Kuna watu na PhD zao wapo nyumbani hawana kazi, Rais Samia tafadhali saidia

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Wapo wasomi wakubwa wamepata PhD kutoka vyuo vyenye sifa kubwa duniani lakini wasomi hawa wapo nyumbani hawana kazi.

Sipendi kuamini kuwa hatuwahitaji watu hawa nchini. Tumewasomesha kwa gharama kubwa na sasa tuwatumie kwa faida ya taifa letu.

Ninashauri rais wetu mama Samia kuwe na kanzi data (data base) yenye majina na wasifu wa wasomi hawa ili waweze kupewa nafasi za ajira na teuzi mbalimbali kwa manufaa ya nchi yetu.
 
Inamaana wameshindwa kutumia gunduzi zao kujipatia pesa?
 
Wapo wasomi wakubwa wamepata PhD kutoka vyuo vyenye sifa kubwa duniani lakini wasomi hawa wapo nyumbani hawana kazi.

Sipendi kuamini kuwa hatuwahitaji watu hawa nchini. Tumewasomesha kwa gharama kubwa na sasa tuwatumie kwa faida ya taifa letu.

Ninashauri rais wetu mama Samia kuwe na kanzi data (data base) yenye majina na wasifu wa wasomi hawa ili waweze kupewa nafasi za ajira na teuzi mbalimbali kwa manufaa ya nchi yetu.
Hizo PhD haziwezi kuwa na manufaa kwa wao binafsi,familia zao,Koo zao pamoja na jamii zao mpaka waajiriwe au wapate teuzi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mazingira ya kujiajiri ni magumu. Pia unakuta mtu ana PhD ya utafiti wa mbu atajiajiri vipi? Sio rahisi kihivyo.

Faida za kuwa msomi ni pamoja na kuiona kesho yako na kusoma kitu chenye kuwanufaisha watu moja kwa moja , Sasa unajijua upo Katika Nchi masikini then unasoma Mambo magumu ili iweje?
 
Umeuliza tu swali la kibabe ila unajua hata waalimu na madaktari wanachangamoto ya ajira kwani walisomea mambo magumu?
 
Wapo wasomi wakubwa wamepata PhD kutoka vyuo vyenye sifa kubwa duniani lakini wasomi hawa wapo nyumbani hawana kazi.

Sipendi kuamini kuwa hatuwahitaji watu hawa nchini. Tumewasomesha kwa gharama kubwa na sasa tuwatumie kwa faida ya taifa letu.

Ninashauri rais wetu mama Samia kuwe na kanzi data (data base) yenye majina na wasifu wa wasomi hawa ili waweze kupewa nafasi za ajira na teuzi mbalimbali kwa manufaa ya nchi yetu.
Hiv we unajua maana ya PhD kweli? Au we ndio unayo? ni ya nini hiyo ambayo haiajiriki.
 
Umeuliza tu swali la kibabe ila unajua hata waalimu na madaktari wanachangamoto ya ajira kwani walisomea mambo magumu?
Kama wewe ni daktari wa Binadamu huwezi kuwa umedufua Hadi PhD ukaanza kunyatia Ajira uchwara za serikalini

As the same mwalimu ukiwa na PhD huwezi kukosa Sehemu ya ku-offer MAARIFA yako .

Sasa mpaka unatoboa masters to PhD hivi kweli unakuwa hauoni Hali halisi ya Nchi yako inahitaji kwa wakati ujao Hadi usomee Maswala ya Mbu.
 
Waombe Tamisemi na Ajira portal waje kwenye fair ground wapambanie Asali

Kama upo smart sio lazima kuwa serikalini

Pia Nchi yetu haitaji PhD Maana Hadi Muda sijaona imuhimu wa PhD za bongo.
Hujaona umuhimu kwasababu huna. wanatafutwa watu wa masters hawapatikani vyuo vinarudia matangazo mara mbilli mbili mtu anatokea kuna PhD ziko mtaani. Nyie ni mapoyoyo tu hakuna mnalojua.
 
Back
Top Bottom