Kuna yeyote aliyeoa single mother na wakafanikiwa kuishi vizuri tu kwenye ndoa?

Dah kwahiyo mkuu, single mother hawana haki ya kuolewa? Kipi ni Bora kumchukia single mother na kuona hafai au kumuweka ndani Binti aliyetoa mimba kadhaa, aliekua anatumia P2 n.k?
Bikra wapo kibao. Shida yenu vijana hamtaki kushirikisha wazee pindi mnapotafuta life partner eti ni mambo ya kizamani. Mwisho wa siku unaenda kuangukia kwa makahaba wastaafu na kuwafanya mke.
Ukitaka kuoa usitumie akili yako, washirikishe wazoefu yaani wazee. Hao hawatataka uharibikiwe japo pia mapungufu hayakosi.

Shida mnaona wazee hawatawatafutia wanawake kama wale mnaowaona insta na fb. Since they don't regard Tako na Sura nzuri as main point of a Good wife-y
 
Mkuu kwan bado uko hapo 🤔? ,Nlitegemea sahv uko mbali sana,

Mtego huo kaka
 
Sio kweli davinc, hasa kwa wazazi hawa wa mjini ambao wengi wao wanapenda sifa waonekanaje kwa marafiki zao, mfano mzuri ni Mimi, Mother alinitafutia mchumba ambae yeye kwa maono yake anafaa kuolewa, tena kwa sababu anamuona kanisani jinsi anavyojitoa n.k Binti ni mzuri, Mimi kwenye maongezi na huyo binti nikaona hapa hakuna kitu, Binti mjuaji then washikaji wakanambia jinsi ambavyo hajatulia nikapiga chini, basi nikatafuta mchumba mwenyewe kutoka kigoma huko Tena alikua bikra maana Binti kwenye harakati za kunihakikishia hajapigwa ikabidi iwe hivyo, japo sikuitoa nilipompeleka nyumbani wazazi wakamkataa kisa muonekano wake sio mzuri/elimu n.k unaelewa? Kwahiyo kwa wazazi wa sasa sio wazazi woote wanafaa kua washauri kwenye upande huo, ndio maana sasahivi nafanya mambo yangu bila kuwashirikisha kwa lolote.
 
Nina jamaa huwa ninamuita Uncle.
Huu mwaka wa tisa Tangu amuoe huyo mwanamke.

Mwanamke ndoa ya kwanza aliolewa na jamaa manager wa kiwanda cha mabati baada ya ndoa kufa, yule mwanamke akumaliza miaka miwili akaolewa na jamaa ni accountant wa kiwanda kikubwa tu.

Huu mwaka wa tisa ninawafahamu wanaenda mpaka kufanana.

Ndoa inahitaji utayari na roho ngumu sikuhizi tuna watoto wa kiume ila wanaume ni wachache.
 
Jamaa anataka muhuri tu wa MMU lakini kila kitu kashamaliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…