Ninapenda kujua mitazamo yenu juu ya Hawa watu kunena kwa lugha
Chief mleta mada, Afrocentric
Mimi sipo mbali na maelezo ya
mshamba_hachekwi hayo yaliyohusisha hypnosis na ecstacy.
Zamani hizoo watu ili waongee na Mungu huku Afrika na kwingineko kama Amazon (huku bado wanaendelea nnaona). Lakini pia ma Rastafarians kuna kitu wote hawa wanafanya kinashabihiana;
Wanatumia kilevi fulani kitakatifu 'sacred' kuweza kujiweka hali ya kuishusha akili ya mbele yenye kujizuia na kujitambua na kuruhusu akili na sehemu nyingine za ubongo zijitawale. Wanaruhusu hisia na subconscious mind vijiachie.
Pombe inaweza kusaidia kufanikisha hilo
Bhangi husaidia kufanikisha
Uyoga, mizizi, majani na hallucinogens mbalimbali husaidia sana kufanikisha hilo.
Pia sherehe hizi huambatana na ngoma na sherehe na kufunga vitakavyosaidia kuwahisha mchakato na kuushikilia 'maintain it'. Hao wanaolewa kwanza huweza kukaa hata siku tatu wanawasiliana tu na roho.
Subconscious mind ndiyo huhusika zaidi ndiyo maana wanawasilisha kihisia mawazo yao ya ndaaaani kabisa (communicating deeply desires with ones' God) na tuseme tu kuhusu kusikia Mungu anawasikia na kuwaelewa ile deeeply kabisa. Hapo zinawasiliana will kwa Will, utashi kwa Utashi mkuu.
Ni kwa nini basi maneno hayaeleweki ama kukosa muunganiko maalumu. Kumbuka cerebrum ndiyo hutumia mantiki kuwasilisha wazo. Lakini ikizimwa data au ikafifia basi wazo, haja na hisia huwasilishwa kwa namna ambayo mwanadamu mwingine hatang'amua maana kanuni za jamii za lugha hazijatumika hakuna tena inhibition kamilifu.
Turudi kwa walokole; walokole hunena kwa lugha, huongea hisia na haja zao za ndani kabisa. Ni kweli wanasali na wanawasilisha mawazo yao ya ndani kwa Mungu wake. Man to God.
Wao wamejifanyia ama self hypnosis ama kiongozi wao mwenye mamlaka juu yao kawahakikishia kwamba hicho kitu kinawezekana(wameunda constructs kwamba ni kweli mtu anaweza ongea na Mungu kwa njia hizo), na pia wamesaidiwa na nyimbo na vyombo ngoma na muziki kuifikia hali hiyo. Ni kuongea na Mungu as far as hao wawili wanahusika yaani subconscious ya mtu na superconscious ya Mungu.
Bandugu, chukulieni tu kama mama na mwanaye. Mtoto akikua kidogo anaweza sema 'mama, taka, kula' akaeleweka na mama ake na watu wote.
Au akalia na mama ake akaelewa na watu wachache wakaelewa.
Au akazubaa tu na hapo ni mama ake anauemjua vizuri, aliyemlea ndo atamuelewa hisia zake. Mama anaweza kujua mtoto kilio hiki anaumwa, au amechoka, au ni usingizi, njaa etc.... same concept