Kuna watu mnasababisha mikosi kwenye ndoa na familia

Kuna watu mnasababisha mikosi kwenye ndoa na familia

Mivyumba

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2017
Posts
275
Reaction score
533
Kuna wanaume baadhi huwa wanajiona wanaakili sana, kumbe ndiyo chanzo cha wao kuleta uharibifu kwenye familia zao. Hofu ya Mungu isipotawala ndani yako, vitu kama hivi ndiyo huwa vinafanyika! Naomba usome hiki kisa👇👇👇👇

Wamama nimekuta sms mchepuko anamtumia mume wangu nanukuu, "Baby vipi ule mpngo wa kuhamia kwenye nyumba yetu vipi? ,tuhamie bwana mimi hera ya kuamia nitatoa afu kule kibambq panafaa kufuga mifuko itabidi tutengeneze na mabanda", imeishia hapo.

Na mimi na mume wangu tuna wiki moja tumehamia kwetu na ni huko Kibamba, kiwanja kila kitu kina jina lake na langu. nilichofanya nikaingia Mpesa nikaangalia jina lake nikamsearch huku fb, nikaona kapost picha ya nyumba yetu kaandika:

"Mama mjengo, asante Mungu kumaliza nyumba yangu😭😭."

Mpaka sasa nimeganda kama barafu sijaongea chochote na wala mume wangu hajui.

Nimuulize au niwaachie wenyewe mambo yao?
 
Duh! Mwandiko ni tatizo.

On a serious note, ye si majina yake yapo kwenye hati na kila kitu? Amcheki tu mchepuko aje ashangae maajabu.

In short jamaa anakula kimasihara kwa kumdanganya mchepuko kua anahamia nae kwenye nyumba while in real sense n kwa mkewe.
 
Kuna Wanaume baadhi huwa wanajiona Wana akili sanaa,kumbe ndo chanzo cha wao kuleta Uharibifu kwenye Familia zao. Hofu ya Mungu isipotawala Ndani yako...
Hifadhi ushaidi wa picha za hizo sms mapem .... kesi bila ushaidi hainogi
 
Mama mjengo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kama dini inaruhusu, mke wa pili huyo jiandae
 
Hamna kesi hapo.... Meseji za kubumba kufurahisha genge siku zipite
 
Yanafurahisha 😃😃, pole ila mbona we ndio ma mjengo....

Nikajua nashangaa peke yangu, mume Bado Yuko nae, hati Ina jina lake na mumewe, wameshahamia mjengoni, yeye wasiwasi wa nini?

Ila mkiambiwa maradhi ya akili yanalitafuna taifa na jamii Kwa ujumla mjue Hali ni mbaya.

Sasa hapo Kwa mfano Demi alipita FB akaona hiyo post si anajiona kama kenge tu kwamba yeye si chochote na si lolote mbele ya Mama mjengo, kumbe mazingaombwe matupu! Haya mambo ya mitandaoni unaweza vunja ndoa au kuuharibu mahusiano Kwa vituvya kijinga sana.

Umeshapata mtu wa kukuunga FM?
 
Bado sijapata naomba uniunge.....

Hamna ukiachana na ukweli kwamba huyo mchepuko hana cha kufanya ila kuna vitu tu kiubinadamu vinakera.
Ila sie wanaume, kama wapo watakaofika mbinguni itabidi wapewe tuzo maalum.

Subiria kwanza wakamilishe mchakato wa kuwapokea wanawake.

Alafu kama tuna unfinished business...ule mpango uliishia wapi tena?
 
Yaani mwanamke nyumba umeshaamua.

Hati Ina jina lako.

Unataka Nini kingine?

Kuna wakati inabidi umdanganye mtu ndio umkule.

Usianzishe mgogoro mkaishia kugawana vijiko.
 
Back
Top Bottom