Kundi kubwa la watanzania wanao ishi maisha standard ya uhakika ni waajiriwa, wafanyabiashara wengi hali ni mbaya

Kundi kubwa la watanzania wanao ishi maisha standard ya uhakika ni waajiriwa, wafanyabiashara wengi hali ni mbaya

Wafanyabiashara Wana hela sana mfanyabiashara mmoja unaweza kukuta anatengeneza faida ya million 30 hapo kariakoo kwa mwezi unazani hiyo ni mishahara ya wafanyakazi wangapi
 
Wafanyabiashara Wana hela sana mfanyabiashara mmoja unaweza kukuta anatengeneza faida ya million 30 hapo kariakoo kwa mwezi unazani hiyo ni mishahara ya wafanyakazi wangapi
Ni kweli wana pesa na ndio wenye utajiri mkubwa, wapo wanaopiga milioni 30 daily,

"LAKINI NI WACHACHE"

Kwa mazingira yetu mfanyabiashara anaepiga pesa ndef inabidi alidhibiti soko au kuwe na kikundi cha wafanyabiashara wachache kulidhibiti soko kwa kuwaminya wafanya biashara wengine wengi wasipate channel

Ukiwa kwenye hao wengi waliominywa ni ngumu kutoboa kwa mazingira ya hapa bongo yaliyojaa umafia, rushwa, siasa, nk.
 
Kuporomoka ghorofa kariakoo kutafilisi wengi
 
Nimewahi kuajiriwa na nimewahi kufanya biashara.
Nilikaa kwenye ajira miaka saba,sikuweza kuwa hata na nyumba ya kuishi zaidi ya kupanga na kuhangaika na kodi za nyumba.
Nilipoacha kazi na kuwa committed na michongo yangu kitaani saizi nina nyumba yangu nzuri tena ya kisasa,nimejenga kwa nguvu zangu bila hata mkopo.
Hapa nilipo sidaiwi hata songesha.
Nilipokua mfanyakazi kila siku nilikua napigiwq simu za kudaiwa.
Ajira ikusaidie kupata mtaji ili baadae uwe mfanyabiashara nawe uajiri.
Ukijiona wewe ni smart kazini na unasifiwa lakini huwezi kumanage hata biashara ya mtaji wa milioni mbili ya kwako jua umefeli.
Changamoto za biashara ni kuwa unakua huna uhakika wa kipato muda wote,kuna kipindi unakua na pesa lakini kuna kipindi unakua huna kabisa tofauti na Maisha ya Mshahara.
Yes ni kweli Tanzania mazingira ya biashara ni changamoto lakini angalau unaweza kuwarithisha watoto wako biashara tofauti na mfanyakazi atawarithisha nini watoto wake?
Binafsi napenda uhuru wa kuamua mambo yangu(own boss),niamue ratiba zangu,nisafiri,n.k
Mfanyakazi unapewa 28 days za rikizo tena kama ni private inabidi hizo 28 days usizichukue kwa mfululizo.
Heri nipate pesa ndogo lakini niwe huru,kuliko nipate pesa nyingi kwa manyanyaso makubwa.
Biashara au ajira ni suala subjective na sidhani kama kuna haja ya ku generalize,coz wengine tumepitia yote mawili ajira na biashara.
Yes kuna muda biashara haziendi mpaka unaikumbuka ajira lakini huwezi kunirudisha kwenye ajira kirahisi kwa sasa.
Neno langu sio sheria...
 
Back
Top Bottom