Kuna Watu hawafai jamani: Waliokaa chini wakatengeneza hizi Series nitawaheshimu siku zote

Kuna Watu hawafai jamani: Waliokaa chini wakatengeneza hizi Series nitawaheshimu siku zote

Mimi Jumong nimeitazama zaidi ya mara 4 ,na kila nikitazama naona kama muvi mpya yaani kuna vitu nagundua ambavyo siku vijua kabisa zamani ,ni muvi yenye akili mnonna mafunzo mengi sana.

Mimi series zangu kama nilitaka kuangalia ni Korea tu tena za zamani kijijini kuhusu historia na ufamle wazungu na wahindi kipindi hiko mdogo sana.Huyu jamaa ana movie yake nyingine ;

*Jang yeong-sill - ya kijijini imebase kuhusu mambo ya sayansi ila ni nzuri mno hiyo series ni shule tosha, japo imebase kwenye sayansi lakini wamebalance na kuingizie maudhui ya uongozi na chama za kiutawala ,ushupavu nk

*Emperor of the Sea - Hii nayo ya kijijini Star wa Jumong humo kama adui hii movie kwangu mimi badala ya Jumong hii ndio ya pili kwa ubora bado kidogo tu niseme hii ndio bora ya muda wote.Humo kuna shule kubwa ya kutokata tamaa ,nidhamu ,uaminifu nk.

Nakusanya data nikipata wasaa nitaandaa uzi maalaumu kwa ajili ya hiyo series ya Jumong pekee kukiwa na uchambuzi wa kina wa nyuma ya pazia kuhusu kila kitu.View attachment 2603386
Emperor of the sea nayo ni nzuri sana

Ninayo kwenye pc, narudiaga episode zote kama sijawahi kuiona hapo awali
 
The Veil
Six Flying Dragons
Deep Rooted Tree
Lee (Yi) Bang Won King of Tears
Slave Hunters

Kwakuwa Six Flying Dragons iligusia simulizi za kweli kuna baadhi ya characters ambao niliwakubali kama Yi Songye, Yi Bang Ji (Ddang Sae), Mu Hyul (alikuwa kabla ya kulitoa panga kwenye sheath anasema warrior Mu Hyul)

Royal Gambler
Hapa mwandishi wa Screenplay aliwaumba wahusika wake vizuri, kuna Baek Dae Gil, Yeoning , mfalme Sukjong, Yi In Jwa na yule binti ambaye alikuwa kwenye love triangle na Baek Dae Gil na Yeoning
Aisee Hidden roots na Six flying dragon nilizikubali sana hizo zingine sijaziona
 
Kwa wabongo Korean movies zimewateka akili sana lakini nafikiri ni sababu ya lugha ya malikia ila Nina watu kadhaa nafahamiana nao kutoka mataifa ambayo wanazungumza kimombo wanasema series ya 24 na prison break, ndio the best series ever .Nafikiri Wabongo kuto kumaster lugha ya malikia ipasavyo imetufanya kupenda Korean series sana kuliko series za western .ndio maana walio wengi wapo very limited juu ya maswala haya ya series more especially intelligence series wengi wanapenda movies za mapanga na mishale sababu hata kwa kuangalia action tu unajua mini kinamaanishwa.

Kiukweli series ya 24 Hours ni next level kwenye huu ulimwengu wa sasa.
 
images (54).jpeg


Hii pia Ina story nzuri 🔥
 
Back
Top Bottom