kuna watu wana tabia zinakera bila wao kuzijua, ukiwapa ushauri wanakuona umewadhihaki, njia zipi za kidiplomasia zinafaa kuwaokoa bila kuzaa uadui ?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
sizungumzii wale waliokaza mafuvu wanafanya tabia kwa kujielewa na walishakataa ushauri, hapa ni wale ambao tabia wanazofanya zinakera wengine ila hawana hatia kamili kwenye tabia zao aidha wao hawajui kwamba wanachofanya ni tabia mbaya, wameishi na watu au sehem flan kwa mda mrefu iliyowafanya wazoee tabia flani,n.k hawa bado wana nafasi ya kuokolewa na wanahitaji msaada.

- anaringa ila yeye hajui kwamba anachofanya kwenye jamii ni maringo, huenda kwao alikuwa getikali inakua ngumu kujichanganya.

-mtu ananuka ila hajijui, anaona ni kawaida, yeye hasikii harufu, n.k.

-mtu ni mmbeya a.k.a kisimpite, huenda kakaa sana na mashangazi wenye hizi tabia kwake kawaida

-mtu ana masifa ila yeye anaona kawaida, yawezekana huko alikoishi kwa muda mrefu ndivyo wanavyoishi.

-mtu anaongea matusi kwake kawaida, yawezekana kakaa muda mrefu na watu wanaoongea hivi, yeye kwake haoni tatizo

ukimwambia ukweli anaanza visingizio unrelated kwamba mti wenye matunda hupigwa mawe, tafuta pesa, n.k.

ni mbinu zipi za kidiplomasia unamjulisha mtu juu ya tatizo alilonalo na wala halipi uzito ?
 
Mbinu yangu naaita kimemo

huwa naenda stationery naprint jumbe kwenye karatasi naweka kwenye bahasha, hio bahasha naandika jina lake naiweka sehemu ambayo ataikuta.....kero ya tabia zake kwakuwa inatuathiri wengi hawezi jua ni nani kamuandikia...na kiukweli huwa nampa makavu machungu sana bila huruma lakini nakazia faida za yeye kubadilika
 
mkuu mtu akiringa wee inakuhusu nini? labda Kama anakutukana lakini Kama hakudhuru kwa chochote muache mkuu Wala usijihangaishe kumtaftia mbinu dili na Mambo yako
 
kuna waaoringa maksudi hao wala hatuna shida nao, wenye shida ni wale hawajui kwamba wanachofanya ni kuringa,
 
Mmoja alikuwa rafiki yangu kumbe alikuwa ananisnitch kwa Boss ...nimempiga chini kimyakimya Hadi amejuta...

Yaani unamshauri kuhusu maisha yake nacwanawe then anakuona adui...Mpige BAN ya kimyakimya tu...
 
Mkuu haina haja ya kujitoa kiasi hicho maana utaonekana una nongwa
 
sizungumzii wale waliokaza mafuvu wanafanya tabia kwa kujielewa na walishakataa ushauri, hapa ni wale ambao tabia wanazofanya zinakera wengine ila hawana hatia kamili kwenye tabia zao aidha wao hawajui kwamba wanachofanya ni tabia mbaya, wameishi na watu au sehem flan kwa mda mrefu iliyowafanya wazoee tabia flani,n.k hawa bado wana nafasi ya kuokolewa na wanahitaji msaada.

- anaringa ila yeye hajui kwamba anachofanya kwenye jamii ni maringo, huenda kwao alikuwa getikali inakua ngumu kujichanganya.

-mtu ananuka ila hajijui, anaona ni kawaida, yeye hasikii harufu, n.k.

-mtu ni mmbeya a.k.a kisimpite, huenda kakaa sana na mashangazi wenye hizi tabia kwake kawaida

-mtu ana masifa ila yeye anaona kawaida, yawezekana huko alikoishi kwa muda mrefu ndivyo wanavyoishi.

-mtu anaongea matusi kwake kawaida, yawezekana kakaa muda mrefu na watu wanaoongea hivi, yeye kwake haoni tatizo

ukimwambia ukweli anaanza visingizio unrelated kwamba mti wenye matunda hupigwa mawe, tafuta pesa, n.k.

ni mbinu zipi za kidiplomasia unamjulisha mtu juu ya tatizo alilonalo na wala halipi uzito ?
Ni kweli hizi tabia zinaudhi ila ndugu nikukumbushe kuwa wahenga walishasema samaki mkunje angali mbichi ila akishakauka utamvunja.

Ni ngumu sana kumbadili mtu mzima labda iwe kaamua kubadilika kutokana na mazingira yanayomzunguka.

Hivyo naamini ulimwengu ni darasa hivyo mda mwingine tafuta namna ya kuishi na mtu mwenye sifa hizo as long as haupungukiwi na kitu ila kusema sijui umwambie sijui umshauri ni kutengeneza magomvi yasiyo na tija .

Kaa pembeni tafuta njia bora ya kuishi na mwenye tabia mbaya then ishi naye
Ulimwengu ni mwalimu ikiwa ukiamua kumfundisha atabadilika.
 
Back
Top Bottom