Mimi najitegemea in fact, lakini hakuna maisha mazuri kama mke na mume kuwa marafiki, mume kumhudumia mke, na mke kumheshimu mume, naenjoy mume wangu akiniwekea vocha nikienda saluni lazima atauliza unataka sh ngapi kama nywele ni elfu 20 na ninajua siku hiyo hana kitu ntamwambia nahitaji 10 ingine nilimuachiaga dada wa saluni chenj yangu, au nyingine ntaongezea utanilipa.
Mwanamke unaesoma hapa elewa hata upate vipi hela please usimnyang'anye mwanaume uanaume wake,(manhood) aidha kwa maneno au matendo yako au kwa kujigamba , maintain his man hood please.
Huyo Mercy Mchechu alieongea hivyo amewapa sababu wanawake wandagaji kumtafuta mumewe.
Tuna maisha ya kawaida lakini mgeni akija kwangu kwa anachokikuta lazima atajifunza kitu, utashangaa sasa limama lizima likija linaniita pembeni eti unanyenyekeaje mwanaume atakuja kukusaliti, wanadam wote wanasaliti, ishi ndoa yako Leo sasa hivi, kwamba ulisalitiwa ilishapita utasalitiwa haijatokea bado, kwa hiyo tunaweza kusema mengi kutaka umaarufu lakini UKWELI upo pale pale, Mwanamke anaeaga ana nafasi kubwa ya kuaminimka kuliko asiyeaga, anayepewa hela kulingana na kipato cha mumewe anapendwa zaidi kuliko asiyepewa.