Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
WEKA UTAYARI KWA KILA MTU, SIKILIZA MAWAZO NA USHAURI WAO KWAKO LAKINI KUFANYIA KAZI NI UAMUZI WAKO.
Kwa nini ni vizuri kumsikiliza kila mtu?
Zipo sababu nyingi mno za ni kwa nini ni vizuri kumsikiliza kila mtu lakini sababu kubwa ni ukweli kuwa kila mtu kuna wakati anakuwa sahihi katika mawazo yake. Kwa mfano, hata saa mbovu ya mshale kuna wakati inasoma wakati sahihi ilipoharibikia.
Hii inatufanya kufahamu kuwa siyo kila wakati watu hukosea kukushauri ila kuna wakati wanakuwa sahihi sana katika kukushauri.
Ni kwa nini kufanyia kazi ushauri ni uamuzi wako?
Licha ya uwepo wa sababu lukuki ni jambo lisilopingika kuwa mwanadamu ameumbiwa uhuru wa kuchagua. Hivyo siyo lazima kila wakati watu wafanye kila kitu sawa na matakwa ya mtu fulani au watu fulani tu.
Masikio yapo wazi kusikia kila kitu na macho yapo wazi kuona ila akili ipo huru kuchagua cha kusikia na kuona.