Kuna wengine hatujui tulipokosea

Kuna wengine hatujui tulipokosea

Ep 17

Mapicha picha yameanza nyumbani. Ukienda kama baba hayupo kulala njaa ni kawaida tena mama yetu wa kamboa haoni aibu kukwambia kuwa kuwa leo hatujapika mwanangu huku hakijichekesha hivyo sisi na wadogo zako tumeshakula vitumbua, au maandazi hivyo wewe nawe fanya mpango wako wa kula sisi tumeshashiba. Yaani nyumbani pamebadilika sio mimi sio Joy anayeenda pale asikumbuke uwepo wa Auntie.

Kuna siku nimeenda mororogoro tulikuwa na safari yetu mimi Dav tulikuwa tunaenda Arusha Vacation nikaamua kupitia nyumbani kuwa salimia siku moja kabla ya safari. Chumba changu kimejaa vitu vya auntie, kuanzia nguo zake na makabati yake huwezi kulala mule kwa ufupi kimegeuka stoo ya vitu vya auntie.

Joy mazoea hataki kabisa chumba chake kimefungwa na funguo anazo mwenyewe. Chumba cha wageni kuna ndugu yetu mtoto wa shangazi amefikia pale kutoka kanda ya ziwa kufanya shughuli zake na kuondoka.

Nikaamua kulala chumbani kwa wadogo zangu. Morogoro hali ya hewa ni baridi kidogo tofauti na hali ya hewa ya Dar. Nikachukua gauni langu nimelala nimelivaa. Alfajiri kama saa kumi nastuka usingizini nakuta wenzangu wamelala chini. Nashangaa nimelowa mwili mzima. Mdogo wangu akaniuliza dada umelowa? Nikamwitikia ndio akaguna kwanza pia akasema pole sana dada angu nitafanyaje sasa.

Sikumtilia maanani sana nikahisi labda mdogo wake atakuwa anakojoa kitandani japo ni bint mkubwa tu darasa la sita. nikaamka nikajiandaa na kubeba mizigo yangu na kwenda zangu kwa Dav kwa ajili ya safari. Nguo zangu zilizolowa nikaziweka kwenye mfuko. Nimefika kwa Dav tunaenda kwa mama kwanza kumsalimia safari yetu ni kesho yake. Jioni tumerudi kutoka kwa mama yake Dav ndo nakumbuka nguo nilizoziweka kwenye mfuko. Nikazifuata kwa lengo la kuzifua nikihisi ni mikojo tu lakini ajabu ngu hazinuki hata mkojo na yule bint ana miaka kama 14 mpaka 15 hivi na mkojo wa mtu mzima unavyonuka. Ndio nikagundua kuwa watakuwa walinimwagia maji.

Siku zimeenda namuona mdogo wetu ambaye ni mtoto wa baba na mdogo wake ambaye ni mtoto wa mama yake aliyemza huko kwingine Watoto wameanza dharau siwaelewi. Pale lazima niende kwa sababu ni kwa baba yetu. Joy akienda lazima atatoka kule wamegombana hatuna ukaribu sana na Joy lakini changamoto tunazokutana nazo kwa baba tunaambiana.

Joy ni mkorofi sana hivyo ukitokea umemchokoza unakuwa umewasha moto. Kuna kipindi cha likizo Joy alienda kukaa kule kwa ajili ya likizo yake. Yaani kulikuwa pa moto sana. Ilifika hatua Joy akawa anapika chakula chake na wao wanapika chukula chao. Yaani ni fujo tu. Kuna siku baba alinipigia simu kuhusu Joy anavyokuwa hana adabu na ametaka kuwakalisha kikao Joy kakataa kasema mpaka mama yake au antie mmojawapo awe kwenye hicho kikao ndio atakubali kukaa kikao. Na anajua kuwa haiwezekani ili mradi tu fujo.

Mama mdogo (mama wa kambo) ananigombanisha na baba yangu

Siku zimeenda sana nimemkumbuka baba yangu naamua kumpigia simu. Nilipiga sana simu inaita tu haipokelewei, nikawa na wasiwasi juu yake. Nilikaa muda kidogo nikaamua kupiga tena.

Simu ilipokelewa na mama yetu wa kufikia. Hakunisalimia anaongea kwa jeuri unapiga simu sana wewe na ukiona simu yako haipokelewei jua mwenye simu hayupo. Hiyo kauli ilinikera nilikuwa sijawahi kumjibu ila siku hiyo nilimjibu na mimi nilikuwa sikupigii wewe nilikuwa nampigia baba yangu. Akanambia huyo ni mume wangu

Namimi ni baba yetu tena mama yetu ulimkuta na alikuwa amefunga ndoa na baba yangu tena ya kanisani si kama yakwako ya bomani na umetukuta hivyo tuheshimu ili na sisi tukuheshimu. Pia usisahau mama yetu alichumbiwa na kutolewa mahali.

Sikutaka kusikia neno lingine kutoka kwake.

Kumbe nilipokata simu akaanza kujiliza na kuanza kusema kuwa nimemtukana nasikia baba alivyorudi alimwambia kuwa nimemtukana na kumuita baa med kuwa yeye na baba wote ni wahuni tu kwani walikutana bar na maneno mengine mengi. Hayo aliniadithia Joy sababu kipindi hicho alikuwa Morogoro akiwachachafya na fujo zake.

Nimekaa kama wiki moja tena nikampigia baba yangu simu lakini akawa hapokei namtumia ujumbe hajibu. Nikaamua kuwapigia ndugu zake na kuuliza kama kuna tatizo wakanambia kuwa baba aliwapigia na kuwaeleza kuwa nilimtukana hivyo hanitambui tena kama mtoto wake.

Nilivyoambiwa vile nikamtumia baba ujumbe na kumwambia. Asante baba unawaambia watu kuwa nimekutakana wewe na mke wako na kuwa hunitambu kama mtoto wako nashukuru ila ungejiuliza swali moja huyo mkeo angekuwa mama yetu na kweli nimekutukana angekwambia navyojua angekuwa amekutukana mwanae kama mnavyodai asingekwambia angemkalisha chini mwanae na kumkanya ila kwakuwa mimi sio wa kwake lazima atafanya anavyoona ni sawa kwake. Nakushukuru sana baba ila mimi nishazoea kuishi bila wazazi tangu nipo mdogo hivyo sioni ajabu kwangu.

Baba hakunijibu. Tulikaa karibia miezi sita pasipo kuwasiliana na baba nikaamua kuishi ulimwengu wangu kama alivyosema Joy. Nikienda Morogoro naishia kwa Dav labda na kwa mama yake Dav na kurudi zangu Dar. Baba alikuja kunitafuta kunipa taarifa kuwa yeye na mke wake wamepata mtoto mwingine wa kike. Ndio ukawa mwanzo mpya wa mimi kuwasiliana na baba. Ila sasa mimi ndio mtoto kipenzi cha baba hakifanyiki chochote bila kunishirikisha. Haijalishi nimepitia nini bado nampenda sana baba yangu.

Nawatakia weekend njema. Niko na mafua yananitesa kweli naona yananiletea homa. Nikipata nafuu nitarudi kuendelea. Asanteni!
 
Pole
 
Pole sana dada kidot. Haujapata nafuu jamani tupate episode ingine😋
 
Kwa Dav apo umeondoa mambo mengi sana...kula Tunda kimasihara umechana page
 
Nisameheni mafua yamenitesa sana.

Ep 18

Penzi letu na Dav linaendelea vizuri, tumeamua kutambulishana rasmi kwenye familia zote mbili. Wazazi hasa upande wa Dav wanasisitiza tuoane haraka iwezekanavyo lakini mimi na Dav tunakataa kwa sababu Dav alikuwa anaishi kwenye nyumba ya kupanga bado lakini anaendelea na ujenzi hivyo tunasubiri akimaliza kujenga tu. Tunafunga ndoa na kuhamia kabisa kwenye nyumba yake. Wazazi wanakubali pendekezo letu lakini wananitolea barua ya posa hivyo uchumba wetu hupo rasmi kabisa.

Nikiwa kwa dav kama kufua tutafua wote, jikoni tunapika wote, usafi tunafanya wote yaani kila kitu tupo pamoja, kuchokozana kwa hapa na pale. Yaani ilikuwa ni furaha tupu. Hakuna aliye na mashaka juu ya mwenzake. Mimi na Dav ni wambea jamani asikujue mtu umekwisha tukiwaga wenyewe hatuna kazi tutakusengenya wewe. Dav atanipa umbea wa kazini kwake na mimi nitampa umbea wa mashoga zangu hata ambao hawajui.

Siku zimekuwa nyingi tupo kwenye mahusiano na Dav sasa ndo nimeanza kumjua Dav upande wake wa pili wa shilingi hafai hata kurumangia. Naanza kupigwa mapigo.

Pigo la kwanza (la kawaida tu)

Tumemisiana na Dav amenitumia nauli, siku za wiikend kama kawaida yangu ijumaa jioni nipo kwenye Abood naenda zangu Morogoro. Nimeenda moja kwa moja mpaka kwa Dav sikusubiri aje kunipokea msamvu kama ya Dav kuja kunichukua. Nimeenda moja kwa moja mpaka kwake. Kaninulia chakula nipo zangu sebuleni nakula akaniaga anaenda kuoga bafuni. Dav alikaa bafuni zaidi ya lisaa lizima mimi nasikia maji yanamwagika tu lakini mtu hatoki bafuni. Nikawaza huyu anaoga nini muda mrefu na mbona si kawaida yake ya kukaa sana bafuni? Nikawaza au ameshaanza michezo ya kujichua huyu nimeenda mlangoni kumsikiliza au amepatwa na tatizo namgongea aisee Dav alistuka. Ohho mama D nisamehe nakuja nakuja nimekaa sana. (tunaitana baba D na mama D sababu mama Dav ana jina linaanza na D, hivyo alikuwa anatuambia kuwa tukioana tukapata mtoto kama atakuwa wa kike tutampa jina lake) Akili yangu ikanituma huyu ameanza michezo ya kujichua.

Simfatilii sana anatoka bafuni na mimi naingia kuoga. Nipo bafuni nikaona simu yake ameisahau bafuni nikaichukua haina password ni akili moja kwa moja ikanituma inbox, kumbe jamaa alikuwa anachati na mwanamke mwingine ndo maana amechelewa kutoka bafuni. Dav anamwambia huyo mwanamke kuwa mke wake yupo hivyo anamuomba asiwe msumbufu watawasiliana kesho.

Yule mwanamke naye hakubali anasisitiza kuja kwani kama Dav alikuwa anajua ana mwanamke alimtongoza wa nini. Nakwambia Dav nitakuja huko ili huyo unayemwita mke wako ajue ameolewa na mwanaume wa aina gani. Basi Dav anambembeleza huyo mwanamke asije. Mwisho wa siku wanaelewana Dav anaambia atume hela kwa huyo dada ili asije mimi sikufuatilia sana kujua kama amemtumia au Hapana.

Nilivyomaliza kuoga zangu nikachukua simu yake na kumpa. Baba D umesahau simu yako. Alihamaki sana nilimuona ni mtu aliyekosa utulivu sikutaka ajue kama nimesoma jumbe zake. Nikajifanya kuwa hamna kilichotokea. Sisi wanawake baaadhi yetu tukiwa kwenye mahusiano huwa tunaamini kuwa hatupo peke yetu ila tunapenda kuheshimiwa. Halikuninyima amani sana sana. Sababu niliona ameniheshimu japo niliumia kusalitiwa lakini sikutaka mwenzangu ajue kama kuna ninachokijua. Wala sikutaka kumfuatilia huyo mwanamke yaani kwa ujumla niliacha kila kitu bafuni sikutaka kujipa presha ya moyo.

Pigo la pili

Nagundua Dav anatembea na mdogo wangu tunayekutana kwa baba. Siku moja mdogo wangu amekuja Dar kunitembelea. Na ilikuwa kawaida wao kuja Dar na mdogo wake wanafikia kwangu wanakaa hata wiki. Mdogo wangu tunayekutana kwa baba ameshamaliza kidato cha nne hakufauulu. Kwa ujumla hata mtihani hakufanya sababu hata matokeo yake hayakutoka. Mdogo wangu ni mzuri wa sura mpaka umbo. Baba yetu anazaa Watoto wazuri kimwonekano. Ila ni muhuni Morogoro mjini nahisi hakuna asiyemjua. Yaani ni mdangaji maarufu.

Mara nyingi akija Dar anakuwa amekuja kwenye mambo yake au kwa mabwana zake. Yaani mabwana zake sio bwana yake. Kwani hana mmoja. Kwahiyo kwangu anapanya kama sehemu ya kufikia ili kufanya mambo yake. Siku moja mdogo wangu ameweka simu yake chaji ameenda sokon. Anapenada sana kupika na anajua. Sijui kitugani kilinituma niangalie kwenye simu yake watsup. Najuta nilichokiona.

Anachati na Dav. Dav anamsifia alivyomtundu kuliko dada yake na mombo mengine mengi yaani ni uchafu tupu na anamsisitiza ajitahidi kuficha ili mimi nisijue. Anamwambia kuwa atanioa mimi ila siku za mbele atamwomba mdogo wangu amzalie mtoto na anamhaidi kumfungulia biashara akishamzalia mtoto. Niliumia sana. Niliscreen shot zile msg na na kumtumia Dav. Mdogo wangu alivyokuja sikumuuliza chochote nilijikaza kuwa kimya. Huku nikiugulia maumivu.

Mdogo wangu alipika lakini mimi sikula chakula chake yaani natamani sijui nimfanye nikampigia shoga yangu Jack na kumwambia kila kitu Jack ananishauri niende kwake ili nisijekufanya kitu kitakachonigharimu baadae. Namuaga dogo na kuondoka zangu naona nilivyoondoka Dav aliwasiliana na dogo na kumwambia kila kitu. Dogo aliondoka bila hata ya kuaga. Na sikumuuliza chochote mpaka leo.

Namwambia Dav bora tuachane ili awe huru na dogo. Dav anajitetea sana mpaka mama yake anaingilia kati. Lakini sababu nampenda Dav namsamehe kwa sharti la kusitisha mahusiano na mawasiliano mara moja na dogo. Penzi letu limerudi kama zamani.

ila nipo vibaya yaani nateseka na mafua na kifua.
 
Back
Top Bottom