Kuna watu wanauawa bila Hatia kwa tuhuma za wizi, watanzania tuache kukurupuka

Cleverking hebu pitia shuhuda za hawa wachache zinazoashiria ukubwa wa tatizo hili la kufanya maamuzi pasipo kujiridhisha kama ni ya kweli.
T
 
Huyo uliyemuokoa...Mungu alikuwa hajapenda afe....ila alijarbu kutoa somo tu kwa watu kupitia wewe mana inaonekana watu Wa huko wamekaa kama killers...vinginevyo mbinu uliyotumia si chochote kwa umati wenye hasira...na istoshe hata wewe wange kuunganisha
 
Ni kweli usemacho kuwa siku za mtu hupangwa na Muumba, kwani ni ngumu kumwokoa mtu kwa watu wenye hasira kali,
Pia ujue ikiwa wangekuwa na uhakika wa alichoiba ingekuwa ni vigumu kumtetea, lakini kwasababu nao hawakuwa na uhakika na walitendalo nafsi ziliwasuta kuendelea kumwadhibu.
Nami niliambulia kashfa na matusi ya reja reja kabla hawajaamua kumuachia
 
Jamaa mmoja nilisoma nae baadae akawa mwalimu aliuwawa palle vingunguti miaka kadhaa imepita sasa kwa kudhaniwa mwizi alipokuwa anatoka kula kwa mama ntilie.Alikula akalipa akaondoka, sekunde chache baadae mama ntilie akagundua simu yake haionekani hivyo hakujiuliza akaitia mwizi.
Watu wakamvaa jamaa yangu wakapiga vibaya akafia hospitalini siku iliyofuata.Alikufa siku ambayo mke wake amejifungua mtoto wao asubuhi. Uzuri jamaa aliondoka akiwa ameshaambiwa ana mtoto.
Miaka takribani 8 sasa sijawahi sahau tukio hili.

Yule mama ntilie baadae alikuja kugundua kuwa simu yake ilidondoka chini ya meza ya kulia msosi na si kwamba jamaa alikuwa kachomoka nayo.Anaishi na donge hilo moyoni mpaka leo.
 
Sio kidogo
HII KITU INAITWA "MOB JUSTICE" NA MARA NYINGI MTU ANAYEULIWA UKIAMBIWA KAIBA NINI AU MALI YA THAMANI GANI UTABAKI KUSHANGAAA......UTAKUTA KUKU AU SIMU ETC....NI BORA HASIRA HIZO HAO WANAOJIFANYA KUCHUKUA SHERIA MKONONI WAKAZIAMISHIAA KWA WEZI WA MALI ZA UMMA NA MAFISADI...

OVA
 
Dah very painful,
Nimeifeel
Nikasikia kama moyo umemwagiwa maji yan
 
Hongera Kaka Kwa kuingilia kati swala hili,
Nakumbuka nilitaka kuuwawa mwaka 1998 pale muhimbili hospitali baada ya kuingilia kati kumuokoa kijana ambaye aliiba viatu msikiti wa muhimbili, pair moja ya Viatu ilitaka kutoa uhai wa kijana huyo na wangu ,kwani nilishaona jicho kijana limemtoka na ameshapoteza ufahamu wa kuwepo duniani watu walitupa matofali ,mawe na yalitupata wote lkn nilichofanya ni kumvuta kijana hadi getini kwenye polisi muhimbili na kufika hapo polisi waliingilia kutoa msaada.mimi nilikuwa hoi na nundu usoni lkn kwa uwezo wa mungu wote tulisalimika. Jamii inatakiwa iwe nasubira ktk kuushirikisha ubongo hasa kwenye matukio ambayo hayahatarishi maisha ya mtu,mfano hata kama mtu ni mwizi na hahatarishi uhai wako au wa mtu mwengine kwanini tatizo listatuliwe kwa kufuata sheria na kuepuka kujichukulia maamuzi ya kutoa roho ya mtu mwengine hata kama ni mwizi.
 
Wakati tunafanya utafiti mwizi yupo tu amesimama anasubiria utafiti uishe???
NDIO MAANA HAKUIBA
alisubiri ukweli kwa aliyemuibia
mm namshukuru sana aliyemuokoa
QUIGLEY
mdogo wangu alishawahi kuitiwa mwizi na mwanamke tu hawakuelewana na akashtukia kundi kubwa likimfukuza akajichomeka nyumba ya watu na walipoulizwa kaiba nini wakasema kamuibia mwanamke . Mwanamke kuulizwa kakanusha wakatawanyika
 
Ni Mwanza Hostel za St.August.
 
Hii ni mbaya sana mkuu, hatufikiri, kama tunachukia wizi tungeandamana kushinikiza wizi wa mabilioni tunayoibiwa na watawala ili wachukuliwe hatua.
 
Akili za watz sijui zikoje jmn
 
Uko sahihi sana kiongozi
 
Kinacho sumbua taifa letu hili ni, kukulupuka, siasa za kukulupuka, elimu kukulupukia, kua nako ni kukulupuka, kila kitu kukulupuka, kuchangia mawazo kukulupuka, kilimo kululupuka, muziki kukulupuka, yaani kila kitu ona sasa tutauana tutakwisha bila sababu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…