Kunambi: Wakurugenzi wa Halmashauri wasiwe Wanasiasa, wapatikane kwa mchakato wa ajira

Kunambi: Wakurugenzi wa Halmashauri wasiwe Wanasiasa, wapatikane kwa mchakato wa ajira

Shida mi CCM haitaki hiyo kitu Mkurugenzi akiwa mtumishi wa umma by credentials na asiwe mwanasiasa, matokeo ya uchaguzi yatachakachuliwaje?

Hapa tatizo hatizo halitakuwa ni CCM bali wananchi.
Wananchi pamoja na wawakilishi wao wanapaswa kujitambua na kuweka masala yao na vizazi vya Taifa hili mbele kwa kuweka misingi bora na mifumo bora ya uendeshaji na ufanyajinkazi.
 
Akichangia katika mjadala wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na uwekezaji, Mbunge wa jimbo la Mlinga, Godwin Kunambi amependekeza Wakurugenzi wa halmashauri wasiwe wanasiasa, wapatikane kwa mchakato wa ajira.

Kunambi, ambaye pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, amesema “nchi iliyobaki inateua wakurugenzi (local government directors) ni Tanzania peke yake”

Amesema katika nchi nyingine kama vile Afrika Kusini, ni lazima watu wa cheo hicho wanapitia mchakato wa ajira.

Nchini Tanzania, kwa mujibu wa sheria, Wakurugenzi wa halmashauri za mamlaka ya serikali za mitaa wanateuliwa na Rais.

Kunambi amesema kama taifa Watanzania inabili wabadidi fikra.

C.E.Os wa taasisi za umma wote wapatikane kwa Mtindo huo.

Hata wakuu wa idara, wakuu wa Wilaya , mikoa.

IGP, Jaji Mkuu n.k
 
Akichangia katika mjadala wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na uwekezaji, Mbunge wa jimbo la Mlinga, Godwin Kunambi amependekeza Wakurugenzi wa halmashauri wasiwe wanasiasa, wapatikane kwa mchakato wa ajira.

Kunambi, ambaye pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, amesema “nchi iliyobaki inateua wakurugenzi (local government directors) ni Tanzania peke yake”

Amesema katika nchi nyingine kama vile Afrika Kusini, ni lazima watu wa cheo hicho wanapitia mchakato wa ajira.

Nchini Tanzania, kwa mujibu wa sheria, Wakurugenzi wa halmashauri za mamlaka ya serikali za mitaa wanateuliwa na Rais.

Kunambi amesema kama taifa Watanzania inabili wabadidi fikra.

Tanzania tumechelewa sana, Sijui hata Dunia inatuonaje?! 🤔🤔🤔

Najiuliza inamaana ofisi ya CAG imeshawahi kushauri jambo hili?
Je wao hawaoni kuna shida kubwa kwenye mfumo wa teua ?
 
CCM hawawezi kukubali. Kuwa na vyeo vingi vya kuteuliwa maana yake makada wanakuwa na pa kuwekwa. Makada wakiachwa wazagae kitaa ni tatizo.
 
Wakurugenzi wa sasa wanafanya kazi na kusikiliza wanasiasa waliowateua, ila wakianza kuajiriwa kwa sifa zao bila siasa ,na waajiriwe na wananchi na madiwani wao sio wizarani au Lumumba, total control from kuajiri, auditing, kushtaki mpaka kufukuza itoke hapo hapo panapohusika
 
Hata na wabunge pia waajiriwe kwa uwezo wa elimu na si siasa

Kwa kweli kusema Eti ajue kusoma na kuandika pia imebaki Tanzania peke yake. 🤔🤔

Unaweza kuzani kama kusadikika kumbe ni uhalisia .

Mbunge minimum awe graduate ambae hajaungaunga.
 
Kwa kweli kusema Eti ajue kusoma na kuandika pia imebaki Tanzania peke yake. 🤔🤔

Unaweza kuzani kama kusadikika kumbe ni uhalisia .

Mbunge minimum awe graduate ambae hajaungaunga.
Hamna nchi duniani ina mpanmtu wadhifa yet kuajiri kwa kusoma na kuandika. Ni TZ Pekee tu
 
Hapa tatizo hatizo halitakuwa ni CCM bali wananchi.
Wananchi pamoja na wawakilishi wao wanapaswa kujitambua na kuweka masala yao na vizazi vya Taifa hili mbele kwa kuweka misingi bora na mifumo bora ya uendeshaji na ufanyajinkazi.
Hilo kundi la wawakilishi waondoe, hao kwa TZ siyo sehemu ya wananchi na hawapo kwa maslahi ya wananchi, japo hutumia wananchi kwa kuwahadaa kana kwamba wapo kwa ajili ya wananchi, ila ukweli hawapo kwa ajili ya wananchi. Kama mbunge anashinda ubunge kwa tamko la Rais na hakuna anayehoji hapo mbunge anawajibika kwa wananchi au kwa Rais?
 
Hata mkuu wa majeshi kwa mujibu wa sheria anateuliwa na rais, lakini siamini kama rais anaweza kukubaliwa kumteua koplo kuwa mkuu wa majeshi.

Kinachofanyika kwa sasa ni sawa na kumteua koplo kuwa mkuu wa majeshi, na utaratibu uliozoeleka ambao ilikuwa kumpandisha daraja mmoja wa wakuu wa idara ulikuja kuvurugwa na kikwete.

Kabla ya kikwete wakuu wa idara (hasa maofisa mipango/wachumi) ndio walikuwa na nafasi kubwa kuwa wakurugenzi.

Leo mtu hana uzoefu wa kazi hata miaka miwili unampa ukurugenzi, what do you expect!
Kuna kadada kalikuwa muuza "vitumbua maarufu" leo ni mkurugenzi mitaa flani.... hopeless state
 
WALE NEVER WALE WANA KAZI MAALUM MKUU KUSHUGULIKIA ..........
 
Ukisema aliyevuruga ni Kikwete unamuonea bure. Aliyevuruga ni mtangulizi wake kwa zile tumbua tumbua zake na kuanza kuweka wateule wasiokuwa na sifa
Umevurugwa. Siyo bure. Hebu tutajie huyo mtangulizi wa Kikwete aliyekuwa anatumbuatumbua hovyo ili kuwaweka ndugu zake wasio na sifa.
 
Back
Top Bottom