine jikoni lakini ustaarabu ni kuhakikisha kilichotokea mezani kila mtu amepata na nyongeza ni ziada.
 
Mtoa mada punguza roho za njaa , wanawake vyakula vinawapaga stress.
Wewe unasema tu kwakuwa ni mwanaume, ila kuna wageni siyo wastaarabu kabisaa, na hapo ndo unaanza kuona mama mwenye nyumba mbaya kumbe mbaya wewe ambaye hujatumia ustaarabu kuto jali wengine vitu vinaenda kwa bajeti tena samaki walivyo bei halafu hawagawikagi unakuta watoto wanaambulia macho ya samaki kisa wewe mgeni

#kama mpo wengi nyumbani pika nyama ili kuepuka shari#[emoji16]
 
We ukija kwetu utaishi kwa tabu sana

Bi mkubwa wangu ukipakua paja moja la kuku anakuongezea yeye mawil..hahahah..hata muwe wangap kwenye meza.....sasa sis wengne tumeendeleza hyo tabia..


Hahah natania.......ila kwel bi mkubwa wangu sis watoto wa kiume alikua anatuoverload mda wa kula sana...
 
My dear Sky Eclat

Ndio maana siku zote wazazi huwa wanashauriwa kuwa wanakula meza moja na watoto wao ili wawafundishe TABLE MANNERS ikiwamo kuwafikiria wengine na hata namna ya kutafuna chakula.

Inawezekana hao wageni ndio wale waliopelekwa boarding wakiwa bado wadogo sana (darasa la tatu) wakakosa muda wa kufundishwa tabia njema na wazazi/walezi wao.
Absolutely right,
Kuacha Table manner viko vingi vya kuchunguza na kuwafunza wenetu.

Nimewahi kununiwa na staff mwenzangu baada ya kumrekebisha kuhusiana na uchakuaji(utafunaji) mbovu wa chakula.

Ni tabia mbaya kutafuna Kama mbuzi,hufungi mdomo pia unaongea.
 
Sky Eclat Kupakua chakula bila kujali wanao baki ni ujinga wa kukosa malezi Bora kutoka kwa wazazi, muhimu kwamba kitu kinapo kuwa kidogo mnagawana kidogo kidogo ili kila mtu apate.

Ila Tabia nyingine ambayo siipendi ni kubakiza chakula kwenye sahani, Kuna watu kubakiza chakula kwenye sahani wanaona fashion, wanachukia kingi cha nini Kama hawawezi kumaliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Absolutely right,
Kuacha Table manner viko vingi vya kuchunguza na kuwafunza wenetu.

Nimewahi kununiwa na staff mwenzangu baada ya kumrekebisha kuhusiana na uchakuaji(utafunaji) mbovu wa chakula.

Ni tabia mbaya kutafuna Kama mbuzi,hufungi mdomo pia unaongea.
Watu wengi wanatafuna Kama nguruwe sio mbuzi, mtu anatafuna mpaka nyumba ya nne wanasikia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unakaribishwa chakula kwenye familia, mabakuli makubwa ya chakula na mbogamboga yanawekwa kati kati. Inakuja wakati kila mtu ajiwekee chakula anachopenda.

Mezani mpo nane. Wewe ni mtu wa tatu kujiwekea chakula, utamsikia shemeji leo umenipatia kweli, hawa samaki ndiyo ugonjwa wangu. Anachukua vipande vitatu pasi kufikiria watano wanaomsubiri watapata samaki.

Ustaarabu ni kuchukua chakula kidogo, subiri round ya kwanza iishe. Kama ulipenda sana samaki unaweza kujiongezea katika round ya pili kama watakuwa wamebaki. Wakati huo ndiyo unaweza kusema kama hakuna anaeongeza ninatongeza hawa samaki maana hiki ndiyo chakula ninachokipenda, leo shemeji umenipatia.

Kuna wengine anakula huku anashika smart phone yake mezani anaangalia messages. Jamani hao wanaokutumia hawawezi kusubiri mpaka umalize kula na wenzako? Kama una ujumbe wa muhimu sana deal la mahela unaweza kuwataarifu wenyeji wako kuwa kuna ujumbe ninautegemea lakini ni ustaarabu kuachana na simu wakati mko mezani.
Naona umeamua kutusema sisi akina mabula na maduhu
 
Absolutely right,
Kuacha Table manner viko vingi vya kuchunguza na kuwafunza wenetu.

Nimewahi kununiwa na staff mwenzangu baada ya kumrekebisha kuhusiana na uchakuaji(utafunaji) mbovu wa chakula.

Ni tabia mbaya kutafuna Kama mbuzi,hufungi mdomo pia unaongea.
Sahihi kabisa mkuu
 
Ndio maana sisi nyumbani tunapakua kwenye sinia kubwa kila kitu ni spidi yako tu na efficiency, na bahati yako kukaa upande mzuri utaweza kufaidi vinono. Shika smartphone uone kama utapata kitoweo
 
Ndiyo maana leo huli bali unafukia, kumbe ulishazoeshwa na bi mkubwa wako kufukia, wewe hufai kukaribishwa na Sky Eclat, unafaa uje nyumbani kwangu ili uwe overloaded.[emoji1787]
Kabisa mkuu....na unawekaje samaki 8 exactly na idad ya wageni buana....weka misamaki yakutosha kama una wagen usibanie

Mi bi mkubwa wangu akiandaa meza aisee..mnaweza kula had mkatambaa
 
Back
Top Bottom