Mimi Jumong nimeitazama zaidi ya mara 4 ,na kila nikitazama naona kama muvi mpya yaani kuna vitu nagundua ambavyo siku vijua kabisa zamani ,ni muvi yenye akili mnonna mafunzo mengi sana.
Mimi series zangu kama nilitaka kuangalia ni Korea tu tena za zamani kijijini kuhusu historia na ufamle wazungu na wahindi kipindi hiko mdogo sana.Huyu jamaa ana movie yake nyingine ;
*Jang yeong-sill - ya kijijini imebase kuhusu mambo ya sayansi ila ni nzuri mno hiyo series ni shule tosha, japo imebase kwenye sayansi lakini wamebalance na kuingizie maudhui ya uongozi na chama za kiutawala ,ushupavu nk
*Emperor of the Sea - Hii nayo ya kijijini Star wa Jumong humo kama adui hii movie kwangu mimi badala ya Jumong hii ndio ya pili kwa ubora bado kidogo tu niseme hii ndio bora ya muda wote.Humo kuna shule kubwa ya kutokata tamaa ,nidhamu ,uaminifu nk.
Nakusanya data nikipata wasaa nitaandaa uzi maalaumu kwa ajili ya hiyo series ya Jumong pekee kukiwa na uchambuzi wa kina wa nyuma ya pazia kuhusu kila kitu.
View attachment 2603386