Kuna watu hawana hela wanajenga, kuna watu tuna hela ila hatujengi

Kuna watu hawana hela wanajenga, kuna watu tuna hela ila hatujengi

Hongera sana hapa hatua nzuri,,,mimi nilifikia hapo nahitaji mwaka huu niendeleze
IMG_20220609_142116_769.jpg
 
Nahisi shida ni moja tu sisi wenye hela tunatamani kujenga kumpita fulani wakati asiye na hela hawazi anajenga vyovyote
Kabisa,inawezekana kabisa.Ngoja tukomae ilimradi watoto wapate pa kuishi....Nyumba za kupanga ni maumivu sana
 
Mishahara ya wizarani ni sawa TU na ya Halmashauri usidanganye Watu pesa huna, at least ungekuwa nssf,tpa,tra,bot,tanapa,ega,
Na anakaa dodoma bila kupenda
Kila siku kuuliza mafuta gan mazur kwa kuzuia kupasuka mdomo.kiwanja chake barabara ya 9 kwenye vitumbua pale na bajia
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
ukijua kupiga hesabu mfano
kuweka kila siku 3000 x30= 90000 unapata mifuko mingapi.!
basi utaweza kujua kujenga.
Kujenga kunataka hesabu hata kama unauza nyanya.

ili mradi kuthamini kipato chako kwa kidogo.alafu nyumba unaweza kujenga ukahamia na bado ukawa unaendeleza kuiboresha
Kujenga kwa kunyanyua boma sijawahi ona Ni shida Ila kuezeka Sasa huko ndio mziki ulipo,kupata Pesa yote kwa pamoja sio Jambo la mchezo.
 
tatizo ni kwamba mkikutana na wehu kwenye hizo bar mnazoenda wanawajaza ujinga wanawaambia kujenga ni uoga wa maisha na mlivyo na akili visoda mnawaskiliza

Kumbe wenzenu wanajua wanapochuma ela na nyumba wanazokaa ni za urithi. Influence mbaya itawapoteza vijana wengi anakuja kustuka na kujenga kwa ela ya kustaafu kazi kusumbua tu watoto
Safi sana. Nimeipenda hii. Warithi wana shida mnoo, wanarahisisha sana maisha.

Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom