Kuna Watu hawafai jamani: Waliokaa chini wakatengeneza hizi Series nitawaheshimu siku zote

Kuna Watu hawafai jamani: Waliokaa chini wakatengeneza hizi Series nitawaheshimu siku zote

Mkuu Nafaka , kuna hii inaitwa Moon lovers, sijui ushaiona tayari?

Soundtracks za humu zina balaa pia 🔥🔥
images (13).jpeg
 
Ile njia ya kukimbia na kuchinja kwa haraka Yi Bang Ji naye alii-master alipopigana na Gil Tae Mi kule maeneo ya sokoni. Tae Mi alikuwa ameshaua wanajeshi wengi na watu walibaki wakimuogopa na kama sio Yi Bang Ji sijui hali inhekuwaje.

Tae Mi alimuuliza unaitwa nani maana nimekutana na shujaa, muda huo hata Mu Hyul naye alitamani kupambana na Gil Tae Mi ila Bang Ji alimuwahi.
Anamuomba at least ajue ameuwawa na nani
 
My love from another star ina most nzuri balaa, ikifuatia na chuno na pia za kwenye city hunter sio mbaya pia
 
Series ni INTO THE BAD LAND
LEGEND OF THE SEEKER

kwangu ndio babkubwa hakuna Korean
 
Kuna Jumong na A man called god zote ni korean, mtaalamu akiwa Song il gook, a.k.a Jumong

Jamani tuacheni maskhara, kwa upande wangu, movie/series zitakuja na kuondoka, hizi mbili ni mwisho

pongezi kwa wote waliofanikisha hizi series (directors, actors, etc), wamefanya kazi kubwa sana

kwa ambao washawahi ziona hizi series watakubaliana na mimi

______________________

jumong ni jina la mhusika mkuu katika tamthilia ya Kikorea ya Jumong ambayo ni moja ya tamthilia maarufu sana nchini Korea na ulimwengu kwa ujumla.


Tamthilia hii ilikuwa inahusu maisha ya Jumong, kiongozi wa kikabila wa kihistoria wa kundi la Wajoseon, ambaye aliishi katika karne ya tano KK. Jumong alikuwa shujaa wa vita na alipigana kwa ajili ya kujenga ufalme wake na kutetea watu wake. Tamthilia hii ilikuwa maarufu sana na ilipata umaarufu mkubwa katika nchi nyingi duniani kote kutokana na hadithi yake ya kuvutia na uigizaji mzuri.
View attachment 2603333

View attachment 2603975


______________________
______________________

A Man Called god ni tamthilia ya Korea Kusini ambayo ilikuwa inahusu maisha ya Michael King, mtu wa kawaida ambaye alijikuta akihusika katika vita vya kisiri vya kimataifa baada ya kugundua siri ya familia yake. Baada ya kuwa na kifo cha ghafla cha baba yake, Michael King anajiweka katika safari ya kutafuta ukweli kuhusu familia yake na anajikuta akikabiliana na wapinzani wenye nguvu na hatari. Kupitia safari yake, Michael anapata ujuzi wa kupigana na kujifunza sanaa ya kijeshi na kuwa shujaa wa vita.

Tamthilia hii ilikuwa na mandhari ya kimataifa, na ilikuwa na ujumbe wa upendo, ujasiri na uaminifu. Ilipata umaarufu mkubwa nchini Korea Kusini na katika nchi nyingine za Asia, hasa kutokana na uigizaji mzuri na hadithi yenye kusisimua. Hata hivyo, tamthilia hii ilikuwa na baadhi ya matukio ya vurugu na maonyesho ya nguvu ambayo yanaweza kuwa sio ya kila mtu.
View attachment 2603335
Dah,

Umenikumbusha aisee.

Kwenye jumong bana umenikumbusha Prince Taesso na na Prince Youngpo. Jamaa walikua hawampendi Jumong wakamfanyia kila aina ya vitimbi vya kutosha tu ila mwishoni aliwadhibiti.

Wapi chawa wa Jumong Oi, Mari na Hyoppo. Vibaka wa mtaani waliokuja kugeuka kua mawaziri kwe serikali ya Jumong.

Na mwisho ni swahiba wangu na rafiki yangu wa damu kabisa Cha Pombe Mo Palmo, mtaalam wa kutengeneza Silaha. Huyu loyalty yake kwa Jumong ni undoubted.

Hii series pamoja na kua na episodes za kutosha lakini niliiangalia kwa kuirudia zaidi ya mara tatu. Mwanzoni nilikubali mateso ya ITV niwe nakaa macho mpaka saa tano za usiku ilivyotoka.

Ila baadae alosto yake ilivyozidi nikaja kuzikuta zinauzwa kariakoo unanunua DVD moja ina episodes kama 10 hivi nikairudia.
 
Back
Top Bottom