Kunambi: Wakurugenzi wa Halmashauri wasiwe Wanasiasa, wapatikane kwa mchakato wa ajira


NIONGEZE NA YANGU
WAKUU WA WILAYA NA MIKOA WASIWE WANA SIASA NA WASIWE NA VYAMA

AMA LAH

KUWE NA EQUALITY KATIKA TEUZI KUWE NA BALANSI SIO NCHI NZIMA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA WANAKUWA WATU WA SISIEMU TU
 
Ni ujuha kutozungumzia ukweli na uhalisia kisa tu uliwahi kuwa mnufaika wa jambo linlotakiwa kubadilishwa.

Kongole kwake Kunambi kwa kuliona na kulisema hili la "vilaza" wanaoitwa DEDs.
 
CCM hawawezi kukubali. Kuwa na vyeo vingi vya kuteuliwa maana yake makada wanakuwa na pa kuwekwa. Makada wakiachwa wazagae kitaa ni tatizo.

Wananchi wanapaswa kuanza kujitambua wasioelekeshwe na chama chochote cha kisiasa.
Misingi lazima ikwekwe sawa kwaajili ya haki na ufanisi.

Mfumo uliopo sasa ni wakujuana tu. Asokujua hakuthamini.

Hivi tukiuliza hao wateule wa CEOs na DEDs, DCs RCs n.k wanateuliwa kwa utaratibu upi ? Kuna jibu lililonyooka?

Kwani watanzania wengine wanawezaje kupata fursa ya kuteuliwa iwapo hawajuani na Rais?

Iwapo hawajuani na walinzi wa Rais?

Iwapo hawajuani na kina Kikwete?

Mamlaka ya uteuzi inawezaje kuwafikia watanzania wote wenye Sifa wakawachuja kwa haki ili kupata wenye kustahili?

Ni watanzania wangangapi wenye Sifa Rais anaweza kuwajua, Kikwete anaweza kuwajua? Watu wa karibu ya Rais kama bodigadi wake, na marafiki wa Rais ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…