Akichangia katika mjadala wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na uwekezaji, Mbunge wa jimbo la Mlinga, Godwin Kunambi amependekeza Wakurugenzi wa halmashauri wasiwe wanasiasa, wapatikane kwa mchakato wa ajira.
Kunambi, ambaye pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, amesema “nchi iliyobaki inateua wakurugenzi (local government directors) ni Tanzania peke yake”
Amesema katika nchi nyingine kama vile Afrika Kusini, ni lazima watu wa cheo hicho wanapitia mchakato wa ajira.
Nchini Tanzania, kwa mujibu wa sheria, Wakurugenzi wa halmashauri za mamlaka ya serikali za mitaa wanateuliwa na Rais.
Kunambi amesema kama taifa Watanzania inabili wabadidi fikra.