Kuna watu hufa mara mbili

Kuna watu hufa mara mbili

kuna kitu kinaitwa RIGOR MOTIS...Kukakamaa kwa misuli baada ya mnyama kufa..hali hii haitokei kwa binadamu tu ata kwa wanyama wengine..ndiyo maana inashauriwa kumuweka marehemu vizuri kama kumfunga macho n.k kabla hajakakamaa au haja undergo rigor motis..unapochelewa kumuweka vizur ndiyo hizo nyundo unazoziongelea hufuata....kwa hyo siyo uchawi mzee..
Hili jambo halijulikani kwa jamii yote mkuu.
 
kuna story niliwahi kuisikia juu ya mortuary technician mmoja miaka ya zamani kidogo pale mawenzi regional hospital moshi.
alikua akiingia kwenye wodi za wagonjwa na yasemekana akimwambia mtu utanifuata basi ilikua haichukui muda mtu huyo anafariki...
je jambo hili linawezekana au ni story za kahawa?
Hizi ni stori za watu, labda alikuwa mchawi anachukua watu misukule, nje ya hapo kifo kitabaki kuwa ni siri ya Mungu.
 
Unaweza kudhani ni stori za kijiweni au kufikirika lakini haya mambo yapo na uzoefu wangu wa kuhudumia wafu ulinifanya nikutane naye.

Kuna watu hufa mara mbili na mara nyingi ikiwa ni usiku, wahudumu wa mochwari wanalifahamu hili vema! Unaletewa mwili uuhifadhi kwenye jokofu lakini kwa wakati huo majokofu aidha yamejaa au kuna miili mingi inahitaji kuipanga vema kabla hujaiload kwenye jokofu.

Miili yote inayoletwa mochwari imeshathibitishwa na daktari kwa maandishi kuwa huyu ni marehemu/maiti hana uhai tena hapumui na ni mzoga lakini ukiwa kwenye harakati za kupanga hizo maiti ghafla mojawapo ya maiti inasimama wima na kutaka kupiga hatua huku macho bila kupepesa yakiwa yamemtoka pima! !! Huna jinsi unaisindikiza na teke irudi ilipokuwa na baada ya hapo hainyanyuki tena.

Mochwari kuna mengi ya ajabu ya kutisha na kustaajabisha na wahudumu wa huko wanaona mengi! Lakini kitu kisicho na majibu ni kwamba kwanini kuna maiti hua zinafufuka na kufa tena ?

Bado kuna mengi hatuyajui.
Kaka naelekea kuacha kufuatilia post zako... sometimes naona kama kuna UONGO FULANI
 
Katika uumbaji Mwenyezi Mungu kamficha mwanadamu mambo mengi saana, laiti tungelipewa walau 2% tu ya siri za uumbaji, ingelikuwa hatari saana duniani pasingelikalika.

Hapa duniani mbali na Binadamu, Wanyama, ndege lakini kuna viumbe wengi mno tunapishana nao mabarabarani humo, majumbani tunaishi nao lakini hatuwaoni, hata hili la maiti kuibuka na kuzimika pia ni baadhi ya miujiza michache ambayo hutokea.

Sasa ukifikiria saaana unafika sehemu "beyond human thinking....... inakuwa kiza". Hii ni siri nzito ya uumbaji ambayo tumenyimwa access.
 
Aise kuna maisha megine baada ya kifo
Haya ndiyo kati ya yale ambayo tumefumbwa, tumenyimwa access, hakuna binadamu yoyote duniani anayejua kwamba je kuna maisha ama hakuna, au alikuwa wapi kabla hajazaliwa...

Kinachofanyika ni mambo ya imani tu, unaamini vitu ambayo havina prove yoyote ile...though ni vizuri ukaamini in a positive way sababu ukikuta yapo kweli uwe tayari kuyakabili.
 
Kuna jamaa aliajiriwa huko kukamshinda akakimbia! wale wahudumu wanaenda kwa wangaga ili wasivione!
Waganga ni wajanja kidogo tu, wanajaribu kusoma elimu ya siri ya uumbaji na kujaribu kuigusagusa yaani kuifanyika implementation, unapoenda kwa mganga wanachofanya wao ni kutumia nguvu zako ulizopewa wakati wa uumbaji na kuzifanya active - kifupi kila binadamu kapewa nguvu ila wachache mno wanajua kwamba wanazo za aina gani na wazitumie vipi.

Sasa ukienda kwa mganga anachofanya ni kuzitumia ili zukusaidie - ndiyo maana anakuagua upate pesa wakati yeye hata mia 200 mfukoni hana, anasubiri umpe sadaka ya kuku ama mbuzi.
 
[emoji35] [emoji34] sasa MTU kaamka alaf unampiga buti...ndio nini sasa..hamumtendei Haki.....Je kam alikua kaamuka moja kwa moja
 
mshana jr ni bora ikifufuka usiipige teke ni kuirudisha wodini na nduguze wakija watakushukuru kuwa umeifufua ukaingia katika vitabu vya Guinness
[emoji28] [emoji28] [emoji28]
Umeona Eeh....but hatendei Haki unampigaje MTU alieamka anatak kurudi
 
ha
[emoji28] [emoji28] [emoji28]
Umeona Eeh....but hatendei Haki unampigaje MTU alieamka anatak kurudi
huyo hataweza kurudi tena, kinachofanyika pale ni mauza uza tu, hata kama usipompiga teke mara nyingi hatachukua muda mrefu ataanguka tena. ile ussue ya mtu kupiga chafya mochware inawezekana ilikuwa ya kweli ila yule mlinzi nafikiri hajui hakujua siri za mochware alikuwa mgeni wa kazi ile - mambo kama hayo ni ya kawaida. akikohoa wewe mpige kofi ili alale moja kwa moja asikusumbue ili ndugu zake wakija asubuhi wakamzike.
 
Ukiona hivyo ujue alikuwa hajafa, mkamuwahisha mochwari
 
Mmmh Wauwaji Nyie.....kweli....
Anaefanya kazi Mochwari nije niokoe wafu Pliiiiz
 
Unaweza kudhani ni stori za kijiweni au kufikirika lakini haya mambo yapo na uzoefu wangu wa kuhudumia wafu ulinifanya nikutane naye.

Kuna watu hufa mara mbili na mara nyingi ikiwa ni usiku, wahudumu wa mochwari wanalifahamu hili vema! Unaletewa mwili uuhifadhi kwenye jokofu lakini kwa wakati huo majokofu aidha yamejaa au kuna miili mingi inahitaji kuipanga vema kabla hujaiload kwenye jokofu.

Miili yote inayoletwa mochwari imeshathibitishwa na daktari kwa maandishi kuwa huyu ni marehemu/maiti hana uhai tena hapumui na ni mzoga lakini ukiwa kwenye harakati za kupanga hizo maiti ghafla mojawapo ya maiti inasimama wima na kutaka kupiga hatua huku macho bila kupepesa yakiwa yamemtoka pima! !! Huna jinsi unaisindikiza na teke irudi ilipokuwa na baada ya hapo hainyanyuki tena.

Mochwari kuna mengi ya ajabu ya kutisha na kustaajabisha na wahudumu wa huko wanaona mengi! Lakini kitu kisicho na majibu ni kwamba kwanini kuna maiti hua zinafufuka na kufa tena ?

Bado kuna mengi hatuyajui.
Maiti kufufuka ni pale atakapozinduka toka MAKABULINI (jambo hili halipo)...kushituka akiwa MOCHWARI hili ni swala jingine Brother Mshana....

Sidhani kama kuna mwana JF humu amewahi kuona ama kusikia kuna Maiti amezinduka akiwa Kaburini (labda wale wa kwenye nyimbo ya Thriller)

Vinginevyo ni Maiti za Mochwari ambapo hufanyika makosa wakati mwingine kwa kuingiza wale waliozimia wakidhani ni wafu....
 
Kwahiyo kwa upande mmoja unakubaliana namimi
 
Maiti kufufuka ni pale atakapozinduka toka MAKABULINI (jambo hili halipo)...kushituka akiwa MOCHWARI hili ni swala jingine Brother Mshana....

Sidhani kama kuna mwana JF humu amewahi kuona ama kusikia kuna Maiti amezinduka akiwa Kaburini (labda wale wa kwenye nyimbo ya Thriller)

Vinginevyo ni Maiti za Mochwari ambapo hufanyika makosa wakati mwingine kwa kuingiza wale waliozimia wakidhani ni wafu....
Mmh maiti kushtuka akiwa mochwari?au ndio huko kufufuka?
 
Back
Top Bottom