Kunena kwa lugha ni nini? Na nini hutokea pale mtu anaponena kwa lugha?

Kunena kwa lugha ni nini? Na nini hutokea pale mtu anaponena kwa lugha?

Afrocentric view

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2022
Posts
1,374
Reaction score
2,280
Wakuu,

Hapa duniani Kuna Imani nyingi, Kuna watu ambao hawaamini Mungu (atheists), Kuna waislam,Kuna wabudha. Kuna wakatoliki,wasabato na Kuna hawa wahusika wenyewe (walokole na wengineo).

Ninapenda kujua mitazamo yenu juu ya Hawa watu kunena kwa lugha.

Je ni Mungu au sio?

A) Wanaosema ni Mungu (walokole nk.)
Mechanism ikoje? Ukiwa unanena unajisikiaje? Je unajielewa unachosema?Nani anacontrol mdomo wako?Unapanga cha kuomba? Kuna faida gani?

B) Wanaosema si Mungu
Mechanism ikoje? Ni kweli wananena au usanii tu? Je nini hufanyika pale? Kwanini walokole wengi waumini wa kawaida tu nao wanene? Kuna siri gani nyuma ya kunena kwa lugha? Je wanajitambua au wanatawaliwa na nguvu nje ya akili Yao? Ni nguvu gani hiyo? Nini huendelea kwenye ubongo wa mtu pale anaponena kwa lugha?(mental state)

Uhakika Bro Mshana Jr Tate Mkuu adriz Che mittoga Walker Water Smotor Surya FaizaFoxy KENZY Mcqueenen Kiranga mwakabonao CAPO DELGADO Blood of Jesus
 
Ninavyojua mimi hawa wanaosema wananena kwa lugha wengi sio kweli maana ukiisoma matendo ya mitume(kitabu) kinaelezea kuhusu kunena kwa lugha na kila mtu alisikia kwa lugha yake!

Sasa hii ya shibhobhobho, shalabhashi! Hata wanenaji hawajui wanaongea nini!
 
B)Wanaosema si Mungu
Ni mfumuko mkubwa wa hisia ndani ya muda mfupi(religious ecstasy) unaosababishwa na hypnosis inayoletwa na ile hali ya umakini kwenye ibada, mchanganyiko wa nyimbo za kuabudu, kusifu na kusali kwa muda mrefu unaleta huo umakini.

Pia kuna tatizo la kiakili linaitwa frontal lobe epilepsy, linasababisha mtu kuhisi mchanganyiko wa hisia nyingi ndani ya muda mfupi, visababishi flani vikiwepo.

Uthibitisho kwamba kunena kwa lugha ni uongo ni kwamba imegundulika wanaonena kwa lugha, yale matamshi wanayotamka yana silabi zinazofanana na lugha zao za kawaida, hivyo sio lugha mpya wanaongea bali wako kwenye hali flani ya kihisia inayofanya washindwe kuongea vizuri.

Nimejaribu kuelezea nnachokijua, mnisamehe vitu vingine sijui kiswahili chake nimeandika hivyo hivyo tu
 
Ninavyojua mimi hawa wanaosema wananena kwa lugha wengi sio kweli maana ukiisoma matendo ya mitume(kitabu)kinaelezea kuhusu kunena kwa lugha na kila mtu alisikia kwa lugha yake!Sasa hii ya shibhobhobho,shalabhashi!Hata wanenaji hawajui wanaongea nini!
Kama sio kweli inamaana ni usanii? Wanapata faida gani kufanya Hivyo?

Maana ingekuwa wachungaji na manabii pekee ndio hunena hapo ingeeleweka, ila unakuta ni watu wa kawaida tu tunaoishi nao mtaani wengine mahouse girl wengine maofisa wakubwa kabisa ila wakifika kanisani wanaongea shashaliboroe chumoirataratetete titititshasha.

Na sio Tanzania tu, ni duniani kote.

Kuna mechanism gani?
 
Kunena kwa lugha si complicated phenomenon kama wengi wanavyodhani.

Ile si lugha yenye mantiki.

Wala hakuna maneno yyte yaliyokubalika na jamii flani au husika.

Kunene kwa lugha kinachofanyika, mtu anakua ameongea maneno mengi kiasi kwamba inafika hatua anatamka tu vitu lakini nia kubwa nikufikisha ujumbe flani kwa sehemu anayotaka kufikisha(wanasema kwa Mungu.. yeye anayaelewa).

Illustration mfano;
Muda huu hapo ulipo unayesoma hii, fikiri labda unatamani kuongea kitu ili ueleweke ila kwasbabuunakosa maneno yakueleweka wewe ropoka ropoka tu, ukiwa na tone ya kumaanisha kama maneno kamili. Huko ndio kunena kwa lugha.

Unafikiri nataka mungu anipe gari. Ila kusema Mwenyezi Mungu nipe gari, unaona ni maneno machache yasiyomtosha. Ndio unaongea maneno kwa kuyasigina nia nikufikisha ujumbe nataka gari.

Asante, ile ni receiving wenzetu wameamua kuitumia tu, haina ubaya wala nini.
 
Ndio wote ni vichaa unakuta mtu kapasa sauti anaongea lugha hata ukimuuliza ume maanisha nini hajui,Huo ni ukichaa bin wendawazimu.
Kwanini ukichaa wao udhihirike hapo tu? Kwann haionekani kwenye maisha mengine ni watu tu wa kawaida, wengine Wana mali nyingi,elimu kubwa mpaka vyeo vikubwa hadi serikalini?

Na kwanini ukichaa wa style moja utokee watu wengi kwa wakati mmoja? Mfano unakuta kanisani watu zaidi ya 50 wote wananena...na hii hutokea duniani kote
 
Unaweza ukawa na elimu, pesa na bado ukawa kichaa,We unavyowaona walokole wako sawa.
Sasa kwanini ukichaa wa style moja utokee watu wengi kwa wakati mmoja? Mfano unakuta kanisani watu zaidi ya 50 wote wananena...na hii hutokea duniani kote.

Na inakuwaje Imani tu ya dini imfanye mtu awe kichaa?
 
Back
Top Bottom