Akilindogosana
JF-Expert Member
- Jan 12, 2020
- 4,303
- 12,679
Habari wakuu.
Siku za karibuni pamekuwa na utapeli wa aina nyingi na aina mbalimbali unaohusiana na fedha. Kama bahati nasibu, kamari, network marketing, pyramid scheme, ponzi schemes, "online business" na aina nyinginezo za utapeli.
Hao matapeli wanakuaminisha kuwa utapata faida kubwa na fedha nyingi harakaharaka. Na wanacheza na akili yako kujiona utakuwa tajiri mkubwa sana ndani ya muda mfupi. Tena watakuaminisha kwa kupitia vibali halali, washindi feki, hata matangazo mengi sana na mbinu nyingi sana kushawishi watu. Kwa hiyo wanamgeuza mtu anakuwa kama mjingamjinga hivi. Ile ukiwekeza tu 😂 😂😂 hupati kitu 😂😂😂.
Chanzo cha huo utapeli ni sababu mbili
1. Uwepo wa wajinga weeeeeeeengi katika jamii yetu wenye hamu ya utajiri wa haraka. Hapo ndipo matapeli wanacheza na akili za watu kuona watapata utajiri wa haraka sana.
2. Sababu ya pili ni mtu kuwa na hela ambazo hujui ufanyie nini ili zizalishe fedha zaidi. Hapa matapeli wao wanacheza na akili kukuaminisha kuwa utapeli wao ni uwekezaji utakao kupa faida tena wanasema hauna risk kabisa 😂😂😂. Hii ni kuanzia watu wenye pesa ndogondogo mpaka kubwakubwa. Na unakuta mtu ametapeliwa laki tano, 1m mpaka wengine unakuta kaweka 30m mpaka 100m. Hatimaye pesa inaondoka yote na matapeli.
Sasa ni muda wa watu kutoa ushari kwa watu wa sehemu sahihi ya kuwekeza hela. Ama sivyo matapeli wataendelea kutapeli watu. Na serikali iwafatilie na jeshi la polisi lifatilie matapeli kupitia miamala ya simu, benki na selcom.
Watu wasio na mipango ya pa kuipeleka hela ndio hasahasa wanatapeliwa kwa kutafuta utajiri wa haraka.