Kuna watu makatili kweli kweli, achoma paka moto akiwa hai

Kuna watu makatili kweli kweli, achoma paka moto akiwa hai

Paka mda mwingine ana tabia mbovu kama hujamtrain, anaweza tu ukiwa umetenga chakula akapitisha mkia ili ukisuse, ale. Anaweza hata kunya kwenye unga wako wa ugali kana kwamba amekosa sehemu ya kumaliza haja zake. Paka ni mnyama mwenye vitimbwi vingi mno

Ila yeyote anayepambana na paka atakuwa anajiamini sana. Kwa sifa tunazosikia kitaa hafai
Nikiwa mtoto na wadogo zangu wawili wa kiume tuliyaua mno mapaka shume aka vimburu
 
Nimefuga kuku sana wa kienyeji mbegu za hapa hapa nchini, mbegu ya malawi (wale weusi tiiii) na mbegu ya Kuroiler. Kwa kweli inauma sana pale kuku anapokufa mda mwingine unakosa hadi raha. Kuna kuku kishingo kila nikiingia kwenye malazi ya kuku huwa alikuwa ananifata nyuma nyuma nikstokea kumpenda sana yule kuku. Siku mojan nimedamka mapema kwenda kulisha kuku nikakuta kuku wangu kishingo kadanja nilikosa raha siku nzima. Baba yangu mdogo mfugaji nae alikuja nisabahi home ile kunikuta na simanzi akanitusi acha ufala wewe akisema “mimi nafuga ngombe na mbuzi na wanakufa, wewe kafa kuku unatia huruma, angekufa ngombe wa million 3 si ungekufa??” hahah

Nimeandika haya nikimfikiria huyu mchaga ana roho ya namna gani kuchoma paka moto. Mie kama kuna paka anakula mifugo ningemuwekea sumu kwenye samaki. Lakini huyu jamaa ana roho ya namna gani. Mimi ni mchaga wa mkuu Rombo lakini aisee kuna wachaga wana roho ngumu sana. Nawataadharisha wale wenye wenza wa kichaga chungeni sana kuweni makini mnooo...

View attachment 2004793
Huyo jamaa haya MTU anaweza kuua sababu ya mali
 
Wako very displined wakiwa wadogo mpk umri wa kati,yule alianza tabia za ajabu alivyoanza kuzurura na mipaka ya mtaani.
Ila mwanzo alikua poa sana na nimekaa nae muda tu.
Yes nilifungua mlango atoke,,maana alipoona nampiga akawa anaruka na makucha yake ananata ukutani nikimrushia gongo pale anaruka kuniatack usoni.
Namkwepa
Nikaona tutauana humu
Nikafungua mlango.
Wale wadudu ni km chui ndugu akigeuka zile kucha zake ni ndefu sana.
Anakudhuru vizuri tu.

Paka hujiona mfalme
 
Huyo mshenzi ataandamwa na mikosi na mabalaa maisha yake yote, na wote ambao mmeshaua Paka msijishangae mambo yenu hayaendi sawa ni kile kivuli cha Paka ulichokiua kinakuwinda,

Binaadam hua tunafikiri hii Dunia ni yetu peke yetu, tunasahau kuna viumbe wengine tunachangia nao, tuache ubinafsi, tuache ukatili, Dunia ni mahala salama kama tukipaweka salama.
 
Nimefuga kuku sana wa kienyeji mbegu za hapa hapa nchini, mbegu ya malawi (wale weusi tiiii) na mbegu ya Kuroiler. Kwa kweli inauma sana pale kuku anapokufa mda mwingine unakosa hadi raha. Kuna kuku kishingo kila nikiingia kwenye malazi ya kuku huwa alikuwa ananifata nyuma nyuma nikstokea kumpenda sana yule kuku. Siku mojan nimedamka mapema kwenda kulisha kuku nikakuta kuku wangu kishingo kadanja nilikosa raha siku nzima. Baba yangu mdogo mfugaji nae alikuja nisabahi home ile kunikuta na simanzi akanitusi acha ufala wewe akisema “mimi nafuga ngombe na mbuzi na wanakufa, wewe kafa kuku unatia huruma, angekufa ngombe wa million 3 si ungekufa??” hahah

Nimeandika haya nikimfikiria huyu mchaga ana roho ya namna gani kuchoma paka moto. Mie kama kuna paka anakula mifugo ningemuwekea sumu kwenye samaki. Lakini huyu jamaa ana roho ya namna gani. Mimi ni mchaga wa mkuu Rombo lakini aisee kuna wachaga wana roho ngumu sana. Nawataadharisha wale wenye wenza wa kichaga chungeni sana kuweni makini mnooo...

View attachment 2004793
Yupo mwingine alimtwanga paka kwenye kinu hadi akawa uji[emoji1787]
 
Kwasababu hamjawahi kuwa na touch na mfugo mnaofuga ni rahisi sana kumlaumu mangi. Angalia hapo pembeni kuna kuku wake hana kifaranga hata kimoja halafu paka mwenyewe ki muonekano tu ni yale mapaka pori yasiyo na mwenyewe.
Paka anaedokoa mboga anavumilika maana ni njaa lakini paka anaegeuza banda lako la vifaranga ndio sehemu yake ya mwindo huyo hafai.
Ukute Manginkajaribu mbinu zote, kaimarisha banda lake, kamtega kwa sumu zote zimefeli mwisho kamnasa kwa mtego afanyeje? Njia rahisi ya kumuua ilikua ni hiyo ya kumpelekea moto tu au nyinyi mnadhani ndani ya hiyo cage angemuuaje?

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
Vifaranga vilirudi baada ya kumtesa vile? Angepiga rungu moja la kichwa kwisha habari
 
Paka wezi wanakera sana. Kuna jirani yetu enzi nipo shule kidato cha pili alikuwa amefuga paka wengi na wengine wakawa wezi, ukiacha mlango wazi wanaingia kudokoa chochote. Ikafikia mahali wanakaa karibu na dirishani, ukifungua tu baada ya dk 5 unakuta ameingia yupo uvunguni mara huyoo jikoni au kufungua friji ale chochote atachokikuta.

Basi kuna siku tukiwa na rafiki yangu tukamtegeshea kipande cha nyama kwenye mtego wa panya ule wa spring. Tukauweka chini kidogo ya dirisha pale wanapopenda kuingiliaga. Si tukawa chumba cha pili tunaendelea kupiga msuli, kama dk 30 mara tukasikia mtego umefyatuka na paka analia mauuuuuuuuu mauuuuuu kucheki kumbe amenaswa mguu wa mbele na mtego ameshindwa kuutoa, alivyotuona akapanic zaidi akajaribu kuruka kupita dirishani anashindwa, tukamfungulia mlango akatoka na mtego wake huku analia, nyama kaidondosha chini, tukamwacha. Akaingia kwao sijui hapakuwa na mtu maana tuliendelea kumsikia analia muda mrefu, badae akatoka tena hatukujua alipoenda, ila ulipita muda mrefu sana hatukuona paka mle ndani, na kile kipande kilibaki chini mpaka sisimizi wakakiandama tukafagia. Sema bi mkubwa hakupendezwa sana aliposikia tulichokifanya. Si unajua hofu za ushiriki na.
 
Kuna Waziri Mmoja alichomaga Vifaranga yaani ni roho mbaya ya ukatiri...
 
Sisi tuliofuga njiwa ndio tunaijua vizuri adha ya haya mapaka shume.
Likifanikiwa kuingia ndani ya banda linaweza kuua hata njiwa 10 halafu linachua mmoja linaondoka, njaa ikimshika tena anakuja kuua wengine mpaka njiwa wote wanaisha au wanahama.
Ila yote kwa yote kwa imani yangu amelaaniwa binaadamu yoyote anaetesa au kuua kwa kutumia moto, hukumu ya kuadhibu kwa moto ni ya MUNGU pekee sio binaadamu.
 
hawa wadudu hamuwajui nyinyi,usione hawaishi na msela ukadhani ni bahati mbaya.wanajua.

enzi hizo niko kijijini huko,imechinjwa kuku ikaungwa rost imeliwa robo mchana,inatakiwa iliwe na usiku na kesho yake maana tulibaki watoto 3 tu,wazazi waliondoka mchana huo kwenda seminar mjini.

huwa kuna meza kubwa sana iko nyuma ya nyumba,hiyo tunaweka vyombo na vifaa vingine vya chakula na hata mboga sometime,siku hiyo kwa kuogopa paka hatukuweka sehemu nyingine yoyote isipokuwa sufuria husika iliwekwa juu ya hiyo meza,kisha ikafunikiwa ndoo kubwa juu ya ndoo ikawekwa tofali ya block.

tukaenda kisimani kuchota maji[emoji23].
wakati tunarudi tunashangaa kwa mbaaali kuna kama kuku wanakimbizana kunyang'anyana vitu,kumbe wamegawana nyama ya kuku aliyechinjwa,kuku nao tulikuwa nao kama 130 hivi wa kienyeji,kucheki ndoo juu ya meza iko chini,tukajua hapa tayari tumeshapigwa.

kufika pale paka tuliyekuwa tunamfuga,analamba mchuzi chini na wanaye kujipongeza kwa kazi aliyoifanya huku matumbo yanakaribia kugusa chini,kwa hasira nilipiga mmoja shuti hakuinuka na roho zake 7[emoji1787].
wengine walitawanyika mbiooo.
 
Nimefuga kuku sana wa kienyeji mbegu za hapa hapa nchini, mbegu ya malawi (wale weusi tiiii) na mbegu ya Kuroiler. Kwa kweli inauma sana pale kuku anapokufa mda mwingine unakosa hadi raha. Kuna kuku kishingo kila nikiingia kwenye malazi ya kuku huwa alikuwa ananifata nyuma nyuma nikstokea kumpenda sana yule kuku. Siku mojan nimedamka mapema kwenda kulisha kuku nikakuta kuku wangu kishingo kadanja nilikosa raha siku nzima. Baba yangu mdogo mfugaji nae alikuja nisabahi home ile kunikuta na simanzi akanitusi acha ufala wewe akisema “mimi nafuga ngombe na mbuzi na wanakufa, wewe kafa kuku unatia huruma, angekufa ngombe wa million 3 si ungekufa??” hahah

Nimeandika haya nikimfikiria huyu mchaga ana roho ya namna gani kuchoma paka moto. Mie kama kuna paka anakula mifugo ningemuwekea sumu kwenye samaki. Lakini huyu jamaa ana roho ya namna gani. Mimi ni mchaga wa mkuu Rombo lakini aisee kuna wachaga wana roho ngumu sana. Nawataadharisha wale wenye wenza wa kichaga chungeni sana kuweni makini mnooo...

View attachment 2004793
kuna paka ananilia vifaranga, siku nikimdaka namchoma kama huyu jamaa
 
Back
Top Bottom