Kuna Watu hawafai jamani: Waliokaa chini wakatengeneza hizi Series nitawaheshimu siku zote

Kuna Watu hawafai jamani: Waliokaa chini wakatengeneza hizi Series nitawaheshimu siku zote

Sifagilii series zenye mapanga mara mafarasi,. Hunikalishi hata kwa mtutu

napenda za kutumia akili sana, yaani game za kiakili kabisa sio mamilio ya mafarasi tu. Naombeni majina nizitafute
 
Mimi Jumong nimeitazama zaidi ya mara 4 ,na kila nikitazama naona kama muvi mpya yaani kuna vitu nagundua ambavyo siku vijua kabisa zamani ,ni muvi yenye akili mnonna mafunzo mengi sana.

Mimi series zangu kama nilitaka kuangalia ni Korea tu tena za zamani kijijini kuhusu historia na ufamle wazungu na wahindi kipindi hiko mdogo sana.Huyu jamaa ana movie yake nyingine ;

*Jang yeong-sill - ya kijijini imebase kuhusu mambo ya sayansi ila ni nzuri mno hiyo series ni shule tosha, japo imebase kwenye sayansi lakini wamebalance na kuingizie maudhui ya uongozi na chama za kiutawala ,ushupavu nk

*Emperor of the Sea - Hii nayo ya kijijini Star wa Jumong humo kama adui hii movie kwangu mimi badala ya Jumong hii ndio ya pili kwa ubora bado kidogo tu niseme hii ndio bora ya muda wote.Humo kuna shule kubwa ya kutokata tamaa ,nidhamu ,uaminifu nk.

Nakusanya data nikipata wasaa nitaandaa uzi maalaumu kwa ajili ya hiyo series ya Jumong pekee kukiwa na uchambuzi wa kina wa nyuma ya pazia kuhusu kila kitu.View attachment 2603386
Dah mm kwa sasa najiona sina muda tena wa kuangalia series nahisi izo nilizoangalia zishanitosha mm ata Tv tu siangalii.Naangalia Mpira tu tena mara chache sanaa ila taarifa nyingi nazipata hapa Jf kwaio kwasasa sina muda na Tv kabisaa

Hua napenda niperuzi Jf au kusoma
 
Warriors baek dong soo
1682763165339.jpg
 
OST zao pia nazipenda sana na nyingine zinanifanya kuwa emotional naishia kulia huh!
OST ndicho kitu kinachonifanya nipende scenes na nikumbuke events fulani. Jumong track 7 nnayo kwenye simu, gradiator ninayo now we are free, spartacus ninayo ile theme ya sura, guang's family nnayo hii hizi violin zinacapture sana emotions zangu
 

Attachments

Kuna Jumong na A man called god zote ni korean, mtaalamu akiwa Song il gook, a.k.a Jumong

Jamani tuacheni maskhara, kwa upande wangu, movie/series zitakuja na kuondoka, hizi mbili ni mwisho

pongezi kwa wote waliofanikisha hizi series (directors, actors, etc), wamefanya kazi kubwa sana

kwa ambao washawahi ziona hizi series watakubaliana na mimi

______________________

jumong ni jina la mhusika mkuu katika tamthilia ya Kikorea ya Jumong ambayo ni moja ya tamthilia maarufu sana nchini Korea na ulimwengu kwa ujumla.

Tamthilia hii ilikuwa inahusu maisha ya Jumong, kiongozi wa kikabila wa kihistoria wa kundi la Wajoseon, ambaye aliishi katika karne ya tano KK. Jumong alikuwa shujaa wa vita na alipigana kwa ajili ya kujenga ufalme wake na kutetea watu wake. Tamthilia hii ilikuwa maarufu sana na ilipata umaarufu mkubwa katika nchi nyingi duniani kote kutokana na hadithi yake ya kuvutia na uigizaji mzuri.
View attachment 2603333


______________________
______________________

A Man Called god ni tamthilia ya Korea Kusini ambayo ilikuwa inahusu maisha ya Michael King, mtu wa kawaida ambaye alijikuta akihusika katika vita vya kisiri vya kimataifa baada ya kugundua siri ya familia yake. Baada ya kuwa na kifo cha ghafla cha baba yake, Michael King anajiweka katika safari ya kutafuta ukweli kuhusu familia yake na anajikuta akikabiliana na wapinzani wenye nguvu na hatari. Kupitia safari yake, Michael anapata ujuzi wa kupigana na kujifunza sanaa ya kijeshi na kuwa shujaa wa vita.

Tamthilia hii ilikuwa na mandhari ya kimataifa, na ilikuwa na ujumbe wa upendo, ujasiri na uaminifu. Ilipata umaarufu mkubwa nchini Korea Kusini na katika nchi nyingine za Asia, hasa kutokana na uigizaji mzuri na hadithi yenye kusisimua. Hata hivyo, tamthilia hii ilikuwa na baadhi ya matukio ya vurugu na maonyesho ya nguvu ambayo yanaweza kuwa sio ya kila mtu.
View attachment 2603335
Kwa kweli Jumong ndo movie yangu nambari moja duniani. Yaaan sijawahi kuchoka kuiangalia. Movie hii ilinifanya niipende nchi ya korea nipende product zake. Imefika hatua hata nikienda kununua nguo za mtumba ki ukweli naangalia imetengenezwa wapi,,nikikuta korea naibeba. Na niliweka ahadi Mungu akinipa uzima siku moja nitaenda kutembea korea. Khaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom