Kunambi: Wakurugenzi wa Halmashauri wasiwe Wanasiasa, wapatikane kwa mchakato wa ajira

Kunambi: Wakurugenzi wa Halmashauri wasiwe Wanasiasa, wapatikane kwa mchakato wa ajira

Akichangia katika mjadala wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na uwekezaji, Mbunge wa jimbo la Mlinga, Godwin Kunambi amependekeza Wakurugenzi wa halmashauri wasiwe wanasiasa, wapatikane kwa mchakato wa ajira.

Kunambi, ambaye pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, amesema “nchi iliyobaki inateua wakurugenzi (local government directors) ni Tanzania peke yake”

Amesema katika nchi nyingine kama vile Afrika Kusini, ni lazima watu wa cheo hicho wanapitia mchakato wa ajira.

Nchini Tanzania, kwa mujibu wa sheria, Wakurugenzi wa halmashauri za mamlaka ya serikali za mitaa wanateuliwa na Rais.

Kunambi amesema kama taifa Watanzania inabili wabadidi fikra.


NIONGEZE NA YANGU
WAKUU WA WILAYA NA MIKOA WASIWE WANA SIASA NA WASIWE NA VYAMA

AMA LAH

KUWE NA EQUALITY KATIKA TEUZI KUWE NA BALANSI SIO NCHI NZIMA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA WANAKUWA WATU WA SISIEMU TU
 
Muulize kwanza Kunambi mbunge wa Mlimba ni wapi na lini alifanya interview wakati Magufuli anampa u-DED wa Dodoma Jiji mwaka 2016.

Siyo busara kuongea kwa vile hauko kwenye system. Hata Luhaga Mpina alipokuwa yuko kwenye system alikuwa anachoma nyavu za watu wakati Magu anaua akina Ben Saanane. Sasa hivi anataka iundwe Tume ya kuchunguza kifo cha Magufuli.
Ni ujuha kutozungumzia ukweli na uhalisia kisa tu uliwahi kuwa mnufaika wa jambo linlotakiwa kubadilishwa.

Kongole kwake Kunambi kwa kuliona na kulisema hili la "vilaza" wanaoitwa DEDs.
 
CCM hawawezi kukubali. Kuwa na vyeo vingi vya kuteuliwa maana yake makada wanakuwa na pa kuwekwa. Makada wakiachwa wazagae kitaa ni tatizo.

Wananchi wanapaswa kuanza kujitambua wasioelekeshwe na chama chochote cha kisiasa.
Misingi lazima ikwekwe sawa kwaajili ya haki na ufanisi.

Mfumo uliopo sasa ni wakujuana tu. Asokujua hakuthamini.

Hivi tukiuliza hao wateule wa CEOs na DEDs, DCs RCs n.k wanateuliwa kwa utaratibu upi ? Kuna jibu lililonyooka?

Kwani watanzania wengine wanawezaje kupata fursa ya kuteuliwa iwapo hawajuani na Rais?

Iwapo hawajuani na walinzi wa Rais?

Iwapo hawajuani na kina Kikwete?

Mamlaka ya uteuzi inawezaje kuwafikia watanzania wote wenye Sifa wakawachuja kwa haki ili kupata wenye kustahili?

Ni watanzania wangangapi wenye Sifa Rais anaweza kuwajua, Kikwete anaweza kuwajua? Watu wa karibu ya Rais kama bodigadi wake, na marafiki wa Rais ?
 
Back
Top Bottom