Kuna watu hufa mara mbili

Kuna watu hufa mara mbili

Mmh hili la kupigwa hapana sijawahi kusikia, kwakuwa maiti ni kitu kinachoheshimiwa mno

Mimi nimewahi kusikia ilitokea ni baada ya kila gari iliyotumika kusafirishia maiti husika kupata tatizo lililosababisha gari isiendelee. Watu wakaamua kubeba maiti lakini kilichotokea maiti ikawa nzito hutembei hatua tano unaomba msaada mwingine aje kusaidia. Akatokea mmoja kwenye msafara akaomba sanduku lifunguliwe akaichapa vibao maiti huku anaigombeza. Baada ya zoezi hilo yaani kama wamebeba mwanzi.
 
Duu basi marehemu alikuwa mkorofi sana, na kwa vyovyote huyo aliyemzaba vibao ni mtu mwenye mamlaka naye
 
nimecheka sana,eti unamsindikiza maiti kwa teke na hanyanyuki tena!
 
Nimesoma uzi huu from A to Z. Kuna vitu vingi binadamu hatuvijui, na tunaoamini katika Mungu tunajua Mungu kazuia tusivijue ili tusiwe na hofu ya maisha yetu na tuzidi kuwa na amani...

Haswaa!! Mungu angetufunulia yote, wengi tungekuwa tunakufa ghafla kwa mshtuko. Ni wachache wanaoyaona mambo haya mara kwa mara na akili zao zikabaki salama; wengi wao huwa wanaathirika kwa sababu huwa wanaelemewa na msongo wa mawazo wa kufanyakazi isiyokuwa ya kawaida, tena kwenye mazingira ya upweke; mwishowe huishia uchizi. Kuchuna ngozi ya kichwa cha maiti, kupasua mafuvu na kupakua ubongo; au kupasua maiti kifuani hadi tumboni, kukata kidari na kukiweka pembeni na kutoa moyo, maini au figo, kuvipima kwenye mizani na kuvikatakata kwa uchunguzi, ni kazi nyepesi? Wachinjaji wanyama tu wa machinjioni akili zao huwa zina-twist kwa kumwaga damu kila siku; sembuse ku-deal na maiti, wakati na wewe ni maiti mtarajiwa wa uhakika? Lakini ndivyo maisha yalivyo. Waangalizi wa nyumba za maiti ni watu muhimu sana katika jamii yetu, japo jamii yenyewe inawaona kama watu waliokosa kazi za maana za kufanya! Fikiria kama wasingekuwepo, marehemu wetu wangetunzwa wapi na nani kabla ya mazishi? Au wewe na mimi tutakapokufa (maana tutakufa kwa hakika), maiti zetu zitatunzwa na nani kabla hatujazikwa? Zipo maiti ambazo ni lazima zifanyiwe uchunguzi baada ya kifo kwa sababu zinazokuwepo, ama za kitabibu au kisheria. Waangalizi wa vyumba vya maiti ndio wasaidizi wa madaktari kwenye kazi hiyo ngumu. Ndio wanaochuna, kupasua, kukata n.k kwa maelekezo ya daktari. Maiti ni Mwalimu asiyeongea, anatoa elimu kwa madaktari, elimu ambayo mtu aliye hai hawezi kuitoa. Hayo ndiyo maisha, tulizaliwa na tutakufa. Tuenende katika mapenzi ya muumba wetu, maana kwake tutarejea, duniani tunapita; kama wapendwa wetu wengi walivyopita, relax.
 
Mkuu@Mshana Jr thnx kwa hii...Nimechelewa kuiona nadhana wakati inawekwa humu ndio Joto lakuadabisha maCCM lilikuwa juu kiasi kwamba majukwaa mengine nilikuwa napita....Mkuu nimekuwa nikifatilia mada zako binafsi nimejua mengi....Inaonekana pia umefanya utafiti wa kutosha khs haya...
Plz hebu nami niite kule kwenye mada uliyosema...nikaangalie huko....
 
Sikuwepo hewani kwa siku mbili tatu ila nimerejea usijali
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mshana Jr ni eneo gani au kijiji gani hapa Tanzania wanapatikana wachawi wa kitabu, na je ni uchawi upi mkali kati ya kitabu na huo wa majini?
 
Mkuu mshana Jr ni eneo gani au kijiji gani hapa Tanzania wanapatikana wachawi wa kitabu, na je ni uchawi upi mkali kati ya kitabu na huo wa majini?

Uchawi wa majini ndio unasemekana kuwa ndio kiboko lakini hii taaluma ni pana sana na haina takwimu za moja kwa moja hivyo kuwa ngumu kwa hakika kujua
Mara nyingi maeneo ya pwani au yaliko maziwa na mito mikubwa ndio husifika sana kwa ndumba na ulozi
 
Niite na Mimi mkuu uko pengine, niongezee woga
 
Duu basi marehemu alikuwa mkorofi sana, na kwa vyovyote huyo aliyemzaba vibao ni mtu mwenye mamlaka naye
Kabla hajafariki aliagiza asisafirishwe kwenda kuzikwa kwao. Azikwe pale pale alipokuwa anafanyia kazi. Huyo aliyemchapa makofi hakumjua ila walikuwa wanafanyia kazi kada moja japo mikoa tofauti.
 
Mshana Jr unaonekana unapenda kutishia watu kwa vitu vya kawaida kabisa
 
Nauliza.je hao maiti huwa chiu au ?huwa wanawake na waume au?huwa wamekufa kweli au wamezimia wewe unawamaliza kwa teke?
 
Back
Top Bottom