Kunena kwa lugha ni nini? Na nini hutokea pale mtu anaponena kwa lugha?

Kunena kwa lugha ni nini? Na nini hutokea pale mtu anaponena kwa lugha?

Sasa kwanini ukichaa wa style moja utokee watu wengi kwa wakati mmoja? Mfano unakuta kanisani watu zaidi ya 50 wote wananena...na hii hutokea duniani kote.

Na inakuwaje Imani tu ya dini imfanye mtu awe kichaa?
Lazima wawe vichaa kwa sababu wana abudu kitu ambacho si kweli kwao na wengi wao ni matapeli.
 
ni mfumuko mkubwa wa hisia ndani ya muda mfupi(religious ecstasy) unaosababishwa na hypnosis inayoletwa na ile hali ya umakini kwenye ibada, mchanganyiko wa nyimbo za kuabudu, kusifu na kusali kwa muda mrefu unaleta huo umakini....
Hii kidogo inakuja kuja lakini kwanini hii phenomenon haitokei kwenye aspects zingine za maisha kama kusikiliza muziki, kucheza nk?

Kwann iwe kwenye ulokole tu? Mbona dini nyingi wanakaa maakini kwenye ibada mda mrefu na nyimbo za kumsifu na kuabudi zinakuwepo pia
pia kuna tatizo la kiakili linaitwa frontal lobe epilepsy, linasababisha mtu kuhisi mchanganyiko wa hisia nyingi ndani ya muda mfupi, visababishi flani vikiwepo...
Hili tatizo ni common kiasi gani? Kwanini halitokei kwa waislam,wabudha,wayahudi au wasabato?

Inamaana mamilioni kwa mamilioni ya walokole wanaonena kwa lugha Wana hili tatizo?
 
Kwa Ulokole wangu na kumtumikia Mungu kwa miaka 8 Kanisa TAG huku Nyakatuntu Keisho Karagwe.

Kunena kwa Lugha, ni Karama ya Roho Mtakatifu ambayo huitoa kwa mwanadamu kama karama zingine za unabii, matendo ya miujiza na uponyaji, neno la hekima n.k 1 Korintho 12:1-12 inaeleza wazi kuhusu hizo karama.

Kwa sisi TAG katika misingi 16 ya Imani. Kuna msingi wa udhihirisho wa ujazo wa Roho Mtakatifu ambayo ni kunena kwa Lugha. Hili, Paulo na Mitume waluombea na kuonesha kuwa ndio uthibitisho wa ubatizo wa Roho Mtakatifu.

Je lugha inayotamkwa ni ipi? Biblia katika 1 korintho 13:1-2 inaeleza vizuri "kuwa kunena kwa lugha za kibinadamu na za Malaika". Katika Matendo ya Mitume 2, wanafunzi walinena kwa lugha za kibinadamu ikiwa ni ishara ya ujazo wa Roho mtakatifu pia ikiwa ni maandalizi ya kwenda kuhubiri Injili kwa mataifa mbalimbali. Sasa injili imehubiriwa kila Mahali, tunanena kwa lugha za Malaika. Biblia inasema wazi, "mtu anenapo huwa anawasiliana na Mungu wake moja kwa moja" ila inatusisitizia kumuomba Mungu atupe "karama ya kufasiri lugha unenayo"

Nifahamuvyo, kunena kwa lugha mara nyingi huwa ni kwa ajili ya kumsifu, kumshangilia na kumtukuza Mungu. Mara nyingi mtu anenapo hajui nini anachoongea kwani ulimi na akili(Mawazo) yake huwa yameshikwa na Roho wa Mungu. Kunena kunaenda pia na bubujiko la ndani kunakoendana na machozi japo pia mara nyingi Roho ya kunena ile lugha huambukiza kwani nifahamuvyo, kila kanisa lina Malaika wake na ndio maana Yesu aliongea na Malaika wa yale makanisa 7 ya Asia ndogo kwenye kitabu cha ufunuo.
 
Kunena kwa lugha si complicated phenomenon kama wengi wanavyodhani.
Ile si lugha yenye mantiki.
Wala hakuna maneno yyte yaliyokubalika na jamii flani au husika...
Baadhi ya walokole niliowauliza hili swala wanasema wanapokuwa wananena hata hawajitambui wanaomba nini.

Yaani sio kwamba wanafupisha maneno kama unavyosema bali ni kama wanaingiliwa na nguvu inayoongea mambo ambayo hata wao hawayaelewi, kuyaelewa ni mpaka baadae waombe Mungu awafunulie.
 
Wakuu.
Hapa duniani Kuna Imani nyingi, Kuna watu ambao hawaamini Mungu (atheists), Kuna waislam,Kuna wabudha,Kuna wakatoliki,wasabato na Kuna hawa wahusika wenyewe (walokole na wengineo)...
Ni upotoshaji tu na ukanjanja wa kuwapiga noti watu wenye imani haba na kutoelewa mafundisho yaliyoandikwa kwenye Biblia.

Wajanja ndiyo hupita humo na kukunja noti kiulaini kabisa kupitia uposhaji unaofanywa na makanisa ya leo yanoyojiita ya kiroho.

KUNENA KWA LUGHA KULIANZAJE KIHISTORIA?

Ukisoma kwenye Biblia kunena kwa lugha kulitokea siku ya Pentekoste ( Yaani siku ya Hamsini baada ya Kupaa kwa Yesu).

Katika maandiko tunaona kuwa ujumbe wa neno la Mungu ulikuwa umepokelewa katika jamii moja lakini dhima ilikuwa ni ujumbe huu usambae Ulimwenguni kote. Yaani kwa mfano, tuchukulie kwamba ujumbe wa neno la Mungu ulifikia Tanzania ambapo lugha inayotumika kwa mawasiliano ni Kiswahili, lakini ujumbe wa neno la Mungu ulitakiwa ufike Djibout, Malawi, DRC, Ethiopia na kwingineko Ulimwenguni ambapo hata hawakijui Kiswahili.

KULITOKEAJE?

Kunena kwa lugha kulitokea kwa wale Mitume sio kwa kubadili na kuacha kutumia lugha zao za asili au walijifunza lugha za Mataifa waliyoenda kuhubiri, la hasha, bali walitumia lugha zao za asili lakini waliokuwa wakihubiriwa waliupata ujumbe kwa kuusikia kwa lugha zao wenyewe.

Yaani tukirejea katika huo mfano hapo juu, ni kwamba, wewe Petro Mtanzania ukiwa unazungumza Kiswahili chako sanifu kabisa lakini unawahubiria watu wa DRC na wao wanasikia ujumbe unaowapa kupitia lugha wanayoielewa wao mfano, Kilingala, au Kifaransa.

Kwahiyo ni kama leo hii baada ya kuja teknolojia Uhutubie pale UN lakini wawakilishi wa Oman wanakusikia unaongea Kiarabu kilichonyooka, au Ujumbe kutoka Rome unaona unagonga kile Kilatini chenyewe kabisa, au wajumbe kutoka Brazil wanaona unakibomoa kireno ipasavyo.

Na kwa njia hiyo ndivyo ujumbe wa neno la Mungu ukaweza kuenea Ulimwenguni kote na maandiko kuweza kutafsiriwa katika lugha mbalimbali kulingana na sehemu ujumbe wa neno la Mungu unapelekwa

UPOTOSHAJI WA MAKANISA YA LEO YANAYOJIITA YA KIROHO:
Viongozi wengi wa hayo Makanisa hawaijui dhana ya kunena kwa lugha kwa mapana yake, na kama wanafahamu basi wanatumia ujinga wa waamini wao kufanya upotoshaji wa Makusudi kwa Maslahi yao binafsi.

Ukienda kwenye Makanisa ya leo yanayojiita ya kiroho yamejaa upotoshaji juu ya dhana hii ya kunena kwa lugha kwa kukuta hao viongozi wa makanisa hayo wanaongea lugha ambazo hata waumini wao hawazielewi nini wakimaanisha au ujumbe gani unatolewa kupitia matamshi hayo.

Nachelea kusema usikute hata wao hawajui ni kitu gani wanaongea na wala hawajui hiyo lugha gani wanatamka.

NB: Kunena kwa lugha sio kama kupandisha mashetani na kuongea vitu visivyoeleweka, bali ni njia iliyowatukia Mitume katika zama hizo ili neno la Mungu liweze kufika mahali pote Ulimwenguni.

Kwa ulimwengu wa sasa sidhani kama hiki kitu bado ni applicable.
 
Hiyo ni dalili kubwa ya magonjwa ya akili inaitwa HALLUCINATION
Ukiona unasikia sauti za ajabu pasi na kujua nini kinazungumzwa basi ni ndio kiataalamu inaitwa Shizophrrnia
Kimsingi asilimia kubwa ya walokole hamnazo kuna mmoja hapa jirani alizimia kisa hajala siku 3 kisa yesu kamtokea kamwambia afunge siku 5 jiulize wee unamjua yesu kweli kama sio ukichaaa ni nini yaan usile siku 5 hawa walokole wana magonjwa ya akili na asilimia kubwa ni wanawake
 
Wewe una mtazamo gani?
Kusema Ukweli nimekuwa na mitazamo mingi tofauti iliyobadilika badilika kuhusiana na hili swala mpaka nimefika hatua nimekubali kuwa sijui.

Kutoka kuamini na kujaribu mwenyewe kunena nikashindwa, mpaka kuamini sio karama yangu, kuamini haiwezekani, kuamini ni usanii,kuamini ni ukichaa nk.

Mtazamo wangu wa Sasa ni kuwa sijui lolote, ndomaana nmekuja kuuliza huku.
 
Hii kidogo inakuja kuja...lakini kwanini hii phenomenon haitokei kwenye aspects zingine za maisha kama kusikiliza muziki, kucheza nk.? Kwann iwe kwenye ulokole tu? Mbona dini nyingi wanakaa maakini kwenye ibada mda mrefu na nyimbo za kumsifu na kuabudi zinakuwepo pia
hofu ya moto wa milele inaleta hizo hisia, pia taratibu za ibada za walokole zinafanana na saikolojia ya 'hypnosis'

kiufupi hypnosis ni hali ya juu ya umakini inayosababisha mtu kufikiri na kuhisi kwa namna tofauti
Hili tatizo ni common kiasi gani? Kwanini halitokei kwa waislam,wabudha,wayahudi au wasabato?
Inamaana mamilioni kwa mamilioni ya walokole wanaonena kwa lugha Wana hili tatizo?
hata kama hili tatizo watu wengi hawana, lakini linaweza kua sababu kwa walokole wenye tatizo hilo
 
Hii lugha inakujaje? Mtu anakuwa anajitambua anachosema?
Hapana unaingia kwenye ulimwengu wa roho unapokuwa umezama kwenye maombi.. Hapo inayoongea ni roho sio wewe na kuna vitu unafunuliwa .. Unakuwa kwenye ulimwengu tofauti mno na kujikuta uko mwepesi mno kwenye ulimwengu juu ya ufahamu wako.. Yaani unakuwa umesimama pembeni unajiangalia.. Ni ngumu kuelezea kwa hakika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusema Ukweli nimekuwa na mitazamo mingi tofauti iliyobadilika badilika kuhusiana na hili swala mpaka nimefika hatua nimekubali kuwa sijui. Kutoka kuamini na kujaribu mwenyewe kunena nikashindwa, mpaka kuamini sio karama yangu, kuamini haiwezekani, kuamini ni usanii,kuamini ni ukichaa nk.

Mtazamo wangu wa Sasa ni kuwa sijui lolote, ndomaana nmekuja kuuliza huku.
Ngoja nifikirie kwanza.
 
Ninavyojua mimi hawa wanaosema wananena kwa lugha wengi sio kweli maana ukiisoma matendo ya mitume(kitabu)kinaelezea kuhusu kunena kwa lugha na kila mtu alisikia kwa lugha yake!Sasa hii ya shibhobhobho,shalabhashi!Hata wanenaji hawajui wanaongea nini!
Rikarobo shabababa
 
Hapana unaingia kwenye ulimwengu wa roho unapokuwa umezama kwenye maombi.. Hapo inayoongea ni roho sio wewe na kuna vitu unafunuliwa .. Unakuwa kwenye ulimwengu tofauti mno na kujikuta uko mwepesi mno kwenye ulimwengu juu ya ufahamu wako.. Yaani unakuwa umesimama pembeni unajiangalia.. Ni ngumu kuelezea kwa hakika

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hiyo haikuwa dhana halisi ya kunena kwa lugha, na ukitaka kujua kuwa hawa wajuba ni wababaishaji kwanini wote wawe wanatamka maneno yaleyale au yanakaribisna?

Ingekuwa ni kweli tungekuwa tunawasikia kwa lugha tofauti mara leo Mwamposa kakibomoa Kichina, hatujakaa vizuri Lusekelo anatapika Kireno kabla hatujapoa Mwingira anatupeleka Moscow anabonga Kirusi, wakati tunajiuliza nchi imekumbwa na jambo gani huku Gwajima anatiririka Unyola wa kufa mtu mpaka tujihisi labda tupo Madrid.
 
Back
Top Bottom